Wednesday, 10 June 2015

Ubelgiji Kumkosa Fellaini


Nyota wa Ubelgiji Marouane Fellaini
Timu ya taifa ya Ubelgiji ina wasiwasi wa kumkosa nyota wake Marouane Fellaini katika mchezo wa kuzufu kwa michuano ya ulaya.
Ubelgiji watakua na mchezo dhidi ya Wales siku ya Ijumaa katika kusaka tiketi ya kucheza Euro 2016.
Fellaini anasumbuliwa na maumivu ya nyonga iliyomsabaisha kutojumuika na wenzake katika mazoezi.
kocha wa kikosi hicho Marc Wilmots ameeleza kuwa wanasubiri kauli ya daktari wa timu ili kujua ukubwa wa tatizo na kama wataweza mtumia mchezaji huyu katika mchezo huo.
Fellaini alifunga mabao mawili katika ushindi wa 4-3 dhidi ya Ubelgiji katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa kalenda ya Fifa.

chriss brown baada ya ukimya wa muda sasa atoa tamko kuhusu mapenzi yake. atoboa siri.





Story kubwa nyingine ikachukua headlines, washkaji wa Chris Brown walipanga mchezo marafiki wa kuwakutanisha pamoja wakijifanya eti Karrueche alitaka kukutana na Chris Brown ili kumaliza tofauti zao na kuendelea na uhusiano.
Karrueche Tran
Chris Brown akapata airtime ya interview iHeart Radio, moja ya maswali yaliyoulizwa ni kama anampenda Karrueche?
“Siwezi kuahidi chochote kwa sasa kwani sitaki kukurupuka, ndio bado nampenda sana siwezi kudanganya.. ila katika maisha inafika wakati inabidi tusimame tuangalie mapungufu.
“tusonge mbele na tutafute namna ya kutatua matatizo hayo… nakubali kuwa nilikosea na inabidi sasa nisimame kutazama nilipokosea kipindi cha nyuma …mimi ni baba sasa … kuhusu mimi na yeye, tuipe muda.”
Ameongelea pia kuhusu mtoto wake wa mwaka mmoja Royalty na maisha ya kuwa baba pamoja na magari na anayotembelea.

tazama Waganda wanavyopenda ngono mchana . Waziri wa maadili atoa tamko .



 
 
 

Matamshi ya waziri wa maadili nchini Uganda kuwa Waganda wengi hujihusisha na vitendo vya kufanya mapenzi hasa wakati wa kipindi cha mlo wa mchana yamezua gumzo kali katika vyombo vya habari nchini humo na katika mitandao ya kijamii.
Simon Lokodo ameongeza kusema wamiliki wa nyumba za kulala wageni wakamatwe kwa kuwaruhusu wafanyi kazi wanaotoka maofisini wakati wa mchana na kwenda kula uroda vyumbani humo.
Wengi wanakiri kuwa tetesi hizo zimeenea nchini humo kwamba wengi wa wafanyikazi hutumia fursa ya mapumziko ya mchana kujihusisha na vitendo vya ngono na makahaba au wapenzi wao wa pembeni.
Baadhi wanaunga mkono kauli hiyo ya waziri lakini wengine wamemtaka asijihusishe na maisha ya wengine

eden hazard atikisa katika bei ya usajili duniani.



