![]() |
Kocha wa Chelsea Maurizio Sarry |
Kocha wa CHELSEA, MAURIZIO SARRI anasema ligi ya YUROPA huenda ikawa janga hapo baadae licha ya kikosi chake kuibuka na ushindi wa bao MOJA kwa BILA dhidi ya PAOK SALONIKA ya UGIRIKI.
SARRI anasema ligi hiyo ni ngumu sana kwa vilabu vya ENGLAND na kuongeza kuwa kama ingekuwa ni ITALIA unaweza kuomba kucheza tena jumatatu usiku lakini kwa ENGLAND unatakiwa kucheza tena baada ya saa 63 kitendo ambacho ni kigumu sana.
Kocha huyo anasema hilo siyo tatizo kwa sasa kwa sababu wamecheza mechi sita tu msimu huu lakini kwa baadae inaweza kuwa tatizo hivyo anatamani wafuzu hatua inayofuata huku wakisaliwa na walau mchezo mmoja au miwili mkononi.
Bao la mapema la WILLIAN limetosha kuwapa CHELSEA alama tatu wakiwa ugenini na kuendeleza wimbi la ushindi kwa asilimia mia moja kwa msimu huu licha ya kucheza kwenye dimba lenye kelele nyingi za mashabiki wenye vibweka vya kila aina pale mjini THESSALONIKI.
![]() |
Willian akishangilia baada ya kufunga bao |
Ushindi wa jana unamfanya SARRI kuingia katika rekodi ya makocha 10 wa CHELSEA ambao hawajapoteza mchezo wa kwanza wa mashindano ya ulaya wakiwa katika benchi la ufundi huku timu ya PAOK SALONIKA ikishindwa kufunga bao hata moja katika michezo sita kati ya saba iliyopita ya ligi ya YUROPA waliyocheza nyumbani.
No comments:
Post a Comment