Monday, 24 September 2018

Boban achimba mkwara kwa wanaoibeza Lyon

Nahodha wa African Lyon Haruna Moshi amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu
Nahodha wa AFRICAN LYON, HARUNA MOSHI maarufu kama BOBAN amesema licha ya kupoteza mchezo dhidi ya MTIBWA SUGAR bado wanaimani kikosi chao kipo kwenye kiwango kizuri kitakachowawezesha kumaliza ligi katika nafasi za juu.

MOSHI anasema timu yao ina mchanganyiko wa wachezaji vijana na wakongwe wenye uwezo wa kupata matokeo wakati wowote hivyo mashabiki wa timu hiyo wasikate tamaa kwani wao kama wachezaji wapo tayari kupambana mpaka tone la mwisho .

Mpaka sasa AFRICA LYON imeshacheza michezo SITA ya ligi kuu msimu huuu ambapo imeshinda mchezo MMOJA na kupoteza michezo MITATU huku ikitoka sare katika michezo MIWILI. 

Modric awabwaga Ronaldo na Salah tuzo za FIFA

Luca Modric ametangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa FIFA katika hafla ilifanyika kwenye ukumbi wa Royal Festival mjini London
Kiungo wa kimataifa wa CROATIA, LUCA MODRIC ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa FIFA baada ya kuwashinda CRISTIANO RONALDO na MOHAMED SALAH.

Nyota huyo anayechezea REAL MADRID aliisaidia klabu hiyo kushinda mataji MATATU mfululizo ya ligi ya mabingwa barani ulaya pamoja na kulisaidia taifa lake la CROATIA kufika fainali ya kombe la FIFA la dunia.

Ronaldo na Messi wameshinda tuzo zote kubwa tangu mwaka 2008
Hii ni mara ya kwanza baada ya miaka 10 kupita tuzo kubwa duniani kunyakuliwa na mchezaji tofauti ya RONALDO na MESSI ambapo mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2007 pale mbrazil RICARDO KAKA lisposhinda tuzo ya Balon d’or.

Kwa upande wa goli bora la mwaka tuzo imeenda kwa MOHAMED SALAH wa LIVERPOOL ambapo bao lake alilofunga dhidi ya EVERTON mwezi DESEMBA mwaka jana limeteuliwa kuwa goli bora la mwaka.

Salah akifunga goli lililoshinda tuzo ya goli bora la FIFA dhidi ya Everton mwezi Desemba mwaka jana 
Ushindi huo hata hivyo umeibua mjadala hasa kutokana na ubora wa magoli mawili yaliyoshindwa likiwemo goli la CRISTIANO RONALDO dhidi ya JUVENTUS na lile la GARETH BALE dhidi ya LIVERPOOL katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya.

Tuzo ya kocha bora wa mwaka imeenda kwa DIDIER DESCHAMP wa UFARANSA aliyewashinda ZINEDINE ZIDANE na ZLADKO DALIC wa CROATIA.

Kocha wa zamani wa Arsena Arsene Wenger akimkabidhi tuzo ya kocha bora Didier Deschamp

 Tuzo ya mchezaji bora wa kike ikienda wa MARTA wa BRAZIL ambaye ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya SITA mfululizo. 
Marta mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa kike 

Tuzo ya mashabiki bora ikienda kwa mashabiki wa timu ya taifa ya PERU. Zaidi ya mashabiki arobaini elfu wa Peru walisafiri hadi Russia kuishuhudia timu yao ya taifa ikicheza fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 36.
Mashabiki wa Peru wakiishangilia timu yao huko Russia

Salah na Courtois waachwa kwenye kikosi bora cha FIFA licha ya kutwaa Tuzo katika hafla hiyo
Kikosi bora cha FIFA

Mtibwa Sugar wapania mataji zaidi

Kocha wa Mtibwa Sugar Zuber Katwila
Kocha wa MTIBWA SUGAR, ZUBER KATWILA amesema kama ilivyokuwa msimu uliopita kikosi chake kina malengo ya kunyakua taji mojawapo msimu huu miongoni mwa mashindano wanayoshiriki.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya MTIBWA na AFRICAN LYON, KATWILA anasema wana kikosi kipana walichokiandaa vyema kwaajili kuwania mataji hivyo anaamini msimu huu hawatatoka patupu. 

Katika mchezo wa jana uliochezwa kwenye dimba la uhuru jijin DSM MTIBWA waliwanyuka wenyeji AFRICAN LYON mabao MAWILI kwa BILA mabao yote yakifungwa na RAJAB ZAHIR na msimu uliopita walifanikiwa kunyakua ubingwa wa michuano ya kombe la shirikisho la soka nchini.

MBAO FC yazidi kutakata Ligi Kuu Bara



Wabishi wa jiji la MWANZA, MBAO FC wamekwea kileleni kwenye msimamo wa ligi baada ya kuibuka na ushindi wa bao MOJA kwa BILA dhidi ya maafande wa jeshi la magereza nchini TANZANIA PRISONS.

Katika mchezo huo ulichezwa kwenye dimba la CCM KIRUMBA timu zote mbili zilitandaza kabumbu safi lakini bahati ilikuwa kwa MBAO ambao walipata bao la ushindi katika daika za lala salama likipachikwa kimiani na NDAKI ROBERT.

Matoke hayo yanawafanya MBAO kufikisha alama 13 baada ya kushuka dimbani mara SITA ambapo wameshinda michezo MINNE na kupoteza mchezo MMOJA huku wakitoka sare katika mchezo MMOJA.

Huko NANGWANDA SIJAONA mjini MTWARA wenye NDANDA FC wamekiona cha moto baada ya kutandikwa mabao MATATU kwa MOJA na chama la wana STAND UNITED matokeo yanayowafanya NDANDA kusalia katika nafasi ya 12 na alama zao SABA huku STAND wakipanda hadi katika nafasi ya NANE wakiwa na alama TISA.

Msimao wa Ligi Kuu baada ya michezo 3 ya jana

#StandingsPPts
1Mbao FC613
2Young Africans SC412
3Azam FC511
4Simba SC510
5Mtibwa Sugar FC610
6JKT Tanzania69
7Coastal Union69
8Stand United FC69
9Biashara United68
10Kagera Sugar FC57
11Mbeya City FC67
12Singida United FC67
13Ndanda FC67
14KMC56
15Lipuli FC46
16African Lyon66
17Tanzania Prisons FC65
18Ruvu Shooting FC52
19Mwadui FC52
20Alliance FC61

SIMBA & YANGA JOTO LISILOPIMIKA

Michezo ya Ligi Kuu leo Sept 24
Wakati kivumbi cha ligi kuu TANZANIA BARA kikiendelea leo Jumatau kwa michezo kadhaa kuchezwa vigogo wa soka nchini SIMBA na YANGA wao wapo kwenye mapumziko kujiwinda na pambano lao la SEPTEMBA 30.

Baadhi ya Matokeo ya michezo ya juma lililopita

Msimamo wa TPL kabla ya michezo ya leo Sept 24

#StandingsPPts
1Young Africans SC412
2Azam FC511
3Simba SC510
4Mbao FC510
5JKT Tanzania69
6Coastal Union69
7Biashara United68
8Kagera Sugar FC57
9Mtibwa Sugar FC57
10Mbeya City FC67
11Singida United FC67
12Ndanda FC57
13KMC56
14Lipuli FC46
15African Lyon56
16Stand United FC56
17Tanzania Prisons FC55
18Ruvu Shooting FC52
19Mwadui FC52
20Alliance FC61



CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...