Saturday, 27 June 2015

lione gari alilopewa dogo aslay na mkubwa fella kama hukubahatika kuliona.





 aslay kwa furaha kubwa akasema haya: 

“Asante mungu Kwa kunipa uhai Na kipaji ambacho leo hii kina fanya naitwa Aslay pia nakushukuru kwa kunifikisha kwenye mikono Ya mtu mwenye moyo wa kibinaadamu. Najua kuna mengi makubwa ambayo boss wangu @mkubwafella umenifanyia ambayo si vyema kuyataja yote kwasababu wakati wake haujafikia ila naomba nichukue fulsa hii kukushukuru kwa hiki ulichonifanyia leo katika sherehe Ya kusherehekea siku yangu Ya kuzaliwa umenifanya nijione mwenye thamani kubwa duniani sikutegemea kama leo itakuwa siku yangu ya kumbukumbu ambayo sitoweza kuisahau hata Nije kuwa bilionea @mkubwafella asante kwa kunipa hii zawadi ambayo mimi kama mimi sikuiwazia kabisa kama Leo nitapata gari Na ninaushukuru uwongozi mziki Wa #mkubwanawanawe pamoja na manager wangu @chambusso boss wangu @babutale @mhtemba na mama yangu @sweatfella bila kuwasahau wasanii wenzangu wa @yamoto_band mungu





