Wednesday, 8 April 2015

FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRICA 2017 ZITAFANYIKA NCHI GANI? JIBU HILI HAPA


Gabon imezipiku Algeria na Ghana kuwa mwenyeji wa fainali za Afcon za mwaka 2017
Gabon ndiye mwenyeji wa kombe la mataifa ya Afrika yatakayoandaliwa mwaka wa 2017.
Gabon imeahidi kutumia viwanja 4 katika mashindano hayo yenye timu 16 kati ya mwezi Januari na Februari.
Viwanja hivyo vitakuwa Libreville Franceville, vilivyotumika mwaka wa 2012,huku Port Gentil na Oyem
zikitarajiwa kukamilishwa katika kipindi cha miezi 14 ijayo kwa mujibu wa onyesho la shirikisho la soka la Gabon.
Gabon, inayopewa nafasi ya kushinda kinyang'anyiro hicho, iliandaa kwa pamoja na majirani zao Equatorial Guinea, fainali za mwaka 2012
Wenyeji wa awali wa fainali hizo, Libya, ambako vita vya wenyewe kwa wenyewe vimekwamisha shughuli za mpira, ilijitoa mwaka jana kuandaa mashindano hayo.
Kamati ya shirikisho la vyama vya soka barani Afrika, Caf, itaendesha uteuzi huo katika mkutano wake wa mwaka utakaofanyika mjini Cairo,
Misri kuamua nani atakuwa mwenyeji wa fainali hizo.
Timu ya Gabon
Ghana iliandaa imewahi kuandaa fainali za mwaka 1963, 1978 na 2008 na iliandaa kwa pamoja na Nigeria fainali za
mwaka 2000 kama waandaji mbadala wakati Zimbabwe iliponyang'anywa haki ya kuandaa fainali hizo.
Algeria iliandaa fainali za mwaka 1990 wakati waliposhinda taji hilo pekee barani Afrika.
Caf pia inatarajiwa kupanga ratiba ya kufuzu kwa fainali hizo, ambayo itazishirikisha pia nchi za Morocco na Tunisia.
Morocco ilifungiwa kushiriki katika fainali mbili mfululizo za shirikisho la Caf baada ya kushindwa kuandaa fainali za mwaka 2015
lakini walishinda kesi hiyo baada ya kukata rufaa katika mahakama ya michezo, CAS.
Tunisia imeondolewa adhabu ya kutoshiriki michuano ya shirikisho hilo baada ya kuomba radhi kwa kulishutumu shirikisho hilo kwa upendeleo.

Wanamitindo wembamba wapigwa marufuku kabisa.ni hatari tazama hapa



Wanamitindo
Bunge la Ufaransa limeidhinisha sheria inayopiga marufuku tabia ya makampuni ya wanamitindo nchini humo kutumia wasichana waonesha mitindo walio wembamba kupita kiasi.
Sasa itabidi wanamitindo wembamba kuonyesha kuwa wanauzito wa viwango vinavyokubaliwa kiafya.
Mawakala wa wanamitindo watakaokiuka viwango vilivyowekwa watapigwa faini huku wakuu wa makampuni husika nao huenda wakakabiliwa na vifungo vya hadi miezi 6.
Pia sheria imepitishwa inayopendekeza hatua kuchukuliwa dhidi ya mitandao inayopendelea kuonyesha picha za wasichana walio wembamba kiasi cha kudhoofisha kiafya.

Facebook kufungua huduma mpya ya messenger .soma hii.

28 Machi 2015 Imebadilishwa mwisho saa 10:27 GMT
Mtandao wa facebook umethibitisha kwamba unafungua huduma yake ya messenger kwa wajenzi .Habari hizo zilitangazwa na Mark Zuckerberg katika kongamano la nane la wajenzi lililofanyika mjini San Fransisco.Zaidi ya programmu 40 mpya zikiwemo habari za hali ya anga tayari zimeandaliwa kwa huduma hiyo.Mtandao huo wa kijamii pia ulionyesha programu yake ya video inayomruhusu mtumiaji kusukuma kamera huku kanda hiyo ikicheza.

BAADA YA KUVUNJIKA KWA PENZI LA NEY WA MITEGO HUYU NDIYE ANAEDAIWA KUIVUNJA..INASEMEKANA KUTOKANA NA HAYA HAYA HAPA .JIONEE



Nay 2
Majibu ya Nay wa Mitego kuhusu hii picha ni kwamba ni movie ndio inachezwa ambapo kama kweli ni movie basi hii ndio itakua movie ya kwanza sisi tulio wengi kumuona Nay wa Mitego.
nay 4Wawili hawa wametajwa kuwepo mapenzini kwa kiasi kikubwa siku za karibuni ambapo Shamsa ambaye aliingia kwenye headlines za Magazeti baada ya kuachana na mume wake, amepost picha mbili ndani ya siku tano zilizopita akiwa kwenye Gym ya Nay wa Mitego.
nay 3Kwenye hii picha ya juu hakuandika chochote kama caption ila hii picha ya chini mrembo huyu aliandika >>> ‘On Set‘ yaani ni kwenye utengenezaji wa movie.nay 4

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...