Friday, 21 September 2018

BUSWITA, MWINYI NA MAKAPU WARUDISHWA KUNDINI YANGA

Wachezaji wa Yanga katika moja ya mazoezi yao 

Taarifa mbalimbali zinasema kuwa uongozi wa klabu ya Yanga ya jiji DSM umewasamehe wachezaji wake watatu viungo Said Makapu na Pius Buswita pamoja na beki wa kushoto Haji Mwinyi ambao hawakuwa sehemu ya mchezo uliopita dhidi ya Stand United kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu.

Wachezaji hao waliondolewa kambini na Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani Mwinyi Zahera kwa utovu wa nidhamu na sasa watakuwa sehemu ya kikosi kuelekea mechi zijazo za Ligi Kuu Bara ikiwemo ya mwishoni mwa juma dhidi ya Singida United.

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera

Imeelezwa kuwa wachezaji hao wameomba radhi kwa Kocha wao ambaye ameonekana kuwa mbogo kwa wale wote wanaoleta ujuaji ndani ya timu bila sababu za msingi.



NAOMI OSAKA AZIDI KUWAPA TABU

Naomi Osaka Bingwa wa US OPEN 
Kinda wa Japan Naomi Osaka atamenyana na Barbara Strycova wa jamhuri ya Czech katika mchezo wa robo fainali ya mashindano ya wazi ya Pan Pacific yanayofanyika jijin Tokyo.

Nyota huyo anayeshika nafasi ya TATU kwenye viwango vya ubora ametinga hatua ya robo fainali baada ya kumtandika bila ya huruma Dominika Cibulkova seti mbili kwa bila za ushindi wa 6-2 6-1 ukiwa ni mchezo wake wa kwanza tangu ashinde taji la mashindano ya wazi ya marekani.

NAOMI mwenye miaka 20 bado anakumbukwa baada ya kumnyuka mkongwe Serena Williams na kushinda taji lake la kwanza la mashindano makubwa (GRANDSLUM) mapema mwezi huu katika fainali ambayo SERENA alizozana vikali na mwamuzi wa mchezo huo.

EUROPA LEAGUE YAMTIA SARRI WOGA

Kocha wa Chelsea Maurizio Sarry
Kocha wa CHELSEA, MAURIZIO SARRI anasema ligi ya YUROPA huenda ikawa janga hapo baadae licha ya kikosi chake kuibuka na ushindi wa bao MOJA kwa BILA dhidi ya PAOK SALONIKA ya UGIRIKI.

SARRI anasema ligi hiyo ni ngumu sana kwa vilabu vya ENGLAND na kuongeza kuwa kama ingekuwa ni ITALIA unaweza kuomba kucheza tena jumatatu usiku lakini kwa ENGLAND unatakiwa kucheza tena baada ya saa 63 kitendo ambacho ni kigumu sana.

Kocha huyo anasema hilo siyo tatizo kwa sasa kwa sababu wamecheza mechi sita tu msimu huu lakini kwa baadae inaweza kuwa tatizo hivyo anatamani wafuzu hatua inayofuata huku wakisaliwa na walau mchezo mmoja au miwili mkononi.

Bao la mapema la WILLIAN limetosha kuwapa CHELSEA alama tatu wakiwa ugenini na kuendeleza wimbi la ushindi kwa asilimia mia moja kwa msimu huu licha ya kucheza kwenye dimba lenye kelele nyingi za mashabiki wenye vibweka vya kila aina pale mjini THESSALONIKI.
Willian akishangilia baada ya kufunga bao 


Ushindi wa jana unamfanya SARRI kuingia katika rekodi ya makocha 10 wa CHELSEA ambao hawajapoteza mchezo wa kwanza wa mashindano ya ulaya wakiwa katika benchi la ufundi huku timu ya PAOK SALONIKA ikishindwa kufunga bao hata moja katika michezo sita kati ya saba iliyopita ya ligi ya YUROPA waliyocheza nyumbani.

UNAI EMERY MFALME WA EUROPA LEAGUE

Unai Emery ameshinda michezo 32 ya ligi ya Europa kama kocha
Kocha wa ARSENAL UNAI EMERY ameweka rekodi ya kushinda michezo 32 ya ligi ya YUROPA ikiwa idadi kubwa ya ushindi kuliko kocha yoyote kwenye hoistoria ya mashindano hayo baada ya ARSENAL kuibuka na ushindi wa mabao MANNE kwa MAWILI dhidi ya VORSKLA POLTAVA ya UKRAINE .

Mabao mawili ya PIERRE EMERIC AUBAMEYANG katika dakika za 32 na 56 na yale ya DANNY WELBECK na MESUT OZIL kwenye dakika ya 48 na 74 yanawafanya ARSENAL kuweka reokodi ya kupoteza mchezo mmoja wa ligi ya YUROPA kati ya 13 iliyopita wakiwa nyumbani ambapo wameshinda michezo 9 na kutoka sare 3 huku mmchezo pekee waliopoteza ukiwa dhidi ya OSTERSUNDS FK February mwaka huu.
Aubameyang akishangilia bao na Hendrick Mkitaryan

Mabao mawili aliyofunga AUBAMEYANG yanamfanya kuweka rekodi ya kufunga mabao 21 katika michezo 25 iliyopita ya michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya na ya ligi ya YUROPA huku akihusika katika mabao 12 katika michezo 10 ARSENAL waliyocheza kwenye dimba lao la EMIRATES ambapo amefunga mabao 9 na kutoa pasi za mabao 3.

Kipigo cha jana kinaifanya timu ya VORSKLA kuendelea kusota katika michuano ya YUROPA bila ya kupata ushindi ambapo katika michezo saba iliyopita wametoka sare miwili na kupoteza mitano huku ARSENAL wakizalisha mabao 25 katika michezo yao sita iliyopita kwenye mashindano yote ambapo wamefunga mabao 14 na kufungwa mabao 11.

SAMATTA AIBEBA GENK EUROPA LEAGUE

Mbwana Samatta akishangilia baada ya kufunga bao
Nahodha wa timu ya taifa ya TANZANIA (Taifa Stars) MBWABA SAMATTA amefunga bao la pili katika ushindi wa mabao MAWILI kwa BILA waliopata timu ya GENK dhidi ya MALMO FC.

LEANDRO TROSSAD alianza kuifungia GENK bao la kwanza katika dakika ya 37 kabala ya SAMATTA kuihakikishia ushindi katika dakika ya 71 kwa kupachika bao la pili na kuzima matumaini ya MALMO ya kupata walau alama moja ya ugenini. 

Katika baadhi ya matokeo mengine ya ligi ya YUROPA, SEVILLA wameitandika STANDARD LIEG mabao MATANO kwa moja, LUDOGORETS wamepokea kipigo cha mabao MATATU kwa MAWILI kutoka kwa BAYER 04 LEVERKUSEN, DINAMO ZAGREB wenyewe wameinyuka FENERBAHCE mabao MANNE kwa MOJA huku OLYIMPIC MARSEILE wakikiona cha moto nyumbani baada ya kutandikwa mabao MAWILI kwa MOJA na EINTRAINCHT FRANKFURT.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...