leoleo
 Mtandao wa Shirika la tathmini za thamani za wachezaji CIES kwa upande wa soka limetoa orodha mpya ya thamani za wachezaji katika ligi tano kubwa Ulaya.
Katika orodha iliyotolewa inaonyesha mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard atauzwa kwa bei kubwa zaidi ya mshindi wa Ballon d’OrCristiano Ronaldo msimu huu.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ana thamani ya kati ya Pound Milioni 99 hadi Milioni 110.
Mshindi huyo wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Chama cha Wachezaji wa kulipwa England (PFA), ameshika nafasi ya pili nyuma ya Lionel Messi, ambaye ana thamani ya Pound Milioni 207, wakati mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo anakamilisha tatu bora kwa thamani ya kati ya Pound Mil. 83 hadi Mil. 92.
Wachezaji wenye thamani kubwa zaidi Ulaya
Jina la Mchezaji Muda wa mkataba umri Thamani (Pound)
Lionel Messi (Barcelona) 2018 27 188-207
Eden Hazard (Chelsea) 2020 24 99-110
Cristiano Ronaldo (Real Madrid) 2018 30 83-92
Neymar (Barcelona) 2018 23 66-73
Sergio Aguero (Manchester City) 2019 27 57-63
Raheem Sterling (Liverpool) 2017 20 54-60
Paul Pogba (Juventus) 2019 22 52-57
Diego Costa (Chelsea) 2019 26 52-57
Alexis Sanchez (Arsenal) 2018 26 50-55
James Rodríguez (Real Madrid) 2020 23 46-51
Luis Suarez (Barcelona) 2019 28 44-49
Antoine Griezmann (Atletico Madrid) 2020 24 44-48
Cesc Fàbregas (Chelsea) 2019 28 43-48
Isco (Real Madrid) 2018 23 42-46
Harry Kane (Tottenham) 2020 21 40-44
Gareth Bale (Real Madrid) 2019 25 38-42
Philippe Coutinho (Liverpool) 2020 22 37-41
Thibaut Courtois (Chelsea) 2019 23 37-41
Oscar (Chelsea) 2019 23 35-39
Karim Benzema (Real Madrid) 2019 27 33-37
Mario Gotze (Bayern Munich) 2017 23 32-35
Koke (Atletico Madrid) 2019 23 30-33
Christian Eriksen (Tottenham) 2018 23 30-33
Romelu Lukaku (Everton) 2019 22 29-33
Toni Kroos (Real Madrid) 2020 25 29-32
Willian Borges (Chelsea) 2018 26 29-31
Alvaro Morata (Juventus) 2019 22 28-31
Sergio Busquets (Barcelona) 2019 26 28-31
David Silva (Manchester City) 2019 29 28-31
Edinson Cavani (PSG) 2018 28 28-31
Angel Di María (Manchester United) 2019 27 27-30
Kevin de Bruyne (Wolfsburg) 2019 23 27-30
Wayne Rooney (Manchester United) 2019 29 27-29
Marco Verratti (PSG) 2019 22 26-29
Nemanja Mati? (Chelsea) 2019 26 26-29
Robert Lewandowski (Bayern Munich) 2019 26 26-29
Alexandre Lacazette (Lyon) 2018 24 26-29
Thomas Muller (Bayern Munich) 2019 25 26-29
Manuel Neuer (Bayern Munich) 2019 29 25-28
Mesut Ozil (Arsenal) 2018 26 25-28
Gonzalo Higuaín (Napoli) 2018 27 25-28
Ross Barkley (Everton) 2018 21 25-27
Yaya Toure (Manchester City) 2017 32 25-27
Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal) 2018 21 25-27
Jerome Boateng (Bayern München) 2018 26 24-26
Santi Cazorla (Arsenal) 2017 30 24-26
Danny Welbeck (Arsenal) 2019 24 24-26
Jordan Henderson (Liverpool) 2020 24 24-26
Aaron Ramsey (Arsenal) 2019 24 23-26
Miralem Pjanic (Roma) 2018 25 23-26

The Game huenda akaingia jela kwa muda .soma hii


<> at Greystone Mansion on September 24, 2013 in Beverly Hills, California.
The Game
The Game alikuwa na noma na Polisi mwezi March 2015, video ikanaswa na kusogezwa Youtube.. Baadae Polisi waliona hii wasiiache, story kwenye headlines ni kuhusu jamaa kukamatwa na Polisi japo kosa alilifanya muda mrefu uliopitwa.
Rapper huyu amefunguliwa mashitaka na Polisi wa Los Angeles baada ya kuingia kwenye utata na polisi wakati wanacheza Basketball na kisha kumpiga ngumi polisi huyo tukio ambalo watu walilinasa kwenye video na baadae likarushwa kwenye mtandao wa YouTube.
The Game
Japo video hio ina muda wa miezi mitatu toka irushwe  Youtube, Police wamesema kwamba wamefungua mashitaka kutokana na video hiyo kusambaa Youtube alafu watu wakawa kama wanawadharau Polisi kwa kutomfanya chochote jamaa.
Baada ya kufunguliwa mashtaka, The Game aliachiwa saa chache baadae kwa dhamana.
Hii ndio video inayoonesha tukio la The Game kumpiga Polisi.

Marekani kutuma mamia ya majeshi Iraq

Utawala wa Rais Barack Obama wa Marekani unafanya mipango ya kuanzisha kambi mpya ya kijeshi katika jimbo la Anbar nchini Iraq na kuwatuma wanajeshi wa kutoa mafunzo na ushauri kuliimarisha jeshi la Iraq ambalo limekuwa likipambana na wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS. Duru zinaarifu kuwa Rais Obama huenda akauidhinisha mpango huo wa kuongeza shughuli za kijeshi nchini Iraq hii leo. Wanamgambo wa IS waliuteka mji mkuu wa jimbo la Anbar wa Ramadi mwezi uliopita na Marekani inapanga kuweka mikakati madhubuti kuukomboa mji huo. Marekani ina wanajeshi 3,100 nchini Iraq wanaotoa mafunzo na ushauri hivi sasa. Rais Obama anatarajiwa kuidhinisha mpango huo wa kutuma majeshi zaidi nchini Iraq mapema iwezekanavyo.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...