Muungano wa waasi wa Syria wenye mafungamano na mtandao wa
kigaidi wa al-Qaida, umeuteka mji wa Ariha, ambao ulikuwa wa mwisho
unaoshikiliwa na serikali ya nchi hiyo katika mkoa wa Idlib.
Shirika la kuchunguza haki za binaadamu la Syria lenye makao yake
nchini Uingereza, limesema muungano huo, Al-Nusra Front na washirika
wake wa Jaish al-Fatah, au Jeshi la Ushindi, walichukua udhibiti wa mji
huo baada ya mapambano makali baina yao na jeshi la serikali ya Syria,
ambalo lilikuwa likisaidiwa na wanamgambo wa Hezbollah kutoka Lebanon.
Kundi la Al-Nusra Front limethibitisha kuuteka mji huo kupitia
mtandao wa kijamii wa Twitter, na Shirika la kuchunguza haki za
binaadamu nchini Syria limesema msafara wa magari ya kijeshi ulionekana
ukiukimbia mji huo wa Ariha.
Mshindi wa uchaguzi mkuu nchini Nigeria Muhamadu Buhari anaapishwa leo kama rais mpya wa nchi hiyo.
Bwana
Buhari ambaye ni kiongozi wa zamani wa kijeshi anachukua uongozi kutoka
kwa rais wa zamani Goodluck Jonathan ambaye amemtaka kuiunganisha nchi
hiyo wakati inapokabiliana na tisho kutoka kundi la Boko Haram.
Buhari
anasema kuwa lengo lake ni kupambana ufisadi ambao umekita mizizi
katika taifa hilo lenye watu wengie zaidi barabi afrika.
Lakini je Buhari ni nani ?
Wafuasi wa rais Buhari wakishangilia ushindi huo
Muhammadu Buhari, ni Muisilamu, mzaliwa wa Jimbo la Katsina, Nigeria kaskazini.
Alizaliwa mwaka 1942, Buhari alikuwa kiongozi wa saba wa taifa la Nigeria, baina ya mwaka 1983-1985.
Ni jenerali mstaafu aliyepata mafunzo ya kijeshi katika Nigeria, Uingereza, India, na Marekani.
Na
aliwahi pia kushika nyadhifa za ugavana, kamishna wa raslimali ya
mafuta, mwenyekiti wa shirika la umma la mafuta, na pia mwenyekiti wa
Mfuko wa Amana ya Mafuta.
Anasemekana kuwa si m-kaishi, hakubali kushindwa.
Buhari alimshinda rais anayeondoka Goodluck Jonathan katika uchaguzi ulioshuhudia ushindani mkubwa
Licha ya kushindwa mara katika chaguzi tatu, amerejea kushindania tena urais, dhidi ya rais alo-madarakani Goodluck Jonathan,
Mkristo,
anaye toka eneo la Niger Delta, kusini Nigeria, kwa mara ya pili,
katika uchaguzi wa Machi. Unaonesha kuwa mchuano mkali.
Kuambatana
na mandhari ya kisiasa, Buhari si limbukeni. Kushindwa mwaka 2003 na
tena 2007, alitambia matokeo ya chaguzi hizo mahakamani bila mafanikio.
Ingawaje, Buhari anazingatiwa kuwa kiongozi mwenye ufuasi mkubwa na heshima nyumbani, hususan katika rubaa za kaskazini Nigeria.
Na hii inatokana na sera zake za kupambana na ufisadi na ukosefu wa nidhamu, wakati alipokuwa mtawala wa kijeshi.