Saturday, 13 June 2015

hivi ndivyo alivyovaa wema sepetu usiku huu wa leo hapa mlimani city

miss tanzania siti mtemvu alievuliwa taji nusura ajiue mwenyewe .atoa tamko zito.

Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu aliyeamua kulitema taji hilo baada ya kubebeshwa kashfa amesema kuna wakati alitaka kujiua lakini alirudisha moyo nyuma na kuona ingekuwa shida kubwa nyumbani kwao.

“Sikuwa na amani, niliishi maisha ya hofu, kujifungia ndani, kulia wakati wote. Ilifikia hatua baba yangu alipata mshktuko kiasi cha kwenda kutibiwa Afrika Kusini. Mama yangu pia alipata mshtuko…ningeweza kumpoteza.”—Sitti Mtemvu.

“Mama yangu alisali na mimi, alinipigania, hakuonyesha hadharani jinsi gani anaumia, lakini ukweli ni kwamba nilimwona alivyokuwa anadhoofu na kukosa raha. Nyumba yetu iligeuka sehemu ya huzuni, amani ilitoweka ni kama tulikuwa na msiba.”—Sitti Mtemvu.

Sitti anasema siku moja mama yake alimwambia kwamba aliumia siku alipompoteza mama yake lakini machungu aliyoyasikia kwa Sitti ni mazito zaidi japo baba yake wakati wote alivumilia na hakuonesha maumivu yake.

Anasema kuna wakati baba yake alikwenda Afrika Kusini na akiwa huko alimtumia ujumbe wa kumuomba msamaha na alimwambia kwamba hizo ni changamoto.

Sitti anasema alikuwa katika wakati mgumu kiasi cha kufikia uamuzi wa kutupa laini yake ya simu ya zamani.

hii hapa jinsi ya kutazama live tuzo za kili music zinavyoendelea kusherekewa hivi sasa na kutolea hapa mlimani city

watch-live-stream
Zimebaki saa chache tu kushuhudia historia nyingine kwenye Industry ya Muziki Tanzania ikiandikwa.. Jana JUNE 12 2015 ulitangazwa utaratibu mpya ambapo tofauti na miaka ya nyuma, safari hii zimetolewa Kadi Maalum za Mwaliko kwa wageni wote watakaoingia pale Ukumbi wa Mlimani City.
Haimaanishi kwamba ulie nyumbani ndio umepitwa, Clouds TV itakuwa ikirusha Live.. lakini pia urahisi mwingine ni huu, kuna hii link hapa ambayo ukiibonyeza itakupa nafasi na wewe kushuhudia LIVE popote ulipo hata kwa kifaa kama simu ya mkononi >>>http://livestream.com/accounts/4180642/events/4119876/player?width=960&height=540&autoPlay=true&mute=false

kuelekea kili music awards leo usiku ,haya ndio mabadiliko yaliyotokea hivi punde.


Screen Shot 2015-06-12 at 6.17.31 PM
Leo June 12 2015 tunahesabu saa chache tu kushuhudia Historia ikiandikwa kwenye Burudani ya Muziki TZ, Tuzo kubwa za Muziki Tanzania, KTMA 2015 leo kuna kipya kilichotangazwa na waandaaji wa Tuzo hizo.
Kuna mabadiliko machache tofauti na ilivyokuwa mwaka jana… tumebadilisha mpangilio wa Venue ambao kwa mwonekano watu wote wataangalia mbele… mbali na hayo baada ya Show tumeandaa sherehe ambayo itawajumuisha watu wote kuburudika kwa pamoja tofauti na kipindi kilichopita“>>> Pamela Kikuli
Pia tofauti iliyopo ni kwamba hakutakuwa na utaratibu wa watu kulipia na kuingia kwenye show badala yake watahudhuria wale ambao wamepokea mwaliko tu“>>>
Tumeona sio vibaya kupokea maoni kutoka kwa wadau mbali mbali ambao wanafuatilia Show hizi ndio sababu iliyotufanya tufanye mabadiliko makubwa kwenye show hii kwa mwaka 2015“>>> Pamela Kikuli.
Screen Shot 2015-06-12 at 6.16.58 PM
Pamela Kikuli
Screen Shot 2015-06-12 at 6.17.41 PM
Sauti ya Pamela Kikuli iko hapa.

Ads Separator

ray c alia machozi leo bila msaada wowote. inasikitisha sana, muone na ujue kilichompata


Ray Cleo katika Ukurasa wake wa Instagram na kupost video tatu… analalamika kwamba yuko Hospitali na amekosa dawa.
Nashindwa kuvumilia, niko hapa kitengo cha madawa. Mpaka sasa hivi sijapewa dawa, kwa sababu nilipost ile post nyingine wananifanyia kama makusudi.. Nikikosa dawa wanataka nirudi kuvuta unga?
Wana maamuzi yao lakini unakuta mtu umechelewa kama mimi natoka Bunju kila siku lazima niweke mafuta ya elfu 30 unawaambia nina tatizo bado ukifika unaambiwa imekuwa kama shule
Ile dawa inauma.. Mwili unauma nasikia baridi mifupa inauma.. alafu wanajua lakini wanatunyima

Korea Kusini yakumbwa na ugonjwa wa homa ya ajabu sana.soma hii


Homa ya MERS yasambaa Korea Kusini
Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa mlipuko wa homa ya Middle East Respiratory Syndrome au MERS nchini Korea Kusini na mkubwa na huenda kesi zaidi zikaripotiwa.
Baada ya uchunguzi wa wiki moja shirika la WHO linasema kuwa madaktari nchini korea kusini ambao hawakuhufahamu ugonjwa huo huenda walichangia ugonjwa usambae kwa haraka .
Utawala nchini korea kusini unasema kuwa watu 12 wameambukizwa ugonjwa wa MERS huku 14 wakijulikana kuaga dunia.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...