Sepp Blatter ameutingisha ulimwengu wa soka hapo jana kwa
kusema kwamba anajiuzulu akiwa kama Rais wa Shirikisho la Sola la
Kimataifa FIFA kutokana na uchunguzi wa rushwa ambao hivi sasa
unamjumuisha hata kiongozi huyo mwenyewe binafsi mwenye umri wa miaka
79. Mtu aliezungumza kwa sharti la kutotajwa jina ameliambia shirika la
habari la Uingereza Reuters hapo jana kwamba Blatter ambaye ameliongoza
shirika hilo linalosimamia soka duniani tokea mwaka 1998 anachunguzwa na
waendesha mashtaka wa Marekani na shirika la upepelezi nchini humo FBI.
Msemaji wa FBI amekataa kulizungumzia suala hilo.Blatter raia wa Uswisi
ambaye alikuwa ni mtu mwenye ushawishi mkubwa kwenye FIFA kwa miongo
mingi ametangaza uamuzi wake wa kujiuzulu katika mkutano na waandishi wa
habari ulioitishwa kwa haraka mjini Zurich hapo jana ikiwa ni siku sita
baada ya polisi kuivamia hoteli moja mjini humo na kuwakamata maafisa
kadhaa wa FIFA na ni siku nne baada ya kuchaguliwa tena kwa muhula wa
tano akiwa rais wa FIFA. Amesema uchaguzi wa rais mpya wa FIFA
utafanyika karibuni kadri inayowezekana lakini afisa mmoja wa FIFA
amesema iwapo uchaguzi huo utafanyika mapema basi itakuwa mwezi wa
Disemba.
Maafisa wa mjini Delhi huko India wamepiga marufuku chakula aina ya
tambi ziitwazo ''Maggi noodles'' baada ya kufanyiwa uchunguzi na
kugunduliwa kuwa na kiwango kikubwa cha madini hatari aina ya lead.
Tambi
hizo za ''Maggi noodles'', ambazo zinatengenezwa na kampuni maarufu ya
Nestle ya huko India zilikuwa zikipendwa sana na kununuliwa kwa wingi na
walaji wengi .
Kampuni yenyewe imejitetea kuwa vyakula vyao ni salama.
Lakini kufuatia tukio hilo la kupigwa marufuku kwa ''Maggi noodles'' hisa zao zimeporomoka katika soko lao la huko India .
hii inasababishwa na uwindaji haramu unaofanywa na baadhi ya watanzania , tunaomba ujangili huu ukomeshwe haraka sana kwa ajili ya kuzidi kuhifadhi mali asili ya nchi ambayo ni manufaa kwa kizazi kijacho kama tulivyoikuta sisi baada ya ulindwaji mzuri wa wazee wetu waliotutangulia.
Wanaharakati
wa wanyamapori wameelezea hali ya kutoweka kwa idadi ya ndovu kwa
asilimia sitini nchini Tanzania katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita kama janga.
Kundi linalofuatilia maisha ya wanyamapori, TRAFFIC, linasema idadi hiyo inaashiria kiwango halisi cha uwindaji haramu.
Waziri
katika serikali ya Tanzania Lazaro Nyalandu, amesema kuwa tatizo hilo
lipo kwa kiwango tofauti nchini humo, akitoa mfano kuwa eneo la
Serengeti idadi yao inaongezeka .
Wanaharakati
wa wanyamapori wameelezea hali ya kutoweka kwa idadi ya ndovu kwa
asilimia sitini nchini Tanzania katika kipindi cha miaka mitano
iliyopita kama janga.
Kundi linalofuatilia maisha ya wanyamapori, TRAFFIC, linasema idadi hiyo inaashiria kiwango halisi cha uwindaji haramu.
Waziri
katika serikali ya Tanzania Lazaro Nyalandu, amesema kuwa tatizo hilo
lipo kwa kiwango tofauti nchini humo, akitoa mfano kuwa eneo la
Serengeti idadi yao inaongezeka .