Monday, 4 May 2015

TEXAS WAUAWA WATU WAWILI KATKA TAMASHA LA UCHORAJI WA KATUNI NA VIBONZO VYA MTUME MUHAMMED.


POlisi mjini Texas wamewapiga risasi watu wawili kwa kuwashambulia polisi na risasi
Polisi mjini Texas wanasema kuwa wamewapiga risasi na kuwaua watu wawili waliokuwa na silaha, waliowashambulia walinda usalama kwa risasi, walipofika katika eneo la hafla moja yenye utata ya uchoraji wa vibonzo vya kuwakejeli waislamu na mtume Mohammed.
Duru za habari zasema kuwa kisa cha ushambuliaji wa risasi kimefanyika katika sherehe moja, iliyokuwa ikifanyika mjini Dallas, mahala ambapo waandalizi walikuwa wakiendesha onyesho hilo.
Hafla za Sherehe hiyo iliyoandaliwa na kundi moja la kisiasa la kihafidhina, ambalo limekuwa likikejeli Uislamu, lilikuwa litoe zawadi nono ya dola milioni kumi kwa mchoraji kibonzo mahiri zaidi, atakayeibuka mshindi kwa kumchora mtume Mohamed.
Polisi mjini Texas
Mwanasiasa kutoka Uholanzi Geert Wilders -- ambaye anafahamika kwa matamshi yake dhidi ya kuwadunisha waislamu, alikuwa msemaji mkuu katika hafla hiyo.
Aliyeshuhudia ameiambia BBC kuwa, aliwaona maafisa wa polisi wakimtia mbaroni mshukiwa wa tatu, ambaye alionekana kuwa hana silaha.
Kikosi cha kutegua mabomu pamoja na ndege za helikopta za polisi zimefika mahali hapo kwa sasa.

WATU WATATU WAUWAWA BURUNDI KATIKA MAANDAMO.


ni katika kile kinachosemekana kupinga kuendelea kuiongoza nchi hiyo rais wa sasa ambae inasemekana anataka kujiongezea muda wa kuiongoza inchi hiyo
Ghasia Burundi
Takriban watu wawili wameuawa wakati wa ghasia kati ya polisi na waandamanaji kwenye mji mkuu wa Burundi Bujumbura .
Polisi walifyatua risasi huku waandamanaji wakirusha mawe na guruneti.
Ghasia Burundi
Polisi wawili na waandamanaji sita nao walijeruhiwa.
Waandamanaji hao wanalalamikia hatua ya rais Pierre Nkurunziza ya kuwania urais kwa muhula wa tatu.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...