Tuesday, 28 April 2015

Indonesia yawanyonga wauza mihadarati. pitia hii ni muhimu


Wafanyabiashara wa mihadarati walipokuwa wakipelekwa kunyongwa
Indonesia imewaua wauzaji wanane wa mihadarati baada ya kutoa hukumu ya kifo dhidi yao.
Hukumu hiyo imetekelezwa na kikosi maalum cha kuwapiga wafungwa risasi, licha ya mwito kutoka kwa mataifa ya dunia ya kuwahurumia watu hao.
Kuuwawa kwa mfungwa wa tisa, raia wa Ufilipino, Mary Jane Veloso, kumecheleweshwa baada ya mwanamke mmoja kujiwasilisha kwa polisi Nchini Ufilipino, akisema kuwa ndiye aliyemhadaa mfungwa huyo mwanamke mwenzake, kupeleka dawa za kulevya hadi Indonesia.

Babaake Kim Kardashian sasa ni mwanamke.soma haya maajabu.



Bruce Jenner
Bruce Jenner aliyekuwa mwariadha bora duaniani kabla ya kuwa nyota wa kipindi cha televisheni na familia moja maarufu duniani ''The Kardashians''. sasa amefichua siri ambayo amekuwa akiificha kwa miaka mingi.
''Kwa nia na madhumuni yote, mimi ni mwanamke.'' Jenner aliambia Sawyer kutoka ABC katika mahojiano maalum yaliopeperushwa hewani siku ya Ijumaa.
''Watu wananiona tofauti,wananiona kama mwanaume, lakini moyo na roho yangu na kila kitu ninachofanya maishani ni sehemu yangu.'' Jenner ambaye ana umri wa miaka 65 amesema. '' Upande huu wa kike ni sehemu yangu.
hivi ndivyo mimi nilivyo.''
Bruce Jenner
Katika masaa ya mahojiano na Diane Sawyer mjini New York na California, Jenner alielezea kwa kina mapambano yake ya kuwa na jinsia mbili tangu utotoni.
''Akili zangu ni za kike sana kuliko za kiume.'' Ameongezea. '' Ni vigumu sana watu kuelewa, lakini hivyo ndivyo nafsi yangu ilivyo.''
Jenner aliyejawa na hisia na mwenye nywele ndefu shati na suruali ndefu alisema kuwa amesubiri kwa miaka mingi ili kujitangaza kwa kuwa hakutaka kuwavunja moyo watu.
Kwa miongo kadhaa wake wa zamani wa Jenner na madada zake waliweka siri kuhusu jinsia yake na kwamba walikuwa watu waliokuwa wakijua siri hiyo.
Mtandao wa watu wanaojua siri hiyo hatahivyo ulipanuka hivi majuzi wakati Jenner alipomwambia mamaake na wanawe 10 .
Jenner ana watoto sita Burt,Cassandra,Brabdon,Brody,Kendall na Kylie pamoja na watoto wanne wa kambo akiwemo Kourtney,Kim,Khloe na Rob Kardashian.

mwendelezo wa NEPALI.....serikali ya nepali yakiri kuelemewa..msaada wahitajika.



Watu waliopoteza makwao Indonesia

Serikali ya Nepal inasema kuwa imelemewa na kiwango cha janga lililosababishwa na tetemeko la ardhi siku ya Jumamosi.
Waziri mkuu Sushil Koirala anasema kuwa utawala unapokea maombi mengi ya kutaka msaada kutoka maeneo ya mbali ya vijiji vya Himalaya, lakini jitihada za kuyafikia maeneo hayo zinatatizwa na uhaba wa vifaa na waokoaji.
Waziri huyo mkuu anasema kuwa kuna mahitaji ya dharura ya mahema , chakula na maji. Mwandishi wa BBC aliye kwenye kijiji kuliko kitovu cha tetemeko hilo, anasema kuwa zaidi ya nusu ya nyumba katika kijiji hicho zimeharibiwa.
Zaidi ya watu 4000 wanathibitishwa kuaga dunia lakini waziri mkuu anasema kuwa huenda idadi hiyo ikaongezeka

mabingwa wa ligi kuu ya tanzania hawa hapa.jionee hapa


Mashabiki wa Yanga wakifurahia ushindi
Klabu ya Yanga nchini Tanzania imekata mzizi wa fitina baada ya kunyakua ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa mwaka 2014/2015. Ushindi ulioupata wa magoli 4-1 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ndio ulihitimisha safari ya Yanga na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la klabu bingwa barani Afrika.
Kwa sasa Yanga, ambao wamewavua Azam ubingwa huo, ni wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya CAF, wakiwa na kazi ya kuitoa Etoile du Sahel mapema mwezi ujao katika hatua ya 16 ya kombe la Shirikisho.
“Nimefurahishwa na kushinda taji la ligi kuu Tanzania, wachezaji wamejituma na wamefanikiwa”, amesema kocha mkuu wa Yanga, Hans Pluijm.
Amisi Tambwe kutoka Burundi, ambaye ndiye mfungaji bora wa msimu uliopita akiwa mchezaji wa Simba, alifunga hat-trick (magoli matatu) dhidi ya Polisi Morogoro huku Simon Msuva akitupia moja.


Sherehe za kutwaa ubingwa huo ziliendelea hadi nje ya mitaa kadhaa ya Dar es Salaam kutokana na furaha ya mashabiki. Hata hivyo, Yanga haikukabidhiwa kombe kutokana na kuendelea kwa ligi.

