Thursday, 11 June 2015

kifaa kipya kinachotua Yanga hiki hapa baada ya kuondoka coutinho


Mshambuliaji wa Platinum FC ya Zimbabwe, Donaldo Ngoma anatarajiwa kuwasili Tanzania kwa ajili ya kukamilisha mazungumzo ya kujiunga na mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga.
Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam muda wowote kuanzia sasa, kwa mujibu wa uongozi wa Yanga.
Yanga, wakiwa na kibarua cha kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika mwakani, ipo katika nchakato wa kusajili wachezaji mahiri kwa ajili ya msimu ujao wa 2015/16 wa ligi kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa. Hatua ya kujiimarisha inakuwa baada ya Yanga kutolewa katika ligi ya Kombe la Shirikisho mwaka huu na timu ya Etoile du Sahel ya Tunisia.
Yanga ilivutiwa na Ngoma wakati ilipocheza na Platimun FC katika mechi za awali za Kombe la Shirikisho mwaka huu na kuitoa timu hiyo kutoka kusini mwa Afrika

Wataalamu kutoka Uingereza kuifundisha Azam FC hawa hapa

Benchi la ufundi la Azam FC sasa litakuwa chini ya Stewart Hall wakwanza kushoto
Sasa kazi imeanza, Mkurugenzi wa Fedha na utawala wa Azam FC toka nchini Uingereza pamoja na wasaidizi wa benchi la ufundi kuwasili ijumaa hii tayari kuanza kazi Azam FC kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara.Azam pia wataiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika hapo mwakani baada ya kumaliza washindi wa pili katika msimu wa ligi uliokwisha.
Habari zilizopatikana kutoka mtandao wa klabu ya Azam zimesema kufuatia mabadliko makubwa ya watendaji na mfumo wake wa uongozi, benchi la ufundi la Azam FC sasa litakuwa chini ya Stewart Hall ambaye yupo jijini Dar es Salaam akisubiri kuwapokea wasaidizi wake ijumaa hii.
Watakaowasili ni pamoja na muingereza mwenye asili ya Uganda Eli Eribankya ambaye atakuwa Meneja utawala na fedha. Eribankya atasaidiwa na mwanandinga wa zamani wa Azam FC mtanzania Luckson Kakolaki.
Stewart John Hall ambaye anarejea kwa mara ya tatu kuongoza benchi la ufundi la Azam FC. atasaidiwa na Mganda George Best Nsimbe, huku Mark Philips kutoka uingereza akiajiriwa kuwa kocha wa magolikipa. Hawa wote watawasili ijumaa hii.
Wengine watakaowasili ni Mark Philips atakayekuwa kocha wa magolikipa. Mtaalamu wa tiba ya viungo na lishe “Team Physiotherapist and Nutritionist” Bwana George Adrian Dobre kutoka Romania na Mario Marian Anton Marinica kutoka Romania atakayeongoza benchi la ufundi la timu ya vijana.
Azam FC itaanza mazoezi kujiandaa na Kagame Cup Jumanne ijayo

Andre Ayew asajiliwa ligi kuu uingereza,ijue timu aliyosajiliwa hapa,

Mshambuliaji wa Ghana Andre Ayew amejiunga na kilabu ya Swansea kwa uhamisho wa bure na kuandikisha mtakataba wa miaka minne na kilabu hiyo.

Ayew mwenye umri wa miaka 25,amekuwa katika kilabu ya Marseille tangu mwaka 2006 lakini mkataba wake na kilabu hiyo ya Ligue 1 ulikamilika mwezi uliopita.
Mchezaji huyo aliyetajwa kuwa mchezaji bora na BBC mwaka huu alifunga mabao 52 katika mechi 181 katika kilabu hiyo na amelichezea taifa lake mara 62.
''Nilihisi kwamba huu ndio wakati mwafaka kwangu'',alisema Ayew. Nilihisi hamu ya kucheza katika ligi ya Uingereza na kutaka kukuwa kama mchezaji na kwamba Swansea ndio suluhu kwangu kwa njia yoyote''.
"Uaminifu na hamu ya klabu hiyo ulinifanya kujihisi kwamba ni kweli wananitaka.Wameonyesha hilo kwa kila njia''.

Ebola yarudi tena kwa kasi kubwa sana.


Shirika la afya duniani WHO limeelezea wasiwasi wake kwamba visa vipya vya maambukizi ya maradhi hatari ya Ebola vimeongezeka huko Guinea na Sierra Leone katika kipindi cha wiki tatu zilizopita.
WHO liliripoti kesi 31 mpya katika mataifa hayo mawili.
Uchunguzi unaonyesha kuwa tamaduni za mazishi ndizo zinachangia kusambaa kwa kasi kwa maradhi hayo licha ya tahadhari na mafunzo kupewa raia wa nchi kwamba waripoti visa vyovyote vinavyoshukiwa kuwa vya maambukizo ya Ebola na kuachia maafisa wa matibabu shughuli za mazishi ili yafanyike kwa utaratibu uliofuatwa.

Maporomoko yawaua watu 15 Nepal 11 Juni 2015


Maporomoko nchini Nepal
Takriban watu 15 wamefariki huko Nepal baada ya maporomoko yaliosababishwa na mvua kubwa kuvizika vijiji sita huko kazkakazini mashariki.
Watu wengi wameathiriika na maporomoko hayo, huku idadi kubwa ya watu ikiwa haijulikani ilipo.
Katika jimbo la Taplejung, afisa wa serikali Surendra Bhattarai, amesema kuwa makundi ya maafisa wa utoaji msaada yamefika katika kingo za mito miwili mikubwa ya Mewa na Tamor, ili kuwatafuta watu ambao walisombwa na maji ya mafuriko.
Hali ya hewa nchini Nepal
Nepal,ndio mwanzo inajizoazoa kutokana na tetemeko baya la ardhi lililotokea mwezi wa Aprili na Mei, ambalo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu elfu nane na mia saba.

exclussive video mpya kutoka kwa Psquare ‘Bring It On’ feat. Dave Scott…hawa jamaa ni shida huko marekani.



PSQUP Square wameachia video yao mpya inayoitwa ‘Bring It On’, Ni nyimbo iliyopo kwenye albamu yao mpya ya Double Trouble.
Katika video hiyo yenye vionjo vya R&B na Rock ilifanyika Atlanta na Afrika Kusini huku ndani wakimshirikisha Dave Scott.
Nakukaribisha hapa kuitazama.





CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...