MUME wa mwimbaji Flora Mbasha ,
Emmanuel Mbasha (32 ), amefikishwa katika
Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es
Salaam akikabiliwa na mashitaka mawili
ikiwemo ya ubakaji .
Mshtakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara
na mwimbaji alisomewa mashitaka yake
mbele ya Hakimu Mkazi, Wilberforce
Luago.
Wakili wa Serikali , Nassoro Katuga alidai
kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo
mawili maeneo ya Tabata Kimanga, jijini
Dar es Salaam.
Katuga alidai katika shitaka la kwanza
kuwa , Mei 23, mwaka huu eneo la Tabata
Kimanga, Wilaya ya Ilala , jijini Dar es
Salaam, kinyume cha sheria huku akijua ni
kosa alimuingilia kwa nguvu msichana
anayedaiwa kuwa shemeji yake (jina
limehifadhiwa).
Katika shitaka la pili , ilidaiwa kuwa Mei 25,
mwaka huu eneo la Tabata Kimanga , jijini
Dar es Salaam, kinyume cha sheria ,
mshtakiwa aliumuingilia kwa nguvu
mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa).
Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka
hayo.
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna
pingamizi la dhamana.
Hakimu Luago alitaja masharti ya dhamana
kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili ,
mmoja awe mtumishi wa serikali na
mwingine kutoka taasisi inayotambulika
watakaosaini hati ya dhamana ya Sh.
milioni tano .
Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya
dhamana hivyo alipelekwa rumande na kesi
iliahirishwa
hadi Juni 19 , mwaka huu itakapotajwa .
Mbasha akiwa chini ya ulinzi wa askari
polisi alisindikizwa katika basi la Jeshi la
Magereza kwa ajili ya kwenda kuanza
maisha mapya mahabusu ya Keko , jijini
Dar es Salaam.
Tuesday, 17 June 2014
MWIMBAJI WA NYIMBO ZA DINI KIZIMBANI KWA UBAKAJI WA MFANYAKAZI WA NDANI (HOUSEGIRL)
DUNIA INA MAMBO JANANI, MWIMBAJI MMOJA AFANYIWA UPASUAJI HUKU AKIIMBA ILI KUILINDA SAUTI YAKE ISIHARIBIKE.
Mwimbaji Alama Kante, amelazimika kuimba
huku akifanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe
kwenye koo lake ili madaktari wasiharibu sauti
yake.
Mwimbaji huyo kutoka Guinea mwenye
makazi yake nchini Ufaransa alipatiwa dawa za
kumfanya asisikie maumivu wala uchungu
wakati wote wa zoezi la upasuaji.
Kante alikuwa akiogopa kupoteza sauti yake
lakini daktari wake alipendekeza afanyiwe
upasuaji huku anaimba.
Kante ambaye kwa sasa amepata nafuu
amesema wakati upasuaji ukiendelea alihisi
kama yuko Senegal na wakati alipoamka na
kuzungumza tena madaktari na wauguzi
walifurahi kwakuwa wametimiza lengo lao.
HII NDIO KAULI YA RAISI WA KENYA BAADA YA KUTOKEA KWA MILIPUKO MIWILI YA MABOMU
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa
mauaji yaliyofanywa katika mji wa Mpeketoni,
Pwani ya Kenya hayakufanywa na kundi la
wapiganaji wa kiislamu la Al Shabaab.
Kauli ya Rais Kenyatta inakuja siku moja baada
ya kundi hilo kukiri kufanya mauaji
yaliyotokea Mpeketoni Jumapili usiku.
Akitoa hotuba yake ya kitaifa, Rais Kenyatta
pia amesema maafisa wa polisi Mpeketoni
ambao walifanya uzembe hadi kutokea
mashambulizi hayo watashtakiwa.
Al Shabaab lilikiri katika taarifa kwa vyombo
vya habari kuwa ndilo lilifanya mauaji hayo
Jumatatu jioni.
Mauaji zaidi yalifanyika usiku wa kuamkia leo
licha ya taarifa ya Al Shabaab kusema kuwa
washambuliaji walioshambulia Mpeketoni
walikuwa wamerejea salama nchini Somalia.
Uharibifu mkubwa ulishuhudiwa katika mji
huo huku washambuliaji wakichoma hoteli na
kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari
waliyoyatumia kwa usafiri wao.
Kenyatta amesema kuwa kuna baadhi ya
wanasiasa wanaochochea uhasama miongoni
mwa jamii.
Utahiri mpya kutoka uganda
Hii ndio njia mpya
inayotumika kutahiri wanaume
Uganda.
Wizara ya afya nchini Uganda imeanza
majaribio ya kutumia kifaa kipya kwa ajili ya
kutahiri wanaume ili kujikinga na maambukizi
ya virusi vya Ukimwi.
Kifaa hicho rahisi cha mpira kinatumika kutoa
ngozi ya mbele ya uume wa mwanaume
tofauti na mwanzo ambapo kisu kilikuwa
kikitumika kufanya shughuli hiyo.
Igalla ambaye ni baba wa watoto wawili
amefanyiwa tohara kwa kutumia njia hiyo
ambapo anasema inachukua dakika chache na
hakujihisi vibaya hata kidogo tofauti na
tohara za kimila ambapo mwanaume
hutahiriwa kwa kutumia kisu.
Wanasayansi waligundua kuwa tohara kwa
wanaume inaweza kupunguza kwa kiasi
kikubwa uwezekano wa kupata maambukizi ya
virusi vya Ukimwi.
Mbali na Uganda kifaa hicho pia kinatumika
nchini Botswana, Kenya, Mozambique, Afrika
Kusini, Zambia, Zimbabwe na nchi nyingine.
Uganda ina matumaini kuwa kifaa hicho
kiitwacho PrePex kitawahamasisha wanaume
wakubwa Uganda kwenda kufanyiwa tohara
kama sehemu ya mapambano dhidi ya
ugonjwa hatari wa Ukimwi unaosababisha vifo
vya mamilioni ya watu.
CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA
Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...

-
Tuzo za VMA 2014 zimefanyika na mastaa wengi walifika kwenye hilo tukio. Listi ya mastaa hao iliongozwa na familia ya Jay Z na Beyon...
-
Luca Modric mchezaji bora wa mwaka wa FIFA Wameamua kumpa,ni baada ya kumdhurumu tuzo yake ya msimu wa 2009/10,mwaka huu wameona ai...
-
Mlinda mlango wa Derby Country akipangua mkwaju wa Phil Jones Timu ya DERBY COUNTY inayonolewa na nyota wa zamani wa CHELSEA, FRANK LAM...