Monday, 18 July 2016

Mtu Mweusi awaua Polisi 3 Marekani

Mweusi awaua Polisi 3 Marekani

Rais Barrack Obama wa Marekani amewasihi wamerakani wajizue dhidi ya hisia kali baada ya Mmarekani Mweusi kuwapiga risasi na kuwaua maafisa watatu wa polisi katika shambulizi la pili la kulipiza kisasi dhidi ya polisi wazungu wanaowaua wamarekani weusi.
Obama ameomba uvumilivu utawale mioyo ya wakaazi wa mji wa Baton Rouge Louisiana nchini Marekani ambao sasa wanahofu ya kuzuka mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Image copyright Reuters
Image caption Gavin Long ambaye ni mwanajeshi wa zamani aliwapiga risasi polisi kulipiza kisasi mauaji ya Alton Sterling
Obama aliyasema hayo katika hotuba ya moja kwa moja kupitia kwa runinga kutoka ikulu ya WhiteHouse muda mchache tu baada ya mtu mmoja mweusi kuua maafisa watatu wa polisi hukohuko Baton Rouge alikouawa mtu mweusi
Alton Sterling pasi na hatia yeyote majuma mawili yaliyopita.

Image copyright Facebook
Image caption Alton Sterling aliyeuawa na polisi mzungu pasi na kosa lolote
Hasira imekuwa ikitokota miongoni mwa watu weusi baada ya mtindo wa kuuawa kwa wanaume weusi na polisi wazungu kuendelea kwa muda mrefu ilihali hakuna hatua inayochukuliwa dhidi yao.
Gavin Long ambaye ni mwanajeshi wa zamani alikuwa amerekodi ujumbe katika mji wa Dallas siku chache baada ya polisi watano kuuawa mjini humo katika shambulizi lililotekelezwa kulipiza kisasi cha mauaji ya Sterling.

Image copyright Reuters
Image caption Hasira imekuwa ikitokota miongoni mwa watu weusi baada ya mtindo wa kuuawa kwa wanaume weusi na polisi wazungu kuendelea kwa muda mrefu
Sasa imebainika kuwa Long alikuwa ameweka video kwenye mtandao akilalamika jinsi polisi wanavyowatendea waamerika weusi ambapo alitoa wito kwa wanaume weusi kujitolea kuokoa jamii yao.
Long mwenye umri wa miaka 29 aliwahi kuhudumu kama mwanajeshi wa Marekani .
Rais Obama ameshauri watu weusi dhidi ya kutekeleza mashambulizi dhidi ya Polisi akisema mauaji ya kulipiza kisasi sio suluhisho la tatizo sugu la ubaguzi wa rangi bali utachochea uhasama zaidi dhidi yao na polisoi wazungu.

Abakwa na watu 5 kwa mara ya pili India



Image copyrightREUTERS
Image captionBinti huyo mwenye umri wa miaka 21 amebakwa na wanaume watano kwa mara ya pili.
Kwa mtazamo wa wengi radi haiwezi kupiga mti mmoja mara mbili.,,, lakini kwa mwanamke mmoja nchini India hilo ndilo lililomkuta.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 21 amebakwa na wanaume watano kwa mara ya pili.
Image copyrightREUTERS
Image captionMiaka mitatu iliyopita binti huyo alibakwa na wanaume wao hao watano katika mji wa Bhiwani.
Miaka mitatu iliyopita binti huyo alibakwa na wanaume wao hao watano katika mji wa Bhiwani.
Sadfa ni kwamba binti huyo aliyetorokea mji tofauti wa Rohtak ulioko katika jimbo la Kaskazini la Haryana alishikwa na kubakwa tena juma lililopita.
Alikuwa akitembea barabarani kisha akatekwa nyara na watu ambao nusura wamnyonge.
Alinusurika kufa lakini alichokipitia ni cha kutamausha sana.
Image copyrightREUTERS
Image captionBinti huyo alibakwa kwa mara ya pili na kutupwa kichakani.
Binti huyo alibakwa na kutupwa kichakani.
Kwa bahati nzuri msamaria mwema aliyekuwa akipita eneo hilo alimsikia akitoa sauti hafifu na kumpeleka hospitalini alikotibiwa hadi akarejesha afya yake.
Alipopata afueni alisema maneno yaliyoibua hasira miongoni mwa jamii.
Image captionBinti huyo alibakwa na kutupwa kichakani.
''Nilikuwa nikitembea barabarani nikitoka chuoni kuelekea nyumbani kisha nikawaona walewale wanaume walionibaka huko Rohtak.
Nilishtuka na kuhofia maisha yangu. Walishika na kujaribu kuninyonga.walinieleza kuwa watawaua babangu na kakangu.''
Image captionMamia ya wenyeji wa mji wa Rohtak, wameandamana wakitaka serikali iwachukulie hatua kali washukiwa hao wa kosa hilo la kinyama.
Sijui walikonipeleka kwa sababu nilipoteza fahamu ila ninachokijua ni kuwa walikuwa wale wale walionibaka miaka mitatu iliyopita.'' binti huyo kutoka jamii maskini aliiambia runinga moja ya kitaifa nchini India.
Familia yake inasema kuwa washukiwa hao walikuwa wakiwashinikiza kukomesha mashtaka dhidi yao lakini binti yao akakataa kata kata.
Sasa polisi wametumwa huko kuwasaka watuhumiwa hao.
Mamia ya wenyeji wa mji wa Rohtak, wameandamana wakitaka serikali iwachukulie hatua kali washukiwa hao wa kosa hilo la kinyama.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...