Sunday, 28 June 2015
Aliyejilipua Kuwait huyu hapa pichani, ni raia wa Saudi
Vyombo
vya habari nchini Kuwaiti zinasema kuwa mlipuaji wa kujitolea mhanga
aliyejilipua ndani ya msikiti nchini humo Ijumaa na kusababisha vifo vya
watu zaidi ya 25 ni raia wa Saudi Arabia.
Katika taarifa
iliyotolewa na wizara ya usalama wa ndani nchini Kuwait mshambuliaji
huyo anatambuliwa kuwa ni Fahd Suliman Abdul-Muhsen al-Qabaa.Yamkini taarifa hiyo inasema kuwa Fahd alikuwa ametua katika uwanja wa kimataifa wa ndege ulioko Kuwaiti saa chache kabla yake kutekeleza shambulizi hilo la kwanza kutokea nchini humo.
Kulingana na maafisa wa uhamiaji, Fahd alikuwa nchini humo kinyume cha sheria.
Kundi hilo linawakashifu waislmu washia kuwa wanakufuru na kukiuka maadili haswa na mafundisho ya mtume Muhammad.
Mashambulizi haya haswa kwa mataifa yanayochangia jeshi la muungano linalopigana na Wahouthi nchini Yemen na Islamic State nchini Syria na Iraq yamefikisha ujumbe wa ugaidi nyumbani kwa mataifa ya kanda hiyo ya ghuba kwa mujibu wa mwandishi wa BBC wa maswala ya Mashariki ya kati na ghuba Sebastian Usher.
Kuwait inaidadi kubwa ya washia katika kanda hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)
CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA
Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...

-
Tuzo za VMA 2014 zimefanyika na mastaa wengi walifika kwenye hilo tukio. Listi ya mastaa hao iliongozwa na familia ya Jay Z na Beyon...
-
Luca Modric mchezaji bora wa mwaka wa FIFA Wameamua kumpa,ni baada ya kumdhurumu tuzo yake ya msimu wa 2009/10,mwaka huu wameona ai...
-
Mlinda mlango wa Derby Country akipangua mkwaju wa Phil Jones Timu ya DERBY COUNTY inayonolewa na nyota wa zamani wa CHELSEA, FRANK LAM...