Monday, 22 February 2016

Kizza Besigye kukamatwa leo,rais mstaafu Obasanjo amesema Uganda haipaswi kuzuia upinzani,


Image captionUganda haipaswi kuzuia upinzani, Obasanjo
Aliyekuwa rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, ametaka pande zote pinzani katika uchaguzi wa Uganda kujiepusha na matamshi ya uhasama.
Obasanjo ambaye aliongoza ujumbe wa Jumuiya ya madola uliokuwa ukiangalia vigezo vya kidemokrasia katika uchaguzi uliokamilika nchini Uganda amewashauri viongozi wa uganda kujiepusha na makabiliano na migongano baina yao.
Obasanjo alisema''Uhuru wa kujieleza kutengamana na kuwasilana na umma wa kila kiongozi sharti ulindwe na kama kuna vizuizi dhidi ya kiongozi yeyote lazima iondolewe mara moja''
Image captionUganda haifai kuwazuia viongozi wa upinzani ,Obasanjo
Obasanjo aliyasema hayo bila ya kumtaja kiongozi wa upinzani Kizza Bisigye ambaye kwa sasa amezuiliwa nyumbani kwake.
Aliongezea kuwa ''dosari zilizoshuhudiwa katika uchanguzi mkuu umekuwa na madhara mabaya kwa matokeo ya ukweli haki na uwazi wa uchaguzi huo'' , lakini amesisitiza tofauti kati ya utawala na upinzani zinahitajika kusuluhiswa kupitia mazugumzo.''
Kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda alikamatwa alipokuwa akijaribu kuondoka nyumbani kwake.
Image captionKiongozi huyo wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda alikamatwa
Amekuwa kwenye kizuizi cha nyumbani tangu Ijumaa wakati polisi walimtuhumu kupanga kujitangazia matokeo.
Wakili wake amethibitisha habari za kukamatwa kwake.
Awali kulikuwa na habari kwamba angefika makao makuu ya Tume ya Uchaguzi kuitisha matokeo rasmi ya kina ya uchaguzi wa urais

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...