![]() |
Unai Emery ameshinda michezo 32 ya ligi ya Europa kama kocha |
Kocha wa ARSENAL UNAI EMERY ameweka rekodi ya kushinda michezo 32 ya ligi ya YUROPA ikiwa idadi kubwa ya ushindi kuliko kocha yoyote kwenye hoistoria ya mashindano hayo baada ya ARSENAL kuibuka na ushindi wa mabao MANNE kwa MAWILI dhidi ya VORSKLA POLTAVA ya UKRAINE .
Mabao mawili ya PIERRE EMERIC AUBAMEYANG katika dakika za 32 na 56 na yale ya DANNY WELBECK na MESUT OZIL kwenye dakika ya 48 na 74 yanawafanya ARSENAL kuweka reokodi ya kupoteza mchezo mmoja wa ligi ya YUROPA kati ya 13 iliyopita wakiwa nyumbani ambapo wameshinda michezo 9 na kutoka sare 3 huku mmchezo pekee waliopoteza ukiwa dhidi ya OSTERSUNDS FK February mwaka huu.
![]() |
Aubameyang akishangilia bao na Hendrick Mkitaryan |
Mabao mawili aliyofunga AUBAMEYANG yanamfanya kuweka rekodi ya kufunga mabao 21 katika michezo 25 iliyopita ya michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya na ya ligi ya YUROPA huku akihusika katika mabao 12 katika michezo 10 ARSENAL waliyocheza kwenye dimba lao la EMIRATES ambapo amefunga mabao 9 na kutoa pasi za mabao 3.
Kipigo cha jana kinaifanya timu ya VORSKLA kuendelea kusota katika michuano ya YUROPA bila ya kupata ushindi ambapo katika michezo saba iliyopita wametoka sare miwili na kupoteza mitano huku ARSENAL wakizalisha mabao 25 katika michezo yao sita iliyopita kwenye mashindano yote ambapo wamefunga mabao 14 na kufungwa mabao 11.
No comments:
Post a Comment