Wednesday, 13 January 2016

hivi punde zaidi ya watu 14 wauawa huko Pakistani kwa shambulio la bomu.tazama na soma hii


Polisi pakistanImage copyrightAFP
Image captionPolisi katika mji wa Quetta nchini Pakistani baada ya mlipuko wa bomu kwenye eneo la tukio
Takriban watu 14 wameuawa katika shambulio la bomu nje ya kituo cha kutoa chanjo ya ugonjwa wa kupooza(polio) katika mji wa kusini magharibi wa Quetta nchini Pakistani, kwa mujibu wa maafisa.
Wengi miongoni mwa waliouawa wanadhaniwa kuwa ni polisi waliokuwa wakilinda kliniki.
Mlipuko wa Bomu QuettaImage copyrightGetty
Image captionWanamgambo wa Islamic State wamekua wanasema chanjo za kupooza zinazuia uzazi nchini pakistani
Polisi wenye silaha huwalinda wahudumu wa afya wanaotoa chanjo ya kupooza nchini Pakistani ambao wamekua wakilengwa na mashambulio mabaya ya Islamic State miaka ya hivi karibuni.
Wanamgambo wa Islamic State wanapinga chanjo ya kupooza , wakisema ni mpango wa nchi za magharibi wa kufunga uzazi dhidi ya watoto wa Pakistani.
Pakistan quettaImage copyrightAP
Image captionPakistan na Afghanstan ndio nchi pekee zenye maambukizi mengi ya maradhi ya kupooza zaidi duniani
Pakistan na Afghanistan ni nchi pekee zilizosalia zenye visa vingi vya marathi ya kupooza.
Mlipuko wa bomu hilo ulitokea mapema subuhi wakati wahudumu wa kutoa chanjo na maafisa wa usalama walipokua wakiripoti kazini kabla ya kuelekea nje kwa mizunguko ya kutoa chanjo hiyo , amesema Sarfaraz Bugti, waziri katika jimbo la Balochistan ambalo Quetta ni mji mkuu wake.
Polisi katika eneo hilo wanasema kuwa mlipuko huo uliwauwa polisi 12, mwanajeshi mmoja na raia mmoja. Watu wapao 20 wamejeruhiwa.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...