Mahakama Marekani yaruhusu ndoa za mashoga, ona wanavyoshangilia


Mahakama kuu nchini Marekani imetoa hukumu Ijumaa na kusema katiba ya nchi hiyo inatoa haki kwa wapenzi wa jinsia moja kuoana, na hivyo kutoa ushindi wa kihistoria kwa vuguvugu linalotetetea haki za mashoga.
Hukumu hiyo iliyopitishwa na majaji watano dhidi ya wanne imesema uhakikisho wa katiba wa ulinzi sawa chini ya sheria unamaanisha kuwa majimbo hayawezi kupiga marufuku ndoa za jinsia moja. Kufuatia hukumu hiyo, ndoa za jinsia moja zitakuwa halali katika majimbo yote 50 ya Marekani.
Jaji Anthony Kennedy, akiandika kwa niaba ya mahakama, amesema matumaini ya wapenzi wa jinsia moja wanaopanga kuoana ni kutengwa na kuishi maisha ya upweke, na kutenganishwa na taasisi za moja ya demokrasia za muda mrefu zaidi duniani. "Wanaomba heshima sawa mbele ya sheria. Katiba inawapa haki hiyo," amesema.
Kennedy ambaye hutoa kura ya maamuzi katika kesi katika kesi zenye mvuto mkubwa, aliungwa mkono na wengine wa majaji wanne waliberali wa mahaka hiyo. Kennedy ambaye aliteuliwa na rais Mrepublican Ronald Reagan mwaka 1988, hivi sasa ameandika hukumu zote muhimu nne kuhusu haki za mashoga, ambapo ya kwanza ilikuja mwaka 1996.
Wapinzani wa ndoa za jinsia moja wakiandamana mbele ya mahakama kuu. Wapinzani wa ndoa za jinsia moja wakiandamana mbele ya mahakama kuu.
"Bila kutambuliwa, utulivu na kutabirika kwa ndoa, watoto wao watateseka na unyanyapa wa kujua kuw afamilia zao haziko sawa na nyingine," aliandika Kennedy. Katika maoni yanayokinzana, jaji mhafidhina Antonin Scalia, alisema uamuzi huo unaonyesha kuwa mahakama hiyo ni tishio kwa Wamarekani.
Jaji mkuu wa Marekani, mhafidhina John Roberts, alisoma muhtasari wa upinzani wake kutokea nje ya chemba la majaji, hii ikiwa mara ya kwanza kwake kufanya hivyo katika kipindi cha miaka 10 aliokaa katika mahakama hiyo. Roberts alisema ingawa zipo hoja za nguvu kisera katika suala la ndoa za jinsia moja, halikuw ajukumu la mahakama hiyo kuyalaazimisha majimbo kubadili sheria zake za ndoa.
Obama, Clinton washerehekea, Republican walaani
Rais Barack Obama, ambaye ni rais wa kwanza alieko madarakani kuunga mkono waziwazi ndoa za jinsia moja, alisifu hukumu hiyo, akisema kwenye mtandao wake wa twitter kuwa siku ya leo ni hatua muhimu katika safari ya kuhakikisha usawa kwa watu wote.
Naye Hillary Clinton, mgombea anaepewa nafasi kubwa kupitishwa na chama Demokratic kuwania urais mwaka 2016, aliandika kwenye mtandao wake wa twitter kuwa "Najivunia kusherehekea ushindi wa usawa wa ndoa." Hadi mwaka 2013, Clinton alisema alikuwa anapinga ndoa za jinsia moja, lakini alibadili mtazamamo wake tangu wakati huo.
Rais Barack Obama ameitaja hukumu hiyo kuwa ni ushindi wa usawa nchini Marekani. Rais Barack Obama ameitaja hukumu hiyo kuwa ni ushindi wa usawa nchini Marekani.
Mgombea wa chama cha Republican Mike Hackabee alisema, uamuzi huu wa udanganyifu ni uababe wa mahakama unaokwenda kinyume na katiba." Mgombea mwingine wa Republican Jeb Bush aliongeza kuwa, " nikiongozwa na imani yangum naamini katika ndoa za asili. Naamini mahakama kuu ilipaswa kuyaruhusu majimbo yafanye uamuzi huu.
Ndoa za jinsia moja zilikuwa zinaruhusiwa katika majimbo 36 ya Marekani pamja na Washington DC. Katika jimbo la 37 la Alabama, mahakama iliondoa marufuku dhidi ya ndoa za jinsia moja, lakini mahakama ya rufaa iliwazuwia maafisa wa serikali kutoa leseni kwa wapenzi wa jinsia moja.
Wapinzani wa ndoa hizo wanasema uhalali wake unapaswa kuamuliwa na majimbo yenyewe, na wengine wanasema kuruhusiwa kwa ndoa hizo ni dharau kwa ndoa ya asili kati ya mwanamume na mwanamke, na kwamba Biblia inalaani mahusiano ya jinsia moja.
Hisia juu ya hilo zilikuwa juu wakati wa mjadala mahakamani mwezi April katika kesi hiyo, pale mwandamanaji alipowapigia kelele majaji na kuwambia wataozea jahanam ikiwa watapitisha hukumu kuunga mkono ndoa za jinsia moja.

hii ndio nyimbo pekee nyingine kutoka tanzania inayooneshwa television za marekani

kama nyimbo za mungu hii ni nzuri kupita yoyote unayoijua tanzania. ni mpya . angel benard, download hapa kwa hisani ya innosam

ona kavani alivyopigwa kidole na kuongezwa kadi nyekundu juu.

tazama video na nyimbo mpya p square kama hujaiona. nishidaaaaaaaaa kutoka marekani

tazama video ya huyu mrembo akipiga picha na kukosa pozi baada ya kitu kidogo kumzingua.











WATU 27 WAUWAWA KWA SHAMBULIO HUKO KUWAIT . ONA VIDEO NA PICHA YAKE HAPA





Kuwait yaomboleza vifo vya watu 27

Maombolezi yanaendelea nchini kuwait kuwakumbuka watu 27 waliouawa kwenye shambulizi la kujitoa mhanga kwenye msikiti wa kishia.
Wakati huo huo msemaji wa kampuni ya kitaifa ya mafuta nchini kuwait anasema kuwa usalama umedumishwa katika vituo vyote vya mafuta kote nchuni humo baada ya shambulizi ambalo Islamic State wanasema kuwa walihusika.
Islamic State huwaita waislamu wa madhehebu wa shia kuwa wazushi na hivi majuzi walishambulia misikiti yao miwili katika nchi jirani ya Saudi Arabia.







CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...