Friday, 28 August 2015

tazama hii video the most funny ever

tazama hii video kiuno bila mfupa, ray c tupa kuleeeeeeeeeeee

vunja mbavu hapa na kijana, makarao aliempiga bolisi haaaaa haaaa haaaaa bolisi-polisi

cheka hadi jino la mwisho lionekane na video ya huyu mmasai vs police na maswali.

vunja mbavu zako na vichekesho vya dunia hapa na innosam.blogspot.com

donge nono la $20,000 latolewa kwa atakae toa taarifa kuhusu Mshukiwa wa kike wa ugaidi Kenya,muone hapa


Image captionMshukiwa wa ugaidi Rukia Faraj
Serikali ya Kenya imetoa zawadi ya $20,000 wa mtu yeyote atakaye toa habari za kukamatwa kwa mshukiwa mmoja wa ugaidi wa kike, Rukia Faraj.
Idara ya polisi imesema kuwa Rukia anasakwa kwa madai ya kuwasajili na kuwasafirisha watu wachanga kujiunga na mme wake nchini Somalia kwa mafunzo ya ugaidi na pia kujiunga na kundi la kigaidi la Al Shabaab.
Mume wake Ramadhan Kufungwa pia anasakwa na polisi kwa madai ya kupanga mashambulio ya kigaidi nchini Kenya.
Rukia sasa anajumuika na washukiwa wengine ambao wanasakwa na serikali ya Kenya kwa madai ya kupanga mashambulio ya kigaidi.
Wengine ni pamoja na Mohammed Kuno anayejulikana kwa jina lingine Gamadere au Dhuliadein ambaye anatuhumiwa kupanga mashambulio ya kigaidi katika chuo kikuu cha Garisa, ambapo zaidi ya watu 148 waliuawa

Wahamiaji 71 wafariki kwenye Lori huko nchini Austria



Image copyright4 news
Image captionLori lililokuwa na miili ya wahamiaji
Maafisa wa polisi nchini Austria, wamethibitisha kuwa miili ya wahamiaji 71, imepatikana ndani ya lori moja iliyokuwa imeachwa kwenye barabara kuu.
Miili hiyo inajumuisha 59 ya wanaume, 8 ya wanawake na watoto wanne.
Msemaji wa polisi amesema kuwa wao wanashuku kuwa wahamiaji hao wanatoka nchini Syria.
Ameongeza kuwa watu watatu wamekamata nchini humo kuhusiana na vifo hivyo.
Wawili kati yao wakisiwa kuwa raia wa Bulgaria na mwiinge ni raia wa Bulgaria mwenye asili ya Lebabon
Waziri wa masuala ya ndani amesema tukio hilo linaashiria umuhimu wa suala la uhamiaji kushughulikiwa kwa dharura na viongozi wa Muungano wa Ulaya EU.
Miili hiyo imepatikana wakati viongozi wa Ujerumani ,Austria na nchi sita za mashariki mwa visiwa vya Balkan, wakikutana mjini Vienna kuzungumzia tatizo la uhamiaji.
Kansella wa Ujerumani Angela Merkel, amesema viongozi hao wamesikitishwa na ripoti hiyo.
Image copyright
Image captionKambi ya wahamiaji Austria
Amesema tukio hilo ni onyo kwa mataifa ya Ulaya kwamba swala la uhamiaji linaweza tu kutatuliwa iwapo kutakuwa na ushirikiano na uwajibikaji.
Nchi za ulaya zinazopokea idadi kubwa wahamiaji zimeonya kuwa iwapo nchi zingine hazitakubali kuwapa hifadhi wahamiaji athari za haua hiyo zitashuhudiwa katika Jumuiya nzima ya Ulaya.

wahamiaji 200 wafa maji libya,soma hii


Image copyrightBBC World Service
Image captionWahamiaji wakisafiri katika pwani ya Libya
Zaidi ya watu mia mbili wanahofiwa kufariki baada ya boti mbili iliyokuwa imebeba wahamiaji haramu kuzama katika eneo la Zurawa pwani ya Libya.
Mamia ya wahamiaji wengine wameokolewa na wanamaji wa Libya usiku wa kuamkia leo.
Kwa zaidi ya mwaka mmoja Libya haijakuwa na serikali dhabiti na sehemu kubwa ya nchi hiyo inathibitiwa na wanamgambo wa Kiislamu, na walanguzi wa watu wanatumia fursa hiyo kusafirisha watu kimagendo hadi Ulaya.
Kwa mara ya kwanza wakaazi wa mji huo waliandamana kupinga usafirishaji wa watu kupitia mji huo.
Ripoti zinasema kuwa meli mbili iliyokuwa imebeba wahamiaji hao ilizama muda mfupi tu baada ya kunoa nanga.
Meli moja inasemekana kuzana usiku wa kuamia siku ya Alhamisi na nyingine saa chache baada ya tukio hilo.
Kwa mujibu wa afisa mkuu wa shirika la uhamiaji la kimataifa IOM, nchini Libya, watu mia moja tayari wameokolewa na kusafirisha hadi kambi moja ya muda iliyoko mji wa Sabratha.
Amesema wengi wa manusura hao ni wanaume lakini wamefanikiwa kuwaokoa wanawake tisa na watoto wawili.
Vyanzo vya habari mjini Zuwara zinasema kuwa miili ya watu mia moja zimehifadhiwa katika hospitali moja mjini humo.
\

tazama video ya lowasa na wanawake jana , aliwaahidi mambo lukuki ya mabadiliko.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...