Thursday, 5 May 2016

soma hii.Wapenzi wa Jinsia moja wapinga ukaguzi wa nyama zao.

'


Image captionwapenzi wa jinsia moja
Wanaume wawili wanaosema kuwa maafisa wa polisi wa Kenya waliwalazimisha kufanyiwa ukaguzi wa tupu ya nyuma ili kubaini kwamba walishiriki katika ngono ya mapenzi ya jinsia moja wameanzisha kesi mahakamani wakitaka ukaguzi huo kuwa ukiukaji wa katiba.
Wanasema kuwa walilazimishwa kufanyiwa ukaguzi wa magonjwa ya virusi vya ukimwi na Hepatitis kufuatia kukamatwa kwao mnamo mwezi Februari 2015 baada ya kushukiwa kwamba wanashiriki katika ngono ya mapenzi ya jinsia moja.
Vitendo vya wapenzi wa jinsia moja kushiriki ngono ni kinyume na sheria nchini Kenya na adhabu ya makosa hayo ni miaka 14 jela.
Mahakama ya Mombasa imewapatia mawakili wa serikali wiki moja kutoa jibu.
Chini ya sheria ya kimataifa ,ukaguzi wa lazima katika tupu ya nyuma ni kitendo cha kikatili,unyama na ni sawa na mateso kulingana na kundi la haki za kibinaadamu Human Wrights Watch

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...