Wednesday, 22 July 2015
huyu hapa dada mjamzito anaefungiwa ndani ya geti kila siku , mimba ya miez sita sasa
Hekaheka ya leo inatokea maeneo ya Mbezi ambapo dada mmoja wa kazi za nyumbani amekuwa akifungiwa ndani ya geti lililofungwa kwa nje huku bosi wake akiwa kazini wakati ni mjamzito wa miezi sita.
Dada huyo ambaye anatokea Sumbawanga amesema amekuwa akifungiwa ndani kila siku kwa mwezi mmoja na kutakiwa kulinda nyumba wakati wa usiku.. kingine alicholalamika ni kwamba japo ana ujauzito lakini bosi wake hajamruhusu kwenda kliniki na wala hajawahi kulipwa mshahara wake.
Jirani amesema wamekuwa wakimsikia msichana huyo akiwa kila siku analia na kuamua kumuhoji ndipo walipogundua hufungiwa nje ya nyumba na bosi wake, wanadai ananyanayasika na anatia huruma kwa hali aliyonayo.
Bosi wake amesema si kweli anamlaza nje..alikuja kwake na kumkuta msichana mwingine na kukubaliana watakua wote.
Subscribe to:
Posts (Atom)
CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA
Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...
-
Image caption Uganda haipaswi kuzuia upinzani, Obasanjo Aliyekuwa rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, ametaka pande zote pinza...
-
Tuzo za VMA 2014 zimefanyika na mastaa wengi walifika kwenye hilo tukio. Listi ya mastaa hao iliongozwa na familia ya Jay Z na Beyon...