Image caption
Joka kubwa zaidi kuwahi kukamatwa duniani amekufa.
Joka kubwa zaidi kuwahi kukamatwa duniani amekufa.
Chatu
huyo aliyepatikana katika eneo lililokuwa likijengwa nchini Malaysia
karibu na mti mkubwa uliokatwa katika kisiwa cha Penang.
Joka hilo linakisiwa kuwa takriban mita 8 hivi sawa na futi 26 lilipatikana siku ya Alhamisi iliyopita.
Kwa bahati mbaya joka hilo lilikufa jumapili lilipokuwa likizaa. Image caption
Chatu huyo aliyepatikana katika eneo lililokuwa likijengwa nchini Malaysia
Afisa anayesimamia ujenzi katika kisiwa hicho cha Penang, Herme Herisyam aliiambia BBC.
Kulingana na daftari za kumbukumbu za Guinness, joka anayeshikilia rekodi ya dunia anaurefu wa mita 7.67.
Chatu huyo anayeitwa Medusa ana uzani wa kilo 158 na anaishi katika jumba moja mjini Kansas City, Missouri Marekani. Image caption
Bw Herisyan anasema kuwa alikuwa na uzani wa kilo 250.
Hata hivyo joka huyo wa Malaysia ambaye alikuwa
mkubwa zaidi yake hakuwa amepimwa na kuthibitishwa kuwa mrefu zaidi
kabla ya kufa kwake.
Bw Herisyan anasema kuwa alikuwa na uzani wa kilo 250.
Hata
hivyo katika harakati za kumuokoa kutoka maficho yake inakisiwa kuwa
aliumia na hivyo akafa kabla hajafikishwa kwenye hifadhi ya wanyama
alikotarajiwa kutuzwa hadi ajifungue.
Image caption
Zaidi ya maduka 150 yameteketea kwa moto
Moto mkubwa umezuka
na kuteketeza vibanda vya maduka zaidi ya 150 katika mji wa Kayanga
wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera magharibi mwa Tanzania. Moto huo ambao
ulianza Jumatatu majira ya sa 2:00 usiku umeteketeza mali na bidhaa za
aina mbalimbali kama mchele, sukari, nguo, simu, pamoja na bidhaa
zingine.
Gloria Kilio ambaye alikuwa akiuza vyakula vya nafaka,
amesema stoo zake zote tatu (3) za nafaka zimeungua, “Stoo zilikuwa na
magunia ya unga, mchele na sukari lakini vyote vimeteketea,” amesema
Gloria huku akilia. Anasema wakati moto unatokea alikuwa tayari
amekwisha kwenda nyumbani na kuwaacha wafanyakazi wake wakimalizia
kufunga vibanda.
Wafanyabiashara wengi wanasema walikuwa na mikopo
na wengi wao hawana bima ya mali zao. Jonasi Nyarugenda ni miongoni mwa
wafanyabiashara hao: “Moto umeteketeza stoo zangu nne zenye bidhaa
mbalimbali kama sukari, mchele, ngano na mafuta,: anasema Jonas na
kuongeza, “kwakeli ukitathimini kwa haraka siyo chini ya milioni 45
zimepotea.” Amesema kwamba alikuwa hana bima katika mkopo wake wa
milioni 20 kutoka katika benki.
Image caption
Wafanyabiashara wamedai kupata hasara kutokana na ajali hiyo
Hasara hiyo kwa kiasi kikubwa imechangiwa na ukosefu
wa vifaa vya kuzima moto. Wananchi wa Karagwe imewapasa kusubiri gari
la Zimamoto kutoka Bukoba Mjini (magari ya uwanja wa ndege) ambako ni
kilomita 120 kufika karagwe mjini. Hata hivyo magari hayo yalikuta
maduka mengi yamekwishateketea.
Diwani wa kata ya Kanoni wilaya
karagwe Sabi Rwazo amesema tukio hilo limewastua na ni tukio la kwanza
la moto kuunguza soko wilayani humo. Anasema tatizo la ukosefu wa gari
la zima moto linachangiwa na uhaba wa fedha. “Mara nyingi katika bajeti
yetu imekuwa ikishindwa kununua gari.” Amesema Rwazo na kusema maombi
yao yako serikali kuu.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Deodatus Kinwiro
amesema kuwa Serikali ya wilaya yake itapata gari la zima moto hivi
karibuni, “Bahati nzuri nilikuwa Dar es Salaam, nimekutana na kamishna
mkuu wa zima moto ameniahidi kunipatia gari jipya,” amesema Kinwiro na
kuongeza kuwa, “wakati wowote gari hilo litafika wilayani Karagwe.”
Hata
hivyo baadhi ya wananchi wanasema hawakubaliani na kauli hiyo ya mkuu
wa wilaya kwa sababu wamekuwa wakitozwa kiasi cha TZS 30,000 kwa mwezi
ili kuchangia huduma za zimamoto wilayani hapo lakini wanashangaa kwa
nini hawapati elimu ya kujikinga na majanga, na hakuna hata gari la
dharura.
Mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana lakini
taarifa za awali zimeonesha kuwa kuna Mamalishe mwenye kibanda sokoni
hapo aliacha jiko lake bila kuzima hivyo likashika nguo zilizokuwa
katika kibanda hicho na kusababisha moto kusambaa ghafla.