Monday, 28 March 2016

hivi punde Milio ya risasi jengo la Bunge Marekani, tazama na soma hii


 

 Image copyright d Image caption Jengo la Bunge la Marekani Capitol Hill

Kuna taarifa za milio ya risasi katika viunga vya jengo la Makao Makuu ya Bunge la Congress, US Capitol Hill.
Mashuhuda wanasema wameambiwa kwa vipaza sauti kuwa kila mtu ajifiche.
Taarifa za hivi punde zinasema mtu huyo mwenye silaha amekamatwa na polisi mmoja amepigwa risasi na kujeruhiwa.
Waandishi wa Habari waliokuwa kwenye eneo jengo la Bunge wameambiwa waendelea kubaki ndani.
Ikulu ya White House nayo imefungwa. Msemaji wa Polisi katika Jengo la Bunge hajasema lolote lakini ameahidi polisi kutoa taarifa za tukio hilo wakati wowote.

kichupa kipya cha bidada yemi alade hiki hapa, download Yemi Alade - Ferrari (Official Video) .

Brussels; Watu wanne waliojeruhiwa wafariki huko ubeljiji.






Watu wanne waliojeruhiwa wakati wa mashambulio ya Brussels wiki iliyopita wamefariki na kufikisha idadi ya waliofariki hadi 35, maafisa nchini humo wamesema.

Hayo yamejiri huku waendesha mashtaka nchini Ubelgiji wakisema watu watatu wameshtakiwa kwa tuhuma za kuwa wanachama wa kundi la kigaidi.
Uchunguzi bado unaendelea kuhusu mashambulio hayo yaliyotekelezwa Jumanne.
Washukiwa hao watatu, Yassine A, Mohamed B na Aboubaker O, walikamatwa wakati wa msako wa maafisa wa usalama Brussels na Antwerp.
Serikali ya Ubelgiji imesema bado ni mapema kujua iwapo uwanja wa ndege wa Zaventem, ulioshambuliwa Jumanne, utafunguliwa tena.

Maafisa wa serikali wamesema wafanyakazi 800 watafanyia majaribio kituo cha muda cha kuhudumia wateja ambacho kimejengwa siku ya Jumanne.
Kwingineko, polisi wa Uholanzi walitangaza Jumapili jioni kwamba walikuwa wamemzuiliwa mwanamume raia wa Ufaransa mjini Rotterdam kufuatia ombi la Ufaransa.
Mwanamume huyo wa umri wa miaka 32 alikamatwa akishukiwa kupanga shambulio Ufaransa na atapelekwa Ufaransa.
Mfaransa huyo anadaiwa kuwa na uhusiano na Reda Kriket, aliyekamatwa Paris mnamo Alhamisi na ambaye maafisa walisema alikuwa katika hatua za mwisho mwisho za kupanga shambulio la kigaidi.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...