Friday, 8 April 2016
Njaa: watu wafa njaa mjini Fallujah.
Shirika la kutetea
haki za binaadamu la Human Rights Watch limeeleza kuwa wakaazi wa mji
unaokabiliana na mji mkuu wa Iraq wamezingirwa katika mji wa Fallujah na
wanakufa kwa njaa kali.
Nayo majeshi ya serikali yamesitisha
shughuli ya usambazaji wa chakula katika eneo hilo, eneo ambalo
wanajaribu kulikomboa kutoka katika ngome vikosi vya kundi la kigaidi la
Islamic State.Kundi moja la wanaharakati waishio mjini New York nchini Marekani wanaofanya kazi ya kusambaza misaada ya kibinaadamu wanasema kwamba ni kiasi kidogo mno cha chakula na huduma nyinginezo kilichosalia katika eneo hilo na ili kuokoa uhai watu walioko eneo hilo wanaishi kwa kunywa supu ya majani .
Kuna taarifa pia ambazo hazijathibitishwa juu ya vifo vingi vinavyotokea kutokana na uhaba wa chakula na dawa.
mpya kuhusu talaka ya ndoa kwa wakatoliki,Papa Francis kutoa tamko jingine muhimu
Kiongozi wa kanisa
Katoliki duniani Papa Francis leo anatarajiwa kutangaza wazi msimamo
wake kuhusu ndoa, njia za kupanga uzazi na malezi ya watoto.
Tangazo
hilo linatarajiwa kuwa kwenye ripoti ya mikutano miwili mikuu ya kutoa
maamuzi kuhusu sera za kanisa hilo, maarufu kama sinodi.Wengi wanatumai kwamba ripoti hiyo itafungua njia kwa kanisa hilo kutoa sakramenti ya komunyo kwa watu waliopewa talaka na wale waliooa tena, jambo ambalo wahafidhina katika kanisa hilo wamekuwa wakipinga.
Ripoti hiyo ni matokeo ya kazi aliyoifanya Papa huyo kwa miaka mitatu.
Mwandishi wa BBC anayeangazia masuala ya kidini Caroline Wyatt anasema ripoti hiyo ambayo kwa Kiingereza hujulikana kama Apostolic Exhortation (Ujumbe wa Papa kwa Waumini) ni nyaraka yenye zaidi ya kurasa 200.
Ripoti hiyo ya sasa imepewa kichwa The Joy of Love (Furaha ya Upendo).
Baadaye, aliwaita maaskofu na makadinali kwa mikutano miwili ya sera za kanisa mjini Roma.
Kwenye mkutano huo, aliwahimiza kujadiliana na hata kutofautiana kuhusu masuala ambayo hugawanya waumini wa kanisa hilo katika nchi nyingi.
Masuala hayo ni pamoja na kutoa komunyo kwa watu waliopewa talaka na wale walioolewa tena, njia za kupanga uzazi na pia Wakatoliki ambao ni wapenzi wa jinsia moja.
Mwandishi wetu anasema ripoti hiyo itaonyesha wazi msimamo wa Papa Francis.
Baadhi tayari wanasema itashangaza wengi, huku Papa akijitosa katika bahari ya mafundisho ya kanisa Katoliki kuhusu familia.
Wahafidhina hawamtaki abadilishe imani na msimamo wa kanisa, lakini watu wenye msimamo huru wanatumai kwamba ataliambia kanisa liwe na huruma na kuwakumbatia wale watu walio kwenye familia wasiokumbatia kikamilifu mafundisho ya kanisa.
- Baba Mtakatifu aosha miguu ya waislamu
- Papa: Uoga utawafanya Wakristo wafungwa
- Papa Francis aingia Instagram
Wakati wa kumalizika kwa sinodi ya mwaka jana, Papa Francis aliwakosoa viongozi wa kanisa aliosema wamelifumbia macho suala hilo na kusema kwamba kuendelea kusisitiza kuheshimiwa kwa mafundisho ya dini kikamilifu ni kukosa kutilia maanani dhiki wanayopitia watu wengine katika familia.
Nyaraka hiyo ya papa inatarajiwa kutoa wito wa kuwepo kwa maandalizi mema zaidi kabla ya ndoa na pia kusisitiza mtazamo wa sinodi kwamba ndoa za wapenzi wa jinsia moja haziwezi zikawekwa kwenye kiwango sawa na ndoa za watu wa jinsia tofauti.
Subscribe to:
Posts (Atom)
CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA
Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...

-
Tuzo za VMA 2014 zimefanyika na mastaa wengi walifika kwenye hilo tukio. Listi ya mastaa hao iliongozwa na familia ya Jay Z na Beyon...
-
Luca Modric mchezaji bora wa mwaka wa FIFA Wameamua kumpa,ni baada ya kumdhurumu tuzo yake ya msimu wa 2009/10,mwaka huu wameona ai...
-
Mlinda mlango wa Derby Country akipangua mkwaju wa Phil Jones Timu ya DERBY COUNTY inayonolewa na nyota wa zamani wa CHELSEA, FRANK LAM...