Ripoti kutoka
nchini Yemen zinasema kuwa muungano unaongozwa na Saudi Arabia umefanya
mashambulizi ya angani kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Sanaa, siku mbili
baada ya shambulizi la waasi lililowaua wanajeshi 60.
Walioshuhudia
walisema kuwa mashambulia hayo yalilenga ngome za waasi wa Houthi na
vikosi vilivyo watiifuu kwa rais wa zamani Ali Abdullah Saleh.Ripoti zingine kutoka hospitali za mji wa Sanaa zilisema kuwa zaidi ya raia 20 wameuawa kwenye mashambulizi hayo.