Friday, 1 May 2015

ONA PICHA ZOTE ZA HARUSI YA WEMA SEPETU NA ALICHOSEMA KATIKA KURASA ZAKE BAADA YA KUFUNGA NDOA YA BOMANI ..



WSepetu

Sepetuur


Kuhusu ishu ya kutopata mtoto Wema amesema mwanaume huyo anajua na amekubaliana na hiyo hali lakini inawezekana kwake wakapata mtoto.

MUONE MWANAHARAKATI MDOGO DUNIANI KUTOKA PAKISTANI ALIYEPIGWA RISASI KWA AJILI YA KUTETEA HAKI ZA WOTOTO. WALIOMPGA RISASI WAFUNGWA MAISHA


malala-yousafzai-nobel-prize-winnerJina la Malala Yousafzai liliwahi kukaa kwenye vichwa vya habari vya Kimataifa mwaka 2012 kutokana na tukio la msichana huyo kupigwa risasi akiwa ndani ya basi lao la shule.
Malala alikuwa na umri wa miaka 15 wakati huo, tukio la kupigwa risasi linahusishwa na ishu yake kujihusisha na harakati za kudai haki za watoto hasa wa kike kwenye suala la elimu.
Mwaka 2014 jina lake likarudi tena kwenye headlines baada ya kupewa Tuzo ya amani ya Nobel, kilichoripotiwa leo kinarudisha kumbukumbu ya tukio la kupigwa risasi mwaka 2012.
Watuhumiwa 10 ambao walikamatwa kwa kesi ya kuhusika na tukio la kumpiga risasiMalala wamehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Malala Yousafzai lying in hospital bed
Malala baada ya shambulio akiwa Hospitali.
Baada ya kupigwa risasi Malala alifanyiwa upasuaji Uingereza, baada ya hali yake kukaa sawa ameendelea na kampeni zake Kimataifa.
Malala ni mmoja ya watu wenye umri mdogo na wana rekodi kubwa.. wakati anatunukiwa Tuzo ya Nobel alikuwa na umri wa miaka 17 tu.
Nobel Peace Prize laureate Malala Yousafzai poses with her medal during the Nobel Peace Prize awards ceremony at the City Hall in Oslo December 10, 2014. Pakistani teenager Malala Yousafzai, shot by the Taliban for refusing to quit school, and Indian activist Kailash Satyarthi received their Nobel Peace Prizes on Wednesday after two days of celebration honouring their work for children's rights. REUTERS/Cornelius Poppe/NTB Scanpix/Pool   (NORWAY  - Tags: SOCIETY CIVIL UNREST TPX IMAGES OF THE DAY) NORWAY OUT. NO COMMERCIAL OR EDITORIAL SALES IN NORWAY.
Malala alipotunukiwa Tuzo ya Nobel

LEO NI SIKU KUU YA WAFANYA KAZI DUNIANI KOTE. TAZAMA MATUKIO HAPA PAMOJA NA MIGOMO YA KUTAKA MISHAHARA IONGEZWE KATIKA NCHI MBALI MBALI


Leo ni Siku ya Wafanyakazi Duniani, ambapo wafanyakazi duniani kote wanaungana na wenzao kuadhimisha siku hii, huku kinachoangaziwa zaidi kwa mwaka huu wa 2015 kikiwa ni 'mazingira salama na mazuri kwa afya kazini'