Wednesday, 28 May 2014

eo ni Kumbukumbu ya mwaka 1 toka Albert Mangwea afariki.

Ngwea
Ilikua ni mchana May 28 2013 ndipo zilipotoka taarifa ambazo kulingana na ukubwa wa jina la mangwea Tanzania hakuna aliyekua tayari kuamini kama ni kweli Mangwea kafariki dunia,zilianza taratibu za kuthibitisha taarifa hizi ambapo baadae ilithibitika kweli Mangwea amefariki dunia.
Mpaka sasa ripoti kutoka hospitali ya South Africa familia haijawa tayari kuiweka wazi,kutoka Morogoro nimepata taarifa kuwa leo kutakuwa na ibada asubuhi kisha jioni kutakua na tamasha la kumkumbuka Mangwea ambapo itakua ni kumchangia mama yake Mangwea na imeandaliwa na baadhi ya wadau wa Morogoro na kupata baraka toka kwa Familia ya Mangwea.

Wachezaji 2 wa Ujerumani wapata ajali nchini italy.

Wachezaji 2 wa Ujerumani katika ajali


Wachezaji 2 wa Ujerumani wajeruhiwa Italia
Wachezaji wawili wa timu ya taifa ya Ujerumani itakayoshiriki kombe la dunia hukop Brazil mwezi ujao
wamenusurika baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani wakiwa Italia.
Benedikt Hoewedes na Julian Draxler walikuwa ndani ya magari tofauti katika hafla iliyoandaliwa na kampuni ya magari ya Mercedes .
Moja ya magari yaliyohusika iliwagonga wapita njia wawili karibu na makahawa wanakoiswahi timu ya taifa ya Ujerumani.
Mwathiriwa moja anauguza majeraha mabaya .

Wachezaji 2 wa Ujerumani wajeruhiwa Italia
Ajali ya pili ilimhusisha dereva wa mbio za magari ya langalanga wa Mercedes , Nico Rosberg.
Hoewedes na Draxler ni wachezaji wa timu ya Schalke 04 walioitwa katika timu ya taifa.
Wenyeji wao kampuni ya Mercedes-Benz imetoa taarifa kusema kuwa itashirikiana na maafisa wa polisi kutathmini kilichotokea .
Timu hiyo ya Ujerumani inatarajiwa kuendelea na kambi ya mazoezi katika mji wa Tyrol Kusini mwa Italia hadi juni mosi. .

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...