Friday, 29 May 2015

Jeshi la Syria lapoteza mji wa mwisho katika mkoa wa Idlib

Muungano wa waasi wa Syria wenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida, umeuteka mji wa Ariha, ambao ulikuwa wa mwisho unaoshikiliwa na serikali ya nchi hiyo katika mkoa wa Idlib.
Shirika la kuchunguza haki za binaadamu la Syria lenye makao yake nchini Uingereza, limesema muungano huo, Al-Nusra Front na washirika wake wa Jaish al-Fatah, au Jeshi la Ushindi, walichukua udhibiti wa mji huo baada ya mapambano makali baina yao na jeshi la serikali ya Syria, ambalo lilikuwa likisaidiwa na wanamgambo wa Hezbollah kutoka Lebanon.
Kundi la Al-Nusra Front limethibitisha kuuteka mji huo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, na Shirika la kuchunguza haki za binaadamu nchini Syria limesema msafara wa magari ya kijeshi ulionekana ukiukimbia mji huo wa Ariha.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...