Monday, 24 September 2018

BARCELONA CHUPUCHUPU KUANGUKIA PUA

Gerard Pique akishangilia baada ya kufunga bao la kusawazisha
Gerard Pique amefanya kazi ya ziada kuinusuru FC Barcelona na kipigo mbele ya Girona kwenye Catalan derby baada ya kuifungia bao la kusawazisha na kufanya matokeo kuwa sare ya mabao 2-2.
mpaka dakika ya 35 Barca walikuwa wakiongoza kwa bao 1 wakati beki Clement Lenglet akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kiwiko Pere Pons kabla ya Girona kusawazisha kupitia kwa Cristhian Stuani ambaye pia alifunga bao la pili katika dakika ya 51.
Christian Stuan aliifungia Girona mabao mawili dhidi ya Barcelona
licha ya kucheza pungufu BARCA walipambana na Pique ndiye alikuwa shujaa baada ya kufunga bao la kichwa lililoipa Barca alama moja kwenye dimba la Camp Nou na sasa wanaongoza ligi kwa tofauti ya mabao baina yao na Real Madrid ambao waliinyuka Espanyol bao 1-0 siku ya jumamosi.


Baadhi ya matokeo ya la liga 23 SEPTEMBER 2018

Msimamo wa La Liga baada ya michezo ya weekend hii

TeamPGDPts
1Barcelona51113
2Real Madrid5913
3Alavés5310
4Celta Vigo528
5Atl Madrid518
6Girona5-18
7Sevilla547
8Espanyol517
9Real Sociedad507
10Getafe507
11Eibar5-17
12Ath Bilbao416
13Real Betis5-26
14Villarreal5-15
15Valencia5-24
16Levante5-34
17Huesca5-74
18Real Valladolid5-23
19Rayo Vallecano4-73
20Leganés5-61
@BBC

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...