Monday, 13 July 2015

tazama hii,goal keeper wa congo ,kidiaba katika kushangilia kwa matako na historia yake videoni.

SAFARI YA UCHAGUZI-2015

Polisi 4 wauawa Tanzania usiku wa leo katika shambulizi la kushtukiza ukonga jijini dar es salaam






Polisi 4 wauawa katika shambulizi Tanzania

Maafisa wanne wa polisi na raia wawili wameuawa baada ya watu wasiojulikana kuvamia kituo cha polisi mjini Dar es salaam Tanzania.
Shambulizi hilo limetokea katika kituo cha polisi kilichoko Ukonga, viungani mwa jiji kuu la Dar es salaam.
Polisi wanasema kuwa wavamizi hao walitekeleza shambulizi hilo la kuvizia usiku wa kuamkia leo.
Waliwafyatulia risasi maafisa wa polisi katika kituo hicho na kuua wanne.
Hadi sasa haijabainika iwapo kuna majeruhi.
Aidha inasemekana kuwa walipora handaki ya kituo hicho na kuiba bunduki 30 za polisi na idadi ya risasi isiyojulikana.
Hakuna aliyekamatwa kufuatia shambulizi hilo japo maafisa wa upelelezi wanaendelea na uchunguzi.
Polisi wanawahutubia waandishi katika kituo hicho.
Hakuna kundi lililokiri kutekeleza shambulizi hilo.

baada ya usajili wa Schweinsteiger sasa ni zamu ya Schnederlin, tayari makubaliano yake.

Man United na Southampton wamekuwa na mazungumzo kwa muda wa wiki kadhaa sasa na hatimaye vilabu hivyo usiku wa kuamkia leo vilikubaliana bei ya uhamisho ya £25m kwa ajili ya Schnederlin.
Southampton walithibitisha kuikataa ofa ya kwanza ya Man United mapema wiki iliyopita, lakini yakiwa yamebaki masaa kadhaa kabla ya United kwenda kwenye Tour, hatimaye klabu hiyo imekubali ofa ya United.
   Schneiderlin aliyejiunga na Southampton mwaka 2008 akitokea Strasbourg kwa ada ya uhamisho wa £1.2m – jana usiku alifanyiwa vipimo vya afya na United na leo hii kabla ya safari wanategemea kutambulishwa rasmi yeye na mwenzie Bastian Schweinsteiger.

kauli ya mafisadi kutoka kwa DR magufuli hii hapa baada ya ushindi wake.

huzuni kwa mashabiki wa vichekesho . mzee ojwang afariki dunia hivi punde.



ojuwang
Muigizaji Benson Wanjau wa Kenya maarufu kama Mzee Ojwang wa vipindi kama Vitimbi, Vioja Mahakamani, Vituko, Kinyonga na vingine vingi afariki dunia jana Usiku akiwa amelazwa hospitali ya taifa ya Kenyatta National Hospital. Mzee Ojwang alikuwa anasumbuliwa na Pneumonia.
ojwang3
Wakenya wengi wameguswa na msiba huu huku baadhi ya watu wakipost ujumbe tofauti kwenye mitandao wa Twitter kuonyesha kuguswa kwa msiba huu wa aliekuwa mchekeshaji mkongwe wa Kenya.
Mzee Ojwang amefariki akiwa na miaka 78.

Kenya yashinda dhahabu .kimichezo wako vizuri sanaaaaaaaaaaaaa


Kenya ndio mabingwa wa taji la voliboli katika Grand Prix
Timu ya Kenya ya voliboli ya wanawake ndio mabingwa wa mwaka huu wa mashindano ya Grand Prix.
Kenya imesajili ushindi mkubwa wa seti 3-1 dhidi ya Peru katika fainali ya mashindano ya voliboli ya wanawake ya Grand Prix kundi la tatu mjini Canberra, Australia Jumapili.
Kenya ilisajili ushindi wa alama 21-25, 25-17,25-22 na kisha 25-23.
Kufuatia ushindi huo Kenya ndiyo nchi ya kwanza ya Afrika kushinda taji la Grand Prix, ushindi ambao sasa umewapandisha kidada hao Malkia hadi kundi la pili.
Kenya imesajili ushindi mkubwa wa seti 3-1 dhidi ya Peru
Mercy Moim alikua nyota wa Kenya kwa kuipatia timu yake pointi 22 akifuatiwa na Ruth Jepngetich pointi 17 .
Kwa upande wa Peru Levvy Angela aliongoza na pointi 26.
Mamia ya Wakenya wanaoishi Australia wakiongozwa na balozi wa Kenya nchini humo Isaiah Kabira waliwashangilia warembo hao wa Kenya waliovalia mavazi ya kuvutia ya rangi nyeupe na kijani kibichi.



 null


Mercy Moim alikua nyota wa Kenya kwa kuipatia timu yake pointi 22
Peru ilishinda seti ya kwanza 25-21 lakini katika seti ya pili Kenya ilichangamka na kuibuka mshindi 25-17 na kutoka hapo Peru, ambao wanashiriki mashindano haya ya Grand Prix kwa mara ya nne, hawakuweza tena kutetemesha kina dada wa Kenya walioshinda seti zifuatazo 25-22 na 25-23.
Huku wachezaji wa Kenya wakidondokwa na machozi ya furaha, Peru nao waliambulia kilio cha kuchapwa na mabingwa wa Afrika kwani waliingia uwanjani na matumaini makubwa ya ushindi ikikumbukwa kwamba walishinda Kenya katika raundi ya kwanza nchini Mexico.
''Huu ndio mwanzo wa matokeo mengine bora zaidi katika mashindano ya dunia,'' anasema nahodha wa Kenya Praxidis Agala

 null






Nahodha wa Kenya Braxcedes Khadambi ameomba serikali ufadhili zaidi
''Ushindi wetu unadhihirisha wazi kwamba sio riadha tu ndio mchezo Kenya inafanya vyema.''
''Tunashukuru Wakenya wanaoishi hapa kwa kutushangilia kuanzia mwanzo hadi mwisho.''



 null




Kenya ndio taifa la kwanza Afrika kutwaa taji hilo
Kocha wa Kenya David Lung'aho anasema:
''Tuko tayari kupambana na miamba ya dunia.''
''Tulitizama kwa makini kanda za mechi za Peru walizocheza na tukapata mbinu ya kuwabana''.
Kenya sasa inajiandaa kwa kombe la dunia litakalokuwa Japan
''Sasa tuanaangazia kombe la dunia nchini Japan na michezo ya mataifa ya Afrika nchini Congo Brazaville mwezi wa Septemba.''
Kenya ilishiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano ya Grand Prix mwaka jana na kumaliza nafasi ya tano katika kundi la tatu.





 null
Wakenya wanaoishi Australia waliwashabikia Malkia
Ushindi wao dhidi ya Peru umepokewa kwa vishindo na mashabiki nchini Kenya baadhi yao kwenye mtandao wa Facebook wakimuomba Rais Uhuru Kenyatta awape siku moja ya kupumzika wakailaki timu ya Kenya.
Kulingana na mwenyekiti wa shirikisho la voliboli nchini Kenya, Waithaka Kioni, timu ya Kenya huenda ikarudi nyumbani Jumanne usiku.
Kioni ameiomba serikali itoe fedha za kuwawezesha kufanya mazoezi ng'ambo kabla wasafiri kwa kombe la dunia na michezo ya mataifa ya Afrika.

baada ya Van Persie kuondoka man united tuko timu hii hapa na sio iliyotajwa na kudhaniwa.


 




Van Persie akipokelewa Uturuki
Mashabiki wa manchester United wengi walijua kuwa Van Persie anaondoka kuelekea Fenabashe lakini kwa mtoto mdogo mwingereza wa miaka minne Louis Diamond hakufahamu kuwa kipenzi chake Robin Van Persie anaondoka mpaka pale alipoambiwa na wazazi wake kwamba mpachika magoli Robin alikuwa tayari kuelekea uturuki. Hivi sasa waturuki wameanzisha kampeni ya kuchangishana pesa ili mtoto huyo ambaye video yake imesambaa mitandaoni na kutizamwa na watu wengi aletwe Uturuki kumshuhudia mchezaji huyo.
Shabiki huyo mdogo wa miaka minne alipoambiwa na wazazi wake kuwa Van Persie alirekodiwa na baba yake akilia sana na video yake imesambaa mitandaoni duniani kote.
"hatujamwambia kama video yake imesambaa duniani, tumemwambia tu kuwa tumewaonyesha marafiki zake tu hapa mtaani tu hajui kama ni dunia nzima, mimi na mke wangu tuna hamu ya kumwona atakavyocheka tukimwonyesha video hii miaka kumi baadaye" Alisema baba wa mtoto huyo.
Kuna uwezekano pesa iliyopangwa kuchangwa mashabiki wa uturuki ikazidi kiwango cha pauni 1200 za uingereza kilichokusudiwa kumsafirisha mtoto huyo na baba yake ili kuja kushuhudia mechi ya kwanza ya Van Persie nchini uturuki.
Ni vema pia mtoto akapozwa kwa kuambiwa kuwa kinakuja chuma kipya kutoka southampton, Morgan Shineidelini ambaye atafanya vipimo Man U.
Kwa upande mwingine Liverpool inachukua kitita cha pauni milioni 49 kumuuza Raheem Sterlin kuelekea Man City na kumfanya kijana huyo mdogo wa miaka 20 kuwa mchezaji wa ghali zaidi katika england.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...