Lupita
Nyong'o wa Kenya ametoka mbali tangu alipopata tuzo ya Oscar ya
mchezaji filamu bora msaidizi wa filamu ya mwaka 2013 iitwayo ''Twelve
Years a Slave''.
Monday, 6 July 2015
Dawa mpya ya ukimwi yakosolewa.ione hapa
Kwa muda mrefu wahudumu wa afya ya masuala ya ngono wamesisitiza
matumizi ya mipira ya kondomu kama mbinu bora zaidi dhidi ya maambukizi
ya virusi vya ukimwi.
Lakini tabia moja hatari ya kutumia madawa ya kulevya na wapenzi wa jinsia moja inazidi kuibua wasiwasi.kumekuwa na njia nyingi za kinga dhidi ya virusi vya ukimwi, lakini kuna dawa moja mpya - Pre-Exposure Prophylaxis (PrEP) - ambayo inaweza kutoa kinga dhidi ya maambukizi ya ukimwi iwapo itatumika kabla ya kushiriki ngono.
Utafiti unaofanywa na daktari Sheena McCormack kutoka chuo kikuu cha London, unasema kwamba unapomeza dawa hiyo, inazuia maambukizi ya ukimwi kwa kuzuia ongezeko la virusi, hii ni baada ya majaribio kufanyiwa kundi moja la wapenzi wa jinsia moja, ambao wamo katika hatari kubwa zaidi ya maambukizi
Shirika la afya duniani limetambua kwamba dawa hiyo ya tembe inaweza kupunguza maambukizi kwa kiwango kikubwa.
Baadhi ya wakosoaji wanasema kuwa dawa ya aina hii inahamasisha watu wengi kushiriki ngono bila kutumia mipira ya kondomu
Hata hivyo matumizi ya dawa hii haizuii maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na kaswende, je, kukubalika kwa matumizi ya dawa hii duniani kunamaanisha ongezeko la magonjwa ya zinaa.
nigeria yapata pigo tena leo,Watu 44 waua katika milipuko nchini Nigeria.
Milipuko hiyo imetokea jioni baada ya waislamu kufungua saumu baada ya kufunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Waumini wa kiislamu walikuwa wamekusanyika msikitini kusikiza hotuba ya kiongozi wa kiislamu anayeogopewa.Punde tu wanaume waliojihami kwa bunduki waliwasili na kuanza kufyetua risasi kiholela kutoka lango kuu la msikiti huo.
Mlipuko ulirushwa miongoni mwa waumini na kuwaua watu hao.
Walioshuhudia mkasa huo wanasema wapiganaji wa Boko Haram wanaonekana kumlenga kiongozi huyo ambaye katika siku za nyuma ameshutumu mashambulio na harakati za kundi la wanaamgambo hao.
Polisi katika mji wa Jos hawakuweza kutoa taarifa zaidi, lakini wakaazi wanasema idadi ya waliofariki ipo juu.
Watu watano wameuawa katika mlipuko mwingine wa kujitoa muhanga uliotokea mapema asubuhi kwenye kanisa mjini Potiskum kaskazini mashriki mwa Nigeria.
Milipuko ya Jumapili yamejiri baada ya wiki nzima ya ghasia zilizosababisha vifo vya watu takriban mia mbili.
Serikali imeshutumu mauaji hayo ambayo katika mwezi uliopita yameongezeka.
Maandalizi ya kombe la Kagame Cup yaendelea
Maandalizi
kwa ajili ya michuano ya kombe la Kagame Cup yanaendelea huku timu
zikijiandaa na michuano hiyo.Ratiba na makundi ya michuano hiyo tayari
imetangazwa jijini Dar es Salaam na Baraza la Vyama vya Soka la Afrika
ya Mashariki na Kati (Cecafa).
Michuano hiyo ya Cecafa Cup inadhaminiwa na Raisi wa Rwanda, Paul Kagame. Itaanza jijini Dar es Salaam July 18 mpaka Agosti 2.KCC F.C ya Uganda imepangwa kundi moja na timu mwenyeji, Azam ya Tanzania, Malakia ya Sudani Kusini na Adama ya Ethiopia.
Ratiba iliyotolewa na katibu mkuu wa Cecafa, Nicholus Musonye inaonesha kuwa mabingwa watetezi wa Tanzania Bara, Yanga watacheza na timu ya Kenya, Gor Mahia katika mechi ya ufunguzi.
KMKM ya Zanzibar itacheza na Telecom ya Kenya wakati APR ya Rwanda itacheza na Al-Shandy ya Sudan
Timu ya Ek-Merreikh ya Sudan ndio bingwa mtetezi baada ya kuifunga APR ya Rwanda bao 1-0 katika fainali. Michuano hiyo inafanyika kila mwaka na kuandaliwa na moja kati ya nchi wanachama itakayochanguliwa na Cecafa. Hata hivyo, timu ya El-Merreikh haipo katika ratiba ya michuano ya mwaka huu.
Makundi yaliyopangwa ni kama ifuatavyo.
Kundi A
Young Africans
Gor Mahia
Telecom
KMKM
Kundi B:
APR
El Shandy
LLB
Heegan
Kundi C:
Azam F.C
KCC F.C
Malakia
Adama
Subscribe to:
Posts (Atom)
CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA
Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...

-
Tuzo za VMA 2014 zimefanyika na mastaa wengi walifika kwenye hilo tukio. Listi ya mastaa hao iliongozwa na familia ya Jay Z na Beyon...
-
Luca Modric mchezaji bora wa mwaka wa FIFA Wameamua kumpa,ni baada ya kumdhurumu tuzo yake ya msimu wa 2009/10,mwaka huu wameona ai...
-
Mlinda mlango wa Derby Country akipangua mkwaju wa Phil Jones Timu ya DERBY COUNTY inayonolewa na nyota wa zamani wa CHELSEA, FRANK LAM...