Wednesday, 29 June 2016

Watu zaidi ya 36 wauawa Uturuki



Image copyrightGETTY
Image captionWatu 36 wauawa Uturuki
Watu 36 wameuawa katika shambulio la kujitoa muhanga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ataturk Istanbul nchini Uturuki,na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa
Shughuli za usafirishaji katika uwanja huo zimesitishwa huku shughuli ya uokoaji na huduma ya kwanza vikiendelea..
Gavana wa mji wa Istanbul amethibisha kuuawa watu hao 32 na idadi hiyo ya majeruhi.
Image copyrightREUTERS
Image captionLango la uwanja wa ndege
Mashuhuda wanasema waliwaona washambuliaji watatu,ambapo mmoja kati yao alikuwa akifyatua risasi kabla ya kujitoa muhanga kwa kujilipua kwa bomu na kufa.
Hata hivyo mashambulizi hayo yalihusisha katika eneo la kuingia katika uwanja huo.
Rais wa Uturuk Recep Tayyip Erdogan amelaani shambulio hilo na kusisitiza umoja katika kutokomeza vitendo hivyo.
Uturuki imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi ya kigaidi kutoka pande mbili,kwanza kutoka kwa kundi la Islamic State wanaoingia kutoka nchi jirani ya Syria na waasi wa Kikurud wanataka kuunda dola yao.

vyama vya Upinzani Tanzania watishia kumshtaki rais Magufuli ICC uholanzi

File:Chadema bendera.jpg
Polisi katika kisiwa cha Pemba visiwani Zanzabar nchini Tanzania imepinga vikali kuwa inavunja haki za binadamu kwa kuwatesa na kuwashikilia wapinzani.
Hata hivyo limekiri kuwashikilia baadhi ya wapinzani kwa madai kwamba ni wahalifu.
Hapo jana Muungano wa Upinzani nchini Tanzania ulitoa kauli ya kulaani Polisi huko Pemba kwamba imekuwa ikiwapiga, kuwatesa na kuwafungulia kesi za bandia wafuasi wa upinzani .
Muungano huo tayari umetishia kumpeleka Rais wa Tanzania John Magufuli kwenye mahakama ya kimataifa ya ICC iwapo hataingilia kati mgogoro huo unaoendelea visiwani humo.
Kutoka Dar es Salaam mwandishi wetu Regina Mziwanda amezungumza na Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai wa Polisi Zanzibar Salum Msangi na kwanza alimuuliza hali ya usalama ikoje huko Pemba.

Baada ya kujitoa EU uingereza yapata pigo.



Image captionMuungano wa Ulaya

Uingereza imezuia kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Ulaya ambapo itakuwa mara ya kwanza kufanyiwa hivyo kwa miaka 40.
Waziri Mkuu, David Cameron, hatakuwa mezani wakati viongozi wengine 27 wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Ulaya watakuwa wakihudhuria mkutano usio rasmi juu ya hatma ya muungano huo baada ya kuondoka kwa Uingereza.
Uingereza imeambiwa ianzishe mpango wake wa kuondoka katika jumuiya hiyo bila kuchelewa.
Rais wa Jumuiya ya Ulaya, Jean-Claude Junker, amesema kuwa shughuli za kutegua kujiondoa kwa Uingereza kutoka muungano huo zinapaswa kutekelezwa mara tu Uingereza inapompata Waziri Mkuu mpya.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...