Tuesday, 8 December 2015
Kiongozi wa Al Shabaab auawa huko nchini Somalia kwa shambulio la ndege.
Kongozi mmoja wa kundi la Al Shabaab ameuawa katika shambulizi la ndege ya Marekani.
Msemaji wa makao makuu ya ulinzi ya Marekani ,Peter Cook , kifo cha Abdirahman Sandhere ni pigo kubwa kwa usimamizi na uwezo wa mashambulizi ya kundi hilo linalounga mkono wanamgambo wa Al Qaeda.
Sandhere, anayejulikana pia kama " Ukash'' anadaiwa kuuawa Jumatano iliyopita.
Al Shabaab inaendesha kampeini ya kuing'oa madarakani serikali inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa ilikilindwa na zaidi ya majeshi 22,000 wa umoja wa Afrika.
Kundi hilo limedhibitiwa katika maeneo mengi iliyokuwa ikikalia.
Hata hivyo kuwepo kwake na tishio la amani imedhihirika kupitia mashambulizi ya kigaidi mjini Mogadishu na vilevile katika taifa jirani la Kenya ambapo wapiganaji wake wametekeleza mashambulizi chungu nzima na kusababisha maafa makubwa.
Kwa mujibu wa duru za ujasusi za Marekani Al Shabaab inakabiliwa na changamoto kwa sababu ya ushawishi mkubwa wa Islamic State na Al Qaeda.
Marekani imekuwa ikitekeleza mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani kuanzia mwaka wa 2011.
donald Trump atakiwa kufuta kauli yake kuwa Waislamu wasiingie Marekani
- 8 Disemba 2015
Vigogo wa chama cha Republican nchini Marekani wamemkemea mwenzao Donald Trump, anayetaka kuwania urais kupitia chama hicho, kwa kupendekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani.
Mmoja wa wanaoshindani tiketi ya kuwania urais Jeb Bush amesema Bw Trump "mwenye kasoro akilini”. Makamu wa rais wa zamani Dick Cheney naye alisema pendekezo hilo "linaenda kinyume na yote ambayo huwa tunatetea”.
Ikulu ya White House, Umoja wa Mataifa na viongozi wa Kiislamu pia wamekosoa matamshi hayo ya Trump.
Bw Trump alikuwa amesema Waislamu wengi wana "chuki” dhidi ya Marekani.
Kwenye hotuba wakati wa kampeni, aliomba "Waislamu wote wazuiwe kuingia Marekani hadi wawakilishi wa nchi wajue ni nini kinachoendelea”
Meneja wake wa kampeni alisema marfuku hiyo ingeathiri "kila mmoja” bila kubagua kama ni mhamiaji au mtalii.
Lakini Bw Trump aliambia Fox News kwamba haingeathiri “watu wanaoishi humu nchini (Marekani), akiongeza kuwa Waislamu wanaohudumu katika jeshi la Marekani wangekaribishwa "nyumbani”.
- Mambo 20 makuu anayoamini Donald Trump
- Trump ashutumiwa kwa kupanga kufurusha wahamiaji
- Trump: Dunia ingekuwa bora na Gaddafi na Saddam
Matamshi hayo ya Bw Trump yalitolewa Marekani ikiendelea kuomboleza kufuatia shambulio mbaya zaidi la kigaidi kutekelezwa tangu shambulio la Septemba 11, 2001.
Wiki iliyopita, wanandoa wawili Waislamu, ambao wanaaminika kukumbatia itikadi kali, walifyatua risasi na kuwaua watu 14 na kuwajeruhi wengine 21 katika kituo cha afya San Bernardino, jimbo la California.
Bw Trump alishangiliwa sana aliporudia ahadi yake katika mkutano wa kampeni jimbo la South Carolina saa chache baada ya kutoa matamshi hayo mara ya kwanza.
Subscribe to:
Posts (Atom)
CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA
Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...

-
Tuzo za VMA 2014 zimefanyika na mastaa wengi walifika kwenye hilo tukio. Listi ya mastaa hao iliongozwa na familia ya Jay Z na Beyon...
-
Luca Modric mchezaji bora wa mwaka wa FIFA Wameamua kumpa,ni baada ya kumdhurumu tuzo yake ya msimu wa 2009/10,mwaka huu wameona ai...
-
Mlinda mlango wa Derby Country akipangua mkwaju wa Phil Jones Timu ya DERBY COUNTY inayonolewa na nyota wa zamani wa CHELSEA, FRANK LAM...