Saturday, 11 June 2016

Tamko la Chadema kuhusu mikutano ya hadhara hii hapa.


Image captionWafuasi wa Chadema
Chama cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA kimesema kuwa kitaenda mahakamani kupinga tangazo la hivi karibuni la polisi kwamba mikutano yote ya hadhara inyofanywa na upinzani imepigwa marufuku.
Kulingana na gazeti la Citizen nchini Tanzania, uamuzi huo wa kwenda mahakamani ulitangazwa na naibu katibu mkuu wa CHADEMA Saumu Mwalimu huko Mwanza.
Inajiri baada ya mkutano wa siku mbili wa maafisa wakuu wa upinzani wakiongozwa na mwenyekiti wa kitaifa Freeman Mbowe.
Gazeti hilo limesema kuwa maafisa wa Chadema na wabunge kadhaa wako katika mji huo wa Ziwa baada ya kuzuiliwa kufanya mkutano katika eneo la Kahama siku mbili zilizopita.
Maafisa wa polisi walisema kuwa mkutano huo ulioshirikisha chama cha ACT-wazalendo kinachoongozwa na Mbunge wa kigoma Zitto Kabwe utapigwa marufuku.
Na siku ya Ijumaa Bw Malimu amesema kuwa watawasilisha kesi ya kutaka kubadilisha uamuzi huo wa polisi katika mahakama kuu Mwanza.

Watu zaidi ya 12 wauwa huko Damascus


Image copyrightAFP GETTY
Image captionDamascus
Watu 12 wameuawa katika milipuko miwili ya mabomu viungani mwa mji wa Damascus, katika eneo la madhabahu muhimu ya Waislamu wa madhehebu ya Shia.
Image copyrightREUTERS
Image captionShambulio la Damascus
Shirika la habari la kitaifa linasema mlipuko mmoja umetekelezwa na mshambuliaji wa kujitolea muhanga.
Image copyrightREUTERS
Image captionDamascus
Mlipuko wa pili umetokana na bomu lililotegwa ndani ya gari.
Image copyrightAFP
Image captionDamascus
Watu wawili wameuawa karibu na madhabahu ya Sayyeda Zeinab yanayoheshimiwa na Washia kote ulimwenguni.
Image copyrightAP
Image captionDamascus
Eneo hilo limekuwa likilengwa kwa mabomu na wapiganaji wa Islamic State.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...