Monday, 11 May 2015

kauli ya kocha mkuu wa simba sport club hii hapa kuhusu kikosi chake kwa sasa.



Kikosi cha watoto wa Msimbazi ,Simba
Kocha mkuu wa Simba Mserbia, Goran Kopunovic amesema ameridhishwa na timu yake kushinda nafasi ya tatu katika ligi kuu ya Tanzania Bara iliyomalizika hivi karibuni.
Kopunovic amesema Simba pia ilikuwa na ndoto ya ubingwa, lakini ndoto hiyo ilifutika kutokana na kutofanya vizuri katika mechi za nyuma.
Simba ilianza vibaya ligi hiyo kwa kukumbwa na droo saba mfululizo katika mechi zake saba za mwanzo ikiwa chini ya kocha aliyeondolewa, Mzambia Patrick Phiri.
Kocha huyo amesema anajivunia kuwa na kikosi imara na ana imani timu hiyo itafanya vizuri sana katika msimu ujao.
“Ubingwa tumeukosa, lakini huu sio mwisho wa safari, ni mwanzo wa safari ya msimu ujao” amesema kocha huyo, Simba ilikuwa katika vita ya kugombania nafasi ya pili na Azam, lakini pia ilishindikana.
Yanga, watani wa jadi wa Simba, ndio mabingwa wa ligi hiyo katika msimu wa 2014/2015 wakifuatiwa na waliokuwa mabingwa watetezi, Azam FC na Simba wakiikwaa nafasi ya tatu, hivyo kuwa nje ya michuano ya kimataifa hapo mwakani.
Yanga wataiwakilisha Tanzania katika michuano ya kombe la Washindi barani Afrika wakati Azam watabeba bendera ya nchi katika michuano ya kombe la Shirikisho.
Timu zilizoshuka daraja katika ligi hiyo ni za Ruvu Shooting na Polisi Morogoro ambazo msimu ujao zitacheza Ligi Daraja la Kwanza

wakimbizi zaidi ya 8000 wakwama baharini karibu na thailand



Wakimbizi wakwama baharini karibu na Thailand
Shirika la kimataifa la wahamiaji IOM, linasema kuwa maelfu ya wakimbizi kutoka Bangladesh na Myanmar, wamekwama baharini karibu na Thailand baada na kushindwa kufika ardhini.
Msemaji wa IOM aliiambia BBC kuwa hatua za hivi majuzi za kukabiliana na wahamiaji haramu kutoka jamii ya Rohingya ina maana kuwa walanguzi hawawezi kuwafikisha ardhini wahamiaji na sasa karibu watu 8,000 wemekwama kwenye mashua.
Katika siku mbili zilizopita, zaidi ya wakimbizi 100 walifika nchini Malaysia na Mynmar.
Waandishi wanasema kuwa wahamiaji hao ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wauzwe na baadaye wazuiliwe kwa fidia na watu wanaofanya biashara haramu ya watu nchini Thailand.

JE UMESIKIA HII? NDEGE ZISIZOKUA NA MARUBANI KURUKA MAKEKANI. ONA HAPA

Utumizi wa ndege zisizo na rubani US

8 Mei 2015 Imebadilishwa mwisho saa 16:49 GMT
Wiki hii kulikuwa na habari muhimu kuhusu utumizi wa ndege zisizokuwa na rubani nchini marekani.Shirika linalosimamia anga za juu limesema kuwa litashirikiana na kampuni nyengine tatu ili kulisaidia katika kupanua utumizi wa ndege hizo.Ukaguzi uliofanywa umesema kuwa ndege hizo zitatumika katika kuangalia mimea,kukagua barabara za treni mbali na kuangazia habari.

