Story za watu weusi kuuawa Marekani iligusa wengi, mmoja ya waliouawa ni kijanaFreddie Gray ambaye aliuawa mikononi mwa Polisi kwenye mji wa Baltimore, Marekani.. leo iko hii nyngine inayohusu kisa cha mwanamke kunyanyaswa.
Monday, 8 June 2015
baada ya benitez kuchaguliwa kua kocha mpya wa madrid Tofauti zaanza kati yake na uongozi,
.
Zikiwa zimepita siku tano pekee tangu Rafael Benitez alipotambulishwa kuwa kocha mpya wa Real Madrid kufuatia klabu hiyo kumfukuza kazi Mtaliano Carlo Ancelotti , tayari kocha huyu mpya ameanza kutunishiana misuli na uongozi wa klabu hii ya kifalme yenye maskani yake katikati ya mji mkuu wa Hispania .
Rafa Benitez kwa mujibu wa ripoti zilizoibuka hii leo ametofautiana maoni na bosi wake ambaye ni rais wa klabu hiyo Florentino Perez juu ya mshambuliaji atayaesajiliwa na klabu hiyo ili kuimairisha kikosi chake cha msimu wa mwaka 2015/2016.
Gazeti moja la kila siku nchini Hispania la habari za michezo limeripoti kuwa Rafael Benitez anataka kumrudisha mshambuliaji aliyeuzwa toka Madrid Alvaro Morata baada ya kuridhishwa na kiwango alichokionyesha msimu huu .
Matamanaio haya ya Benitez kumsajili Alvaro Moratta yanakwenda kinyume na Perez ambaye anataka kumsajili Sergio Aguerro ili aweze kuiongoza safu ya mashambulizi ya Real Madrid kwa ajili ya msimu ujao .
Perez amekuwa na utamaduni wa kusajili wachezaji nyota wenye majina makubwa kwa karibu kila msimu ili kuifanya klabu hiyo itengeneze fedha kutokana na biashara inayofanyika nje ya uwanja .
Florentino Perez na kocha mpya Rafa Benitez wameripotiwa kutofautiana juu ya mshambuliaji wa kumsajili.
Hata hivyo bado haijafahamika kama tofauti hii inaweza kuwa na athari yoyote kwenye ufanyaji kazi wa Rafa Benitez lakini itakuwa ishara ya kwanza ya aina ya mazingira ambayo anatajia kuyakuta akiwa ameanza kazi rasmi kama kocha wa moja kati ya klabu kubwa kuliko zote duniani .
Picha 6 za jumba la Asamoah Gyan lenye thamani ya bil 6. tazama uone jinsi michezo ilivyo na utajiri wa milele duniani.
Mshambuliaji wa Klabu ya Al Ain ambaye analipwa kiasi cha $200,000 kwa wiki amenunua jumba hilo lenye thamani inayokadiriwa kufikia dola millioni 3 za kimarekani ambazo zinafikia billioni 6 za kitanzania.
Jumba hilo lipo maeneo ya McCarthy Hills enclave jijini Accra lina baa mbili, bwawa kubwa la kuogelea. Lina ghorofa tatu zilizotengenezwa kwa muundo wa kipekee kila mmoja huku vifaa vya ulinzi vikiwa vya kisasa ikiwepo milango na madirisha yenye bullet proof.
Kwa mujibu taarifa za vyombo vya habari vya Ghana, Gyan aliinunua nyumba hiyo aliyoikarabati alipozuru nchini humo mwezi April wakati alipoenda kutazama pambano la masumbwi kati Emmanuel Tagoe na Jobert Delos Reyes.
fahamu alichokifanya Davido jana jumapili huko nigeria.historia ya kishujaa ndio hii duniani kote.
Posted by: Jesca TZA
June 8, 2015Entertainment, General News
Jana jumapili staa wa Nigeria Davido alihitimu shahada yake ya mambo ya muziki katika chuo kikuu cha Babcock nchini Nigeria.
Superstar huyu kutoka nchini Nigeria amehitimu degree yake ya elimu kutoka chuoBabcock University nchini Nigeria kwenye kitengo cha Muziki.
Davido aliamua kushare baadhi ya picha zake wakati akihitimu masomo yake ambapo wanafamilia akiwemo baba yale mzazi Deji Adeleke na familia yake waliweza kuhudhuria wakiwemo wasanii wenzake kama Don Jazzy.
G7 yatishia kuiongezea Urusi vikwazo vya kiuchumi.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa, viongozi wa mataifa saba yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi Duniani-G7, wamekubaliana kuwa vikwazo dhidi ya Urusi vinafaa kuendelea.
Bi Merkel amesema hadi pale muafaka wa kukomesha mapigano nchini Ukraine utakapoheshimiwa vikwazo sharti ziendelee.
Akiongea katika siku ya mwisho ya mkutano wa siku mbili, Merkel amesema kuwa mataifa ya G7 yalikuwa tayari kuzidishia Urusi vikwazo zaidi, iwapo hali ingeruhusu.
Kuhusu mzozo wa kifedha unaokumba Ugiriki, Bi Merkel, alionya kuwa muda uliosalia kabla makubaliano hayajatiwa sahihi ni mchache mno.
Alishauri Ugiriki kuchukua hatua madhubuti ilikunusuru sarafu ya taifa hilo.
Viongozi hao wanafanya mazungumzo katika siku ya pili ya mkutano mkuu, wenye nia ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, huku pia swala la kuongezeka kwa makundi yenye itikadi kali likijadiliwa.
Bi Merkel pia amewataka wanachama wa G7 kuchangia hazina ya kuyasaidia mataifa maskini ambayo yanaathirika na mabadiliko ya hali ya anga.
jinsi ya kuepuka kansa ya matiti kwa wasichana na wanawake wote. soma hii na uzingatie .
Wanawake wa kati ya umri wa miaka 50 mpaka 69 wanaofanyia uchunguzi matiti yao wanapunguza hatari ya kupata saratani ya matiti kwa asilimia 40 ikilinganishwa na wanawake ambao hawafanyi uchunguzi.
Ripoti ya kimataifa kutoka Taasisi ya kimataifa ya utafiti kuhusu maradhi ya Saratani, IARC imesema kuwa wanawake wanaochunguzwa hupunguza hatari ya kupata ugonjwa huo.
BBC ilizungumza na Dokta Catherine Nyongesa tabibu wa maradhi ya saratani
Subscribe to:
Posts (Atom)
CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA
Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...

-
Tuzo za VMA 2014 zimefanyika na mastaa wengi walifika kwenye hilo tukio. Listi ya mastaa hao iliongozwa na familia ya Jay Z na Beyon...
-
Luca Modric mchezaji bora wa mwaka wa FIFA Wameamua kumpa,ni baada ya kumdhurumu tuzo yake ya msimu wa 2009/10,mwaka huu wameona ai...
-
Mlinda mlango wa Derby Country akipangua mkwaju wa Phil Jones Timu ya DERBY COUNTY inayonolewa na nyota wa zamani wa CHELSEA, FRANK LAM...