Maandalizi
kwa ajili ya michuano ya kombe la Kagame Cup yanaendelea huku timu
zikijiandaa na michuano hiyo.Ratiba na makundi ya michuano hiyo tayari
imetangazwa jijini Dar es Salaam na Baraza la Vyama vya Soka la Afrika
ya Mashariki na Kati (Cecafa).
Michuano hiyo ya Cecafa Cup inadhaminiwa na Raisi wa Rwanda, Paul Kagame. Itaanza jijini Dar es Salaam July 18 mpaka Agosti 2.KCC F.C ya Uganda imepangwa kundi moja na timu mwenyeji, Azam ya Tanzania, Malakia ya Sudani Kusini na Adama ya Ethiopia.
Ratiba iliyotolewa na katibu mkuu wa Cecafa, Nicholus Musonye inaonesha kuwa mabingwa watetezi wa Tanzania Bara, Yanga watacheza na timu ya Kenya, Gor Mahia katika mechi ya ufunguzi.
KMKM ya Zanzibar itacheza na Telecom ya Kenya wakati APR ya Rwanda itacheza na Al-Shandy ya Sudan
Timu ya Ek-Merreikh ya Sudan ndio bingwa mtetezi baada ya kuifunga APR ya Rwanda bao 1-0 katika fainali. Michuano hiyo inafanyika kila mwaka na kuandaliwa na moja kati ya nchi wanachama itakayochanguliwa na Cecafa. Hata hivyo, timu ya El-Merreikh haipo katika ratiba ya michuano ya mwaka huu.
Makundi yaliyopangwa ni kama ifuatavyo.
Kundi A
Young Africans
Gor Mahia
Telecom
KMKM
Kundi B:
APR
El Shandy
LLB
Heegan
Kundi C:
Azam F.C
KCC F.C
Malakia
Adama
No comments:
Post a Comment