MTOTO ASAFIRISHWA KWA BEGI , TAZAMA TUKIO ZIMA


Mtoto aliyebebwa ndani ya sanduku
Mtoto mmoja wa miaka minane amesafirishwa hadi nchini Uhispania kutoka Morroco akiwa ndani ya sanduku kwa mujibu wa maafisa wa polisi wa Uhispania.
Mvulana huyo kwa jina Abou alipatikana ndani ya sanduku hilo lililokuwa limebebwa na msichana wa miaka 19 kuelekea Cueta,eneo lililo karibu na taifa la Morrocco siku ya alhamisi.
Wakati polisi walipolifungua sanduku hilo, mvulana huyo alikuwa katika hali mbaya sana.Mvulana huyo kutoka Ivory Coast sasa anahudumiwa na mamlaka ya Cueta.
Gazeti la Uhispania El Paris liliripoti kwamba msichana huyo wa miaka 19 hana uhusiano na mtoto huyo na kwamba alilipwa na babaake ili kubeba sanduku hilo.
Babaake mtoto huyo anaishi katika visiwa vya Conary na kwamba alitarajia kuonana na mwanawe kulingana na gazeti hilo.
Mtoto aliyebebwa ndani ya sanduku
Chombo cha habari cha Uhispania Efe kimesema kuwa babaake mvulana huyo ambaye anajulikana kama Abou alisafiri hadi nchini Ivory Coast kumchukua mwanawe baada ya kuhamia katika eneo la Gran Canaria mwaka 2013.
Babaake baadaye aliripotiwa kumlipa raia huyo wa Morocco ambaye alimsafirisha mtoto huyo kupitia sanduku.
Msemaji wa polisi aliiambia Efe:''Alionekana kusita na kama ambaye hakutaka kupitia mpakani''.

TANZANIA YAKUBALI KUA MWANDAAJI WA FAINALI ZA KAGAME . ONA UTAMU HUU


Mabingwa watetezi wa Kagame Cup,El-Merreikh ya Sudan.
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) imekubali kuwa wenyeji wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ngazi ya vilabu inayojulikana kama Kagame Cup.
Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ambao ndio wamiliki wa mashindano haya na hutoa mialiko kwa vilabu vyenye sifa ya kushiriki. Watatoa orodha ya vilabu shiriki na ratiba ya michuano hiyo baade mwezi huu au mapema mwezi ujao.
Afisa habari wa TFF, Baraka Kizuguto amesema uamuzi wa kukubali kuwa wenyeji umetolewa na shirikisho hilo mapema Jumapili baada ya kuombwa na Cecafa.
Michuano hii inatarajiwa kufanyika nchini Tanzania kuanzia tarehe 11 Julai mpaka 02 Agosti 2015.
Michuano hiyo inadhaminiwa na Raisi wa Rwanda, Paul Kagame na hufanyika kila mwaka katika nchi mwanachama za ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati. Rwanda ndio ilikuwa mwenyeji wa michuano ya mwaka jana inayohusisha vilabu.

SERIKALI YA KOREA YA KASKAZINI YAZINDUA SILAHA KUBWA MNO ZA KIVITA. TAZAMA HAPA .


Korea Kaskazini yazindua Silaha kali
Serikali ya Korea Kusini inasema inaamini kuwa Korea Kaskazini inaweza kumiliki nyambizi kadha za kufanya mashambulizi kutoka baharini ndani ya miaka mitano inayokuja.
Hii ni baada ya Korea Kaskazini kuchapisha picha zilizomuonyesha kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un akitazama majaribio ya kuizindua nyambizi hiyo.
Korea Kusini imezikagua picha hizo za uzinduzi kwenye vyombo vya habari vya Korea Kaskazini na kusema kuwa ni za kweli.
Korea Kusini ilisema kuwa uzinduzi huo ni suala linalochukuliwa kwa umakini na tahadhari kubwa sana.
Sasa Korea Kusini na Marekani zinafikiria kuweka ngao ya mitambo ya kuzuia makombora kutoka Kaskazini hatua itakayogharimu mabilioni ya pesa.
Korea Kusini ilisema kuwa uzinduzi huo ni suala linalochukuliwa kwa umakini na tahadhari kubwa
Hata hivyo haijulikani ikiwa makombora yanayofyatuliwa na nyambizi hiyo yana uwezo wa kubeba silaha za nuklia
Wadadisi wanasema kuwa Korea Kuskazini inaonekana kufanya mambo kwa kasi zaidi kuliko ilivyokisiwa kuunda zana zilizo na uwezo wa kushambulia kwa haraka.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...