Tuesday, 26 April 2016

kundi la watu 20 wa ash-Shabab wauawa na jeshi la Somalia


Wanapiganaji 20 wa ash-Shabab wauawa na jeshi la Somalia
Wapiganaji wa kundi la kigaidi na kitakfiri la ash-Shabab nchini Somalia wameuawa na askari wa serikali, kaskazini mwa nchi hiyo.
Ismail Khalifah Shira, kamanda wa jeshi la Somalia amethibitisha habari hiyo mapema leo na kuongeza kuwa, wanachama wa kundi hilo la kigaidi la ash-Shabab, wameuawa asubuhi ya leo katika eneo la Dainunay, lililopo karibu na mji wa Baidoa. Shira ameongeza kuwa, magaidi hao wameuawa baada ya kuvamia kambi ya jeshi la serikali katika eneo hilo kwa lengo la kutekeleza shambulizi la kushtukiza, na kwamba jaribio lao lilifeli baada ya askari kufahamu mapema njama hiyo na kuwaua magaidi hao katika eneo la tukio. Hata hivyo kamanda Ismail Khalifah Shira hakutaja hasara yoyote iliyopata jeshi katika hujuma hiyo. Hii ni katika hali ambayo kundi la ash-Shabab limedai kupata ushindi katika hujuma hiyo. Ripoti iliyotolewa na kundi hilo maarufu kwa kutenda jinai dhidi ya binaadamu, imedai kuwa wapiganaji wa ash-Shabab wamefanikiwa pia kudhibiti kambi ya kijeshi la eneo hilo la Dainunay. Aidha limeongeza kuwa, katika hujuma hiyo askari 10 wa serikali wameuawa.

Soma hii: Mapema hivi leo Al-Shabab wavamia na kudhibiti kambi ya jeshi Somalia


Shabab
Image copyrightAFP
Image captionWapiganaji wa al-Shabab wamekuwa wakishambulia kambi za jeshi miezi ya karibuni
Wapiganaji wa kundi la al-Shabab walishambulia kambi ya jeshi nchini Somalia na kuidhibiti kwa muda mapema asubuhi kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Wapiganaji hao walishambulia kambi ya Jeshi la Taifa la Somalia (SNA) katika eneo la Daynuunay, wilaya ya Baidoa katika jimbo la Bay.
Taarifa zinasema magari zaidi ya kumi ya jeshi la Somalia yaliuawa wakati wa shambulio hilo.
Msafara wa wanajeshi wa Somalia kutoka mji wa Baidoa, waliokuwa wakipelekwa kuwasaidia wenzao, pia ulishambuliwa.
Taarifa zinasema kulitokea vifo na majeruhi pande zote.
Afisa mmoja wa serikali eneo hilo ameambia BBC kwamba watu zaidi ya 10 walifariki.
Mwandishi mmoja wa eneo hilo ameambia BBC kwamba wanajeshi 20 waliuawa wakati wa shambulio hilo.
Kikosi cha Umoja wa Afrika (Amisom) kimesema kupitia Twitter kwamba shambulio hilo lilitokea lakini kikakanusha taarifa kwamba kambi hiyo ilidhibitiwa na wapiganaji hao.
Kambi hiyo inapatikana kilomita 30 kutoka mji wa Baidoa.
Al-Shabab wamezidisha mashambulio dhidi ya wanajeshi wa Amisom na Somalia tangu katikati mwa mwaka jana.
Mapema mwaka huu, walishambulia kambi ya wanajeshi wa Kenya wanaohudumu chini ya Amisom.
Al-Shabab wamesema kwamba waliua zaidi ya wanajeshi 200 katika shambulio hilo eneo la El-Ade katika jimbo la Gedo tarehe 15 Januari mwaka huu.

Majonzi: Lucy Kibaki afariki



Image captionLucy kibaki na mkewe wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2007
Mke wa kwanza wa rais Lucy Kibaki amefariki katika hospitali mmoja mjini London kwa ugonjwa usiojulikana.
Lucy alipata umaarufu kwa kumchapa kofi mpiga picha mmoja mwaka 2005 wakati alipovamia afisi za kituo kimoja cha habari mwaka 2005 akikasirishwa na vile habari moja ilivyoandikwa.
Katika kumbukumbu ya kumuhenzi bi Kibaki rais wa Kewnya Uhuru Kenyatta alimsifu kwa jukumu lake kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi nchini Kenya.
Image captionLucy Kibaki pamoja na aliyekuwa mke wa aliyekuwa rais wa Marekani George Bush ,Laura Bush.Picha kwa niaba ya Getty Images
Bwana Kenyatta alimrithi mumewe bwana Kibaki ambaye alitawala kutoka mwaka 2002 hadi 2013.
Bi Kibaki aliyezaliwa mwaka 1940,alijiondoa katika maisha ya hadharani wakati wa mwisho wa utawala wa mumewe.
Image captionLucy Kibaki na mumewe Mwai KIbaki wakiwapungia mkono wafuasi wao mda mchache baada ya kibaki kuwasilisha stakhabadhi zake za uchaguzi katika tume ya uchaguzi mwaka 2007.Picha ni kwa niaba ya Getty images
Mara ya mwisho kuonekana hadharani ni mwezi Agosti mwaka 2010,wakati alipofurahishwa na kupatikana kwa katiba mpya.
Image captionLucy Kibaki na mumewe aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki pamoja na mkewe marehemu Kijana Wamalwa wakati wa misa ya kifo cha Wamalwa.Picha kwa niaba ya Getty Images
Bwana Kenyatta alisema kuwa alikuwa mgonjwa kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita ambapo amekuwa akipata matibabu nchini Kenya na Uingereza.Bi Kibaki ni mwalimu ambaye aliwacha kazi yake kabla ya ndoa yake na kibaki mwaka 1962 ili kuwalea wanawe.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...