Friday, 14 August 2015

unandoto ya kuwa mjasiria mali? tumaini hili hapa

Watu wengi siku hizi na haswa vijana huwa wakishahitimu chuoni wanatafuta ajira kwa kipindi kirefu na hatimaye wanakata tamaa.
Wengi hao huamua kuanzisha biashara ndogo ndogo kwa nia ya kujikimu kimaisha.
Wengi huibukia kuwa wajasiria mali shupavu kutokana na talanta yao.
Aidha wengine uvumbuzi wao huwapatia kipato hata zaidi ya mshahara ambao wangepata laiti wangeajiriwa.

 






Je unandoto ya kuwa mjasiria mali?
Hata hivyo idadi ya wajasiria mali ambao hushindwa kuendeleza biashara zao baada ya miaka mwili ni kubwa mno.
Je wewe unaweza kuwa mjasiria mali mtajika?
Kupata jibu la swali hilo, tafadhali jibu maswali haya ambayo yatakusaidia kutathmini uwezo wako wa kuwa mjasiria mali shupavu
Tahadhari:
Chemsha bongo hii hailengi kukubashiria iwapo utafaulu au la katika ulimwengu wa biashara.
Imeundwa kutokana na nadharia wala haifai kutumika badala ushauri wa kiufundi.
Je maswali yalikusudia nini ?
Swala zima la ujasiria mali limekuwepo kwa muda mrefu lakini ni hivi majuzi tu ndio utafiti wa kina kuihusu umeanza kufanywa kwa nia ya kutambua mbinu vigezo na tathmini ya ubora wa mjasiria mali na somo lenyewe.
Chemsha bongo hili lilitokana na utafiti wetu wa sera nadharia zilizochapishwa kuhusiana na ujasiria mali kwa ushirikiano na mhadhiri wa chuo kikuu cha Cardiff Metropolitan, profesa Brian Morgan.
Nia yetu ilikuwa kutathmini ushawishi wa mjasiria mali binafsi kisaikolojia ushindani wake na ari ya kutaka kujiendeleza na kujisimamia.
Imeandikwa na Gerry Fletcher, Robert McKenzie, Ransome Mpini, Will Smale, Nzar Tofiq na John Walton.

wanajeshi wa Amisom wamewaua 6 harusini Somalia



Amisom waliwaua wageni harusini Somalia

Amisom waliwaua wageni harusini Somalia.
Shirika la kupigania haki za binadamu lenye makao yake makuu huko Washington Marekani,Human Rights Watch (HRW), limesema kuwa majeshi ya mataifa ya muungano wa Afrika Amison yaliwashambulia wageni katika harusi moja iliyokuwa imeandaliwa huko Merka Somalia mwezi uliopita.
Katika ripoti yake mpya shirika hilo la kupigania haki za kibinadamu mpya Human Rights Watch,linasema kuwa wanajeshi wa Uganda walivamia kijiji kimoja ambako kulikuwa na halaiki ya watu harusini.
Waliingia chumbani na kuwatenganisha wanaume na wanawake.





 








Human Rights Watch,linasema kuwa wanajeshi wa Uganda walivamia kijiji kimoja ambako kulikuwa na harusi.
'Katika chumba kimoja kilichokuwa na wageni, wanaume 6 walitenganishwa na wanawake na kisha wakawapiga risasi na kuwaua papo hapo.'
'Kati ya wanaume hao sita, wanaume wanne walikuwa ni ndugu baba yao mzazi na ami wao.'
'Wanne walikufa papo hapo kisha mmoja wa ndugu hao aliyejificha chini ya kitanda akawachwa hapo akavuja damu hadi akafa.'
'Walioshuhudia wanasema kuwa wanajeshi hao walikataa kata kata jamaa zao wasiwapeleke hospitalini'' Ripoti hiyo inaeleza.
Kulingana na HRW tukio hilo lilitokea tarehe 31 Julai.



 







Kulingana na HRW tukio hilo lilitokea tarehe 31 Julai katika kijiji cha Merka Somalia
Umoja wa Afrika haujajibu shtuma hizo za HRW.
Shirika hilo la HRW linapendekeza uchunguzi wa kina ufanyike.
'Kuwaua watu bila makosa ili kulipiza kisasi cha mashambulizi dhidi yenu sio jambo jema na hilo litahakikisha kuwa hali itakuwa mbaya zaidi katika siku za usoni ripoti hiyo inasema.
HRW lingali linachunguza ripoti kuhusu mauaji ya raia huko Marka mapema mwezi huu.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...