Waganga mbali mbali wajitolea kumtibu Wema Sepetu aweze kupata mtoto.
















Wema Sepetu

Waganga wa kienyeji wanaotoka katika maeneo tofauti nchini Tanzania wamejitolea kumtibu Msanii WemaSepetu aweze kupata mtoto.
Kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya Waganga hao waliojitolea walipiga simu kwa mtandao wa Bongo Movies.com baada ya kukiri kwa nyota huyo wa filamu kwamba hawezi kupata mtoto.
Wameapa kumtibu tatizo hilo.''Wajua kuna wanawake wanaopata matatizo madogo kama kutoweza kupata mtoto licha ya kwamba kuna matabibu wanaoweza kutatua matatizo yao.

Tatizo la wema sio la kumtia wasiwasi,linaweza kutibika''walisema.
Mpatie nambari yangu ya simu na umwambie anipigiemmoja wa waganga hao alisema.
Na ili kutaka kujua vile Wema alijibu ombi hilo ,inadaiwa kuwa alikubali kusaidiwa na watabibu hao lakini kwa masharti.

Image result for wema sepetu
''Kuna wengi zaidi mbali na waganga ambao wamejitolea kunisaidia.nina zaidi ya ujumbe 400 niliyotumiwa katika mtandao wangu wa WhatsApp huku simu nyingi zikipigwa.Ukweli ni kwamba niko tayari kupokea usaidizi huo.'',alijibu.

Je,miraa inaongeza nguvu za kiume? soma upate jibu kutoka kwa mtaalamu wa kimataifa



Mtu anayekula miraa kenya
Wanaume katika eneo la Meru mashariki mwa Kenya ambao hawana uwezo wa kuwatosheleza wake zao kupitia tendo la ngono sasa wametakiwa kutokuwa na wasiwasi.
Mwakilishi wa wanawake katika eneo hilo Florence kajuju ameanza mpango wa kuwahamasisha wanaume kutumia miraa badala ya ya pombe haramu .
Akizungumza na gazeti la The Nairobian nchini Kenya,kiongozi huyo amesema kuwa pombe haramu hushusha nguvu za kiume na kuwafanya wanaume kushindwa kuwatosheleza wake zao.
''Ni pombe kama hizi ambazo huathiri nguvu za kiume na kusababisha utasa miongoni mwa wanaume'',alisema.
Kajuju ambaye anasema anapenda miraa aliudhika alipogundua kwamba eneo la Meru ni miongoni mwa maeneo ambayo wanaume hawana uwezo wa kutafuta watoto.
''Vijana wetu wameathirika vibaya na pombe haramu na lazima tuwaokoe''.
Alisema kuwa wale waliopiga marufuku uuzaji wa miraa katika mataifa yao wanafaa kugundua umuhimu wa zao hilo miongoni mwa jamii.

Maandamano ya wananchi wa burundi:Jeshi lasambazwa nchi nzima .



Wanajeshi
Jeshi la Burundi limetawanywa nchini humo kujaribu kukabiliana na wale wanaopinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania muhula wa tatu.
Polisi walivunja maandamano ya Wanaharakati na wapinzani nchini humo waliongia mitaani kwa siku ya pili kufanya maandamano.
Waandamanaji kadha walipigwa risasi jana Jumapili na watu wanne wanaripotiwa kufariki

zaidi ya watu 4000 wathibitishwa kufa nepal kwa tetemeko. soma na jionee hapa

Woman in a tent in Kathmandu, Nepal (27 April 2015)Dharahara tower via satellite before and after the quake


map of Nepal showing areas affected by earthquake


Nyumba zilizoharibiwa Nepal

Utawala nchini Nepal unasema kuwa watu zaidi ya watu 4000 wamedhibitishwa kuaga dunia huku wengine 8000 wakijeruhiwa kwenye janga la tetemeko la ardhi lililosababisha uharibifu mkubwa siku ya Jumamosi.
Jitihada za uokoaji zinaendelea kukiwa na matumaini ya kuwapata manusura, lakini jitihada hizo bado hazijayafikia maeneo mengine yaliyo mbali.
Watu wengi walilala nje kwa usiku wa tatu mfululizo kwenye mji mkuu Kathmandu wakihofia kutokea kwa mitetemeo mingine midogo.
Serikali ya Nepal inasema kuwa inahitaji kila msaada ukiwemo wa mablanketi , helkopta, madaktari na madereva. Kuna uhaba wa maji , chakula na umeme huku ku

Vurugu zazuka mji wa Baltmore nchini Marekani . jionee hapa



vurugu Baltimore
Vurugu kubwa za mapigano baina ya polisi na waandamanaji zimetokea nchini Marekani katika mji wa Boltimore, baada ya maziko ya kijana Freddie Gray ambaye alikufa kutokana kujeruhiwa alipokuwa mikononi mwa polisi mapema mwezi huu.
Hali ya hatari na kutotembea hovyo imetangazwa katika mji huo kufuatia vurugu hizo.
Kifo cha Freddie Gray ambaye ni kijana mweusi mmarekani mwenya asili ya kiafrika kimesababisha maswali mengi kuhusu matumizi ya nguvu za ziada ya polisi dhidi ya raia wa marekani wenye asili ya kiafrika.
Hata hiyo Msemaji wa polisi wa Baltimore Captain Eric Kowalczyk amesema vurugu hizo pia zimesababisha maafisa wake kujeruhiwa na wengine wapo katika hali mbaya.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...