Wednesday, 29 April 2015

list ya wa wakali wa kupambana katika tuzo za kili music award hawa hapa.tazama hapa ujue wa kumpa kura ni nani.

RED3-Red_Carpet_lights_Large_0
mambo yameiva hapa , mchuano huo hapo.
IIIIIIIVVVI

Mawasiliano ya mitandao yakatwa hivi punde huko Burundi . HII NI EXCLUSIVE.

Mitandao ya kijamii
Utawala nchini Burundi umekata mawasiliano ya mitandao ya kijamii kupitia kwa simu ya mkononi mawasiliano ambayo wamekuwa wakitumia kupanga maandamano ya kumpinga rais Pierre Nkurunziza.
Mamia ya waandamanaji wako barabarani kwenye mji mkuu wa Buruni ,Bujumbura kwa siku ya nne ya ghasia kutokana na uamuzi wa rais kwa kuwania muhula wa tatu.
Maandamano Burundi
Mwandishi wa BBC nchini Burundi anasema aliwaona waandamanaji katika eneo la Musaga wakiinua mikono kuwaonyesha polisi kuwa hawakuwa wamejihami.
Wanasema kuwa wanazuiliwa kuondoka na kuwa chakula hakifiki eneo hilo.

police wa marekani wana kibarua kigumu cha kuwatuliza watu kama hawa walio tayari kufa kama mwenzao.

Maelfu ya maafisa wa polisi nchini Marekani wameamriwa kuwasaidia maafisa waliozingirwa mjini Baltimore, baada ya ghasia zilizosababishwa na waandamanaji waliojawa na hasira, kufuatia kifo cha Mmarekani mweusi.
Muandamanaji akiwafokea polisi waliokuwa wanajaribu kudhibiti hali mjini Baltimore
Muandamanaji akiwafokea polisi waliokuwa wanajaribu kudhibiti hali mjini Baltimore
Watu 27 wametiwa nguvuni huku polisi 15 wakijeruhiwa wakati waandamanaji hao wengi wao wanafunzi waliokuwa wanarusha mawe na kupora biashara za watu, walipopambana na maafisa wa polisi.
Ghasia mjini Baltimore zilianza baada ya mazishi ya kijana Mmarekani mweusi kwa jina Freddie Gray, aliyekuwa na miaka 25 na aliyefariki tarehe 19 mwezi wa Aprili kufuatia majeraha mabaya ya uti wa mgongo aliyoyapata wakati alipokuwa anatiwa nguvuni na maafisa wa polisi.
Mmoja wa waandamanaji akiharibu gari la polisi mjini Baltimore
Mmoja wa waandamanaji akiharibu gari la polisi mjini Baltimore
Licha ya maombi ya kudumisha amani kutoka kwa familia ya kijana huyo, vijana mjini Baltimore walimiminika mitaani na kuzua vurugu, kuchoma magari, kupora maduka na kuharibu biashara za watu.
Kufuatia visa hivi Meya wa Baltimore Stephanie Rawlings-Blake ametangaza amri ya kutotoka nje kuanzia usiku wa leo na kuamuru shule za mji huo kufungwa kwa siku moja.
Stephanie Rawlings amesema hawatakubali wezi na wahalifu kuuharibu mji wa Baltimore kwa vurugu na ghasia.
"Watu wengi wametumia muda mwingi kujenga mji huu, hatuwezi kuwaacha wahalifu kuuharibu mji ambao watu wengi wameupigania," alisema meya Rawlings Blake.
Maafisa sita wasimamishwa kazi kwa Muda kupisha uchunguzi
Hizi ni vurugu za hivi karibuni kabisa katika mfululizo wa makabiliano kati ya polisi wa Marekani na vijana Wamarekani weusi waliojawa na hasira kwa kile wanachokiita ubaguzi unaofanywa dhidi yao na maafisa wa polisi.
Huku hayo yakiarifiwa maafisa wapatao sita wamesimamishwa kazi kwa muda kupisha uchunguzi unaofanwa juu ya mauaji ya Freddie Gray, ambapo ripoti ya uchunguzi huo inatarajiwa kukabidhiwa waendesha mashtaka wa jimbo la Maryland.
Polisi wa mjini Baltimore katika jimbo la Maryland
Polisi wa mjini Baltimore katika jimbo la Maryland
Lakini idara ya sheria nchini Marekani ambayo tayari ilikuwa imeshaanza uchunguzi juu ya utumiaji wa nguvu kupita kiasi unaodaiwa kufanywa na polisi wa Baltimore imefungua uchunguzi juu ya haki za binaadamu
Hata hivyo polisi imekiri kwamba Kijana Freddy Gray aliomba kupewa matibabu kwa kupewa kifaa cha kuvutia pumzi baada ya kuzuiliwa na kukiri kwamba gray angepaswa kupewa matibabu mapema.
Kisa hiki kinatokea miezi kadhaa baada ya kisa cha kupigwa risasi mmarekani mweusi ambaye hakuwa na silaha Michael Brown na afisa mmoja wa polisi mjini Ferguson, Missouri hali iliosababisha maandamano makubwa.

Bayern Munich wahifadhi taji la Bundesliga

Kama ilivyotarajiwa Bayern Munich imetawazwa rasmi jana kuwa mabingwa msimu huu wa Bundesliga kwa mara ya 25. Lakini kocha Pep amesema hawastahili kusherekea sana maana kazi bado ipo
Fußball Bundesliga Bayern München vs. Hertha BSC
Mabingwa hao watetezi wamevalishwa taji hilo bila ya kusukuma gozi uwanjani baada ya mchezo wa jana kati ya timu mbili zinazoifuata Bayern kileleni , Borussia Moenchengladbach na VFL Wolfsburg inayoshika nafasi ya pili baada ya Bayern. Wolfsburg iliingia uwanjani ikiwa na matumaini ya kuichafulia Bayern sherehe za ubingwa iwapo ingeshinda mchezo huo. Lakini ilikuwa ni Borussia Moenchengladbach iliyofanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wolfsburg na kusababisha shangwe mjini Munich na kila mahali mashabiki wa Bayern waliko. Bayern ina pointi 15 zaidi ya timu inayoifuatia Wolfsburg na kufungwa kwa timu hiyo kuna maana kwamba hakuna tena timu inayoweza kufikia pointi hizo wakati ikibakia michezo minne Bundesliga ifunge pazia lake msimu huu.
Fußball 1. Bundesliga 27. Spieltag Borussia Dortmund - Bayern München
Bayern wana kibarua dhidi ya Dortmund katika nusu fainali ya DFB Pokal
Kwa kucheza vizuri namna hii , sina hofu ya watu wengi kuipenda michezo. Kwa upande mwingine , kwa kiasi fulani shauku inabidi kurejea katika bundesliga. Ukiangalia mchezo wa leo , Gladbach dhidi ya Wolfsburg , timu namba tatu na namba mbili, timu zote zimecheza kama wanafunzi. Iwapo hali ni hiyo, unapata hofu juu ya soka la Ujerumani kwa jumla.
Bayern ambayo inacheza katika nusu fainali ya Champions League barani Ulaya na pia kombe la Ujerumani iliishinda Hertha Berlin kwa bao 1-0 siku ya Jumamosi na imefikisha pointi 76 kutokana na michezo 30 , wakati Wolfsburg ina pointi 61 katika nafasi ya pili.
Paderborn iliyoko katika nafasi ya pili kutoka mwisho ilipoteza uongozi wake wa mabao 2-0 dhidi ya Werder Bremen na kutosheka na sare ya mabao 2-2 jana.
Kocha Bruno Labbadia wa SV Hamburg amepata ushindi muhimu kwa timu yake ambayo imo katika hatari ya kushuka daraja baada ya kuishinda FC Augsburg inayowania nafasi ya kucheza katika ligi ya Ulaya msimu ujao kwa mabao 3-2. Wakati michezo minne imebakia katika msimu huu wa Bundesliga , SV Hamburg ina pointi 28 ikiwa katika nafasi ya 16 , ikiwa na maana ni nafasi ya tatu kutoka mwisho wa msimamo wa ligi. Lakini shangwe zilikuwa hazina mipaka jana mjini Hamburg.
Fußball Bundesliga SV Werder Bremen vs. Hamburger SV
Bruno Labbadia alipata ushindi wake wa kwanza tangu alipojiunga na Hamburg
Imeonekana baada ya mchezo uwanjani. Hii ni hisia, kama vile tumeshinda ubingwa. Ulikuwa ni ushindi muhimu sana, kwa kuwa tuko mkiani mwa ligi. Wiki iliyopita pia tulicheza vizuri lakini tukashindwa, kiakili hii inaumiza sana. Lakini leo tumecheza vizuri na tulistahili kushinda. Utagundua jinsi maisha yalivyo hapa Hamburg. Matokeo mengine yalikuwa pia mazuri, kwa hiyo bado kuna uhai.
Borussia Dortmund timu ambayo msimu huu umekuwa wa kusua sua , hatimaye inaonesha uhai, baada ya kuishinda Eintracht Frankfurt kwa mabao 2-0 siku ya Jumamosi. Kocha Jürgen Klopp baada ya kutangaza kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu, amesema hofu ya kushuka daraja sasa haipo tena na ni wakati wa mpambano wa kucheza katika kinyang'anyiro cha Ulaya.
Kama ingekuwa tunaongoza kwa pointi tatu , tusingejisikia salama pia. Kwasasa tuko pointi tatu nyuma ya Schalke na Augsburg. Sasa tunahitaji kusonga mbele. Tunahitaji kujaribu kila kitu kinachowezekana. Tunalazimika kutumia kila kilichoko katika uwezo wetu, ili kuweza kukamilisha msimu huu vizuri. Wakati fursa inakuwapo, kuweza kufanya kitu kidogo kuelekea kileleni, basi tutajaribu.
VFL Stuttgart ambayo bado inainamiwa na jinamizi la kushuka daraja ilishindwa kupata matokeo mazuri na iliridhika na sare ya mabao 2-2 dhidi ya SC Freiburg siku ya Jumamosi , nayo Bayern Leverkusen haikuweza kutamba mbele ya FC Kolon baada ya kutoka sare pia ya bao 1-1 katika mchezo wa watani wa jadi (Derby).

bahari ya mediteranian ni hatari kwa wahamiaji haramu kuliko.angalia haya mateso

Picha za maelfu ya vijana wanaojaribu kuivuka Bahari ya Mediterrenean kuingia Ulaya mara nyingi zinawahusu Waafrika ambao kutokana na kukata kwa tamaa, hujining'iniza kwenye maboti, wakielea majini wakiwa maiti, au hoi.
Boot mit Flüchtlingen im Mittelmeer
Boti yenye wahamiaji katika Bahari ya Mediterrenean
Je, picha hizi zinaibua hisia zipi miongoni mwa Waafrika wanaoishi hapa Ulaya? .Kila mara nikisikia maneno, 'Mediterrenean' au 'Lampedusa,' ninatetemeka na kuingiwa na huzuni. Hii ni kwa vile ninajua kuwa watu zaidi ninaowaita kuwa wangu, Waafrika wenzangu watatajwa kuhusika katika mkasa wa hivi karibuni au kuzikwa kwenye fuo za mataifa ya Ulaya.
Labda ungenitarajia, mimi Mwafrika, kughadhabishwa na Ulaya. Lakini nina ghadhabu dhidi ya serikali za Afrika kwa kutofanya inavyostahiki.
Ninachoona kuwa si jambo la kawaida ni kwamba hakuna mwengine, katika Ulaya, anayeonekana kuzitarajia serikali za Afrika kulitafutia suala hili suluhu. Wazungu aghalabu husema wanahitaji kutafuta suluhu, wanahitaji kuboresha hali katika sehemu wanakotokea wahamiaji hawa. Lakini hawaonekani kutumainia au kutarajia serikali za Afrika kusaidia kutafuta suluhu hiyo. Waafrika hawahitaji kusikitikiwa na Wazungu, wanachohitaji ni uwajibikaji.
Ulaya inafaidi kutokana na hali hii ya wafanyakazi kutoka Afrika wanaolipwa ujira mdogo, kweli! Wavuvi wanajipatia vya bwerere katika sehemu maarufu za maji karibu na Afrika. Kakao, matunda, mboga na maua yote yanakuzwa katika bara letu kisha kusafirishwa kwa meli hadi Ulaya na maeneo mengine duniani. Lakini hakuna anayetaka Waafrika kusafiri pamoja na bidhaa zinazosafirishwa kutoka bara letu.
Tangu Ulaya ilipoanza kuangazia suala hilo, imeitisha kikao kimoja tu kuhusu Afrika mjini Kigali. Ninatilia shaka iwapo pendekezo lolote miongoni mwa yaliyotokana na kikao hicho, litatekelezwa.
Ninaamini kuwa tatizo hili linafaa kuwa tatizo la Afrika, ndipo litakaposuluhishwa. Ninafedheheka nikiwa Mwafrika na kufedheheshwa na serikali za bara langu. Changamoto kuu inayotukabili ni kubadili mtazamo wa Waafrika kuhusu Ulaya. Si paradilo kwa wengi wao, ni jahanamu.
Nimekutana na Waafrika walioko Ulaya, wanaolipwa dola 3 kwa siku au chini ya hapo. Kulala ni tabu. Wanauza bidhaa haramu na kutumiwa visivyo au kulazimika kufanya kazi katika maeneo hatari au kushiriki ukahaba. Maisha yao wakiwa Ulaya, huwa mabaya kuzidi ya waliowaacha nyumbani.
Ulaya inasalia kuwa eneo lenye madhara kwa Waafrika wengi. Nilipoishi Italia, nilipokuwa chuoni, aghalabu wanaume walinisogelea na kuniuliza, niligharimu fedha ngapi kwa usiku mmoja. Kile ninachotaka kuwaambia Waafrika wenzangu ni kuwa, ondoeni dhana kwamba Ulaya itatatua matatizo yenu. Upo uwezekano kwamba utaishi katika mitaa duni huku pia.
Ni wakati wa kuzinduka na kumwezesha kila mmoja ajikimu katika taifa lake, badala ya kuwa na matarajio makubwa kuhusu mambo yasiyokuwapo.

ukivuka bahari ya mediterania ni hatari kuliko kitu chochote hatari dunia . tazama wahamiaji harau wanavyoteseka

Kuvuka Bahari ya Mediterrenean ufike hoi au maiti

raisi mpya wa togo huyu hapa .

Rais wa Togo Faure Gnassingbe
Tume ya uchaguzi nchini Togo, imetangaza kuwa Rais, Faure Gnassingbé, ameshinda tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu.
Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa Rais huyo aliyeingia uongozini mnamo mwaka 2005 amepata zaidi ya asilimia 58 ya kura.
Idadi iliyojitokeza kupiga kura siku ya Jumamosi ilifikia asilimia 60.
Bwana Gnassingbé amekuwa uongozini tangu kifo cha babake, Gnassingbé Eyadema, aliyechukua uongozi wa Togo kwa njia ya mapinduzi mwaka 1967.
Mwaka jana, kulikuwa na maandamano makubwa nchini Togo, huku waandamanaji wakiitaka serikali kubuni sheria ya mihula miwili ya Urais.

watoto wa kike na wamama 293 waokolewa nigeria na jeshi la nchi hiyo.

Jeshi la Nigeria
Jeshi la Nigeria limesema limewaokoa watoto wa kike mia mbili na akina mama tisini na tatu kutoka katika kambi ya Boko Haram iliyoko katika msitu wa Sambisa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi hilo limesema watoto hao waliokolewa si kati ya wale waliotekwa mwaka mmoja uliopita na kundi la kiislamu katika eneo la Chibok.
Jeshi limeiambia BBC kwamba wanawake na watoto hao wa kike walikutwa katika kambi nne tofauti ambapo silaha pia zimekamatwa,Msemaji wa jeshi amesema waliwapata wasichana hao baada ya kuziharibu kambi hizo.
"ni muda mfupi tu uliopita, wanajeshi wetu wameingia katika msitu wa Sambisa, kutokea upande wa Alafa, ambapo walikuta kambi nne zinazomilikiwa na wapiganaji na kuziharibu, hapo ndipo walipogundua kuwa kuna wasichana wapatao mia mbili na wanawake tisini na tatu."
Jeshi la Nigeria
Kwa sasa jeshi limezuiwa kutoa utambulisho wa wasichana hao. Hata hivyo, jeshi limethibitisha kwamba wasichana hao sio wale wanafunzi waliotekwa katika mji wa Chibok.
"tuko katika mchakato wa kuwachunguza hawa wasichana ili tuweze kubaini utambulisho wao, lakini kitu kimoja nataka nikiweke wazi kwa umma, tunapotaja idadi ya wasichana mia mbili, tayari watu wanaanza kufikiria wasichana mia mbili wa Chibok waliotekwa mwaka jana, hawa sio wasichana wa Chibok, tutaendelea kuwajuza kadri muda unavyokwenda iwapo kutakuwa na taarifa zozote. "

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...