Monday, 20 June 2016

nchi ya Urusi yapinga makubaliano ya kuumaliza ugomjwa wa UKIMWI


Symbolbild Aids

Umoja wa Mataifa umekubaliana kuongeza jitihada za kumaliza janga la UKIMWI, ifikapo mwaka 2030, ingawa Urusi imetaka kutowalenga zaidi watumiaji wa dawa za kulevya na wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Makubaliano hayo ya kisiasa yamefikiwa na wanachama 193 katika mkutano mkuu, ulioweka msisitizo juu ya mahitaji ya kuwasaidia wanaotumia dawa za kulevya kwa kujidunga sindano, wanaojihusisha na biashara ya ngono, wanaobadilisha jinsia na wafungwa amabo wapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya virus UKIMWI.
Maambukizo ya Virusi vya UKIMWI yamekuwa yakipungua katika muongo mmoja uliopita, lakini bado kuna kiasi ya watu Milioni 36.7 duniani kote wanaoishi na Virusi vya UKIMWI ama UKIMWI, na wengi wao wakiwa katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambako Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI, UNAIDS, Michel Sidibe amesema ndiko kuna idadi kubwa ya watu wanaotumia dawa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amewaambia wajumbe wa mkutano huo kwamba UKIMWI bado ni tishio, kwa hiyo mataifa bado yana nafasi ya kuhakikisha yanabadilisha hali ya janga hilo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Ban ametaka kutolewa kwa huduma na dawa kwa watu wote wanaoishi na Virusi vya UKIMWI bila ya ubaguzi. Aliwalenga zaidi vijana wadogo, wahamiaji, wanawake na wasichana, wanaofanya biashara ya ngono, wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, wanaojidunga dawa za kulevya, wanaobadilisha maumbile na wafungwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS,Michel Sidibe amesema idadi ya watumiaji dawa Barani Afrika inaridhisha
Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Michel Sidibe amesema idadi ya watumiaji dawa Barani Afrika inaridhisha
Makubaliano haya yanatokana na mipango ya awali ya Umoja wa Mataifa kuhusu UKIMWI yaliyopitishwa miaka mitano iliyopita, kwa kuweka msisitizo zaidi kwa kwale walioko kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi. Makubaliano hayo yamelenga maeneo matatu yanayootakiwa kufikiwa ifikapo mwaka 2020, ambayo ni kupunguza maambukizi mapya ya Virus vya UKIMWI, kupunguza idadi ya vifo na kuondoa unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI.
Urusi ilitaka mabadiliko ya mkakati huo mpya kuangazia sheria za kitaifa na namna zinavyoyataja makundi ya wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, watumiaji wa dawa za kulevya na wafungwa. Walisema wanadiplomasia na makundi ya kiraia, Jumanne hii.
Mabadiliko hayo yalipingwa vikali kutokana na hofu kwamba yataruhusu Urusi, Iran na nchi nyingine zinazochukulia mapenzi ya jinsia moja kama uhalifu kuzuia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI na huduma nyingine kwa wanaume hao.
Mkutano huo wa siku tatu, ulianza kwa ombi la mjukuu wa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, Indaba ambaye baba yake alikufa kwa UKIMWI mwaka 2005, akiwataka viongozi wa nchi 35 zinazozuia watu walioathirika kuingia nchini mwao, ikiwa ni pamoja na Urusi na Singapore kuondoa marufuku hiyo.

kikundi cha Al shabaab chawaua polisi 5 Mandera Kenya hivi punde.


Image copyrightAP
Image captionAl shabaab waua polisi 5 Mandera Kenya
Maafisa 5 wa polisi wa Kenya wameuawa mapema leo mjini Mandera katika shambulizi lililotekelezwa na wapiganaji wa kundi la wanamgambo la Al shabab kutoka Somalia.
Kamishna wa jimbo hilo la kaskazini mashariki mwa Kenya bwana Job Borongo ameithibitishia BBC kuwa wapiganaji hao walifanya shambulizi la kuvizia dhidi ya msafara wa magari ya polisi uliokuwa ukienda El Wak wakitumia guruneti.
Maafisa hao tano waliangamia papo hapo huku gari walimokuwa wakisafiria likiharibiwa kabisa.
Maafisa wengine wanne wamejeruhiwa vibaya.
Msafara huo wa polisi ulikuwa ukitoa ulinzi kwa msafara wa mabasi ya uchukuzi wa umma, desturi iliyoanzishwa baada ya wapiganaji hao kuteka basi moja na kuua abiria 28 wakristu.
Gavana wa Mandera bwana Ali Roba aliwalaumu maafisa wa polisi katika eneo hilo kwa kupuuza tahadhari iliyotolewa na wenyeji kuhusiana na mashambulio ya kigaidi.
Image copyright
Image captionMaafisa hao tano waliangamia papo hapo huku gari walimokuwa wakisafiria likiharibiwa kabisa.
Roba anasema walipuuza vyanzo vya kiintelijensia vilivyotolewa kuhusiana na kuonekana kwa wapiganaji hao waliojihami.
Hii si mara ya kwanza Mandera kushuhudia mashambulizi ya al shabaab.
Shambulizi hilo la Novemba mwaka wa 2014 liliwaacha wasafiri wengi wasiokuwa waislamu na hofu ya kusafiri na hivyo kuilazimu serikali kutoa usalama kwa mabasi ya uchukuzi wa umma.
Mwezi mmoja baadaye wapiganaji hao waliwaua wachimba migodi 36 katika eneo hilo la Mandera.
Kundi hilo la wapiganaji wa kiislamu limekuwa likitekeleza mashambulizi katika maeneo ya kaskazini mwa Kenya likitaka kuishinikiza taifa hilo jirani kuondoa majeshi yake nchini Somalia.
Image captionGavana wa Mandera bwana Ali Roba aliwalaumu maafisa wa polisi katika eneo hilo kwa kupuuza tahadhari iliyotolewa na wenyeji
Kenya ilipeleka vikosi vyake vya jeshi nchini Somalia mwaka wa 2011 ikitaka kuzima mashambulizi ya mara kwa mara.
Hata hivyo kundi hilo limeongeza mashambulizi nchini kenya ikiwemo mauaji ya watu 67 katika maduka ya Westgate mjini Nairobi mwaka wa 2013.
Mwaka uliopita Al Shabab ilitekeleza mashambulizi katika chuo kikuu cha Garissa na kusababisha vifo vya wanafunzi 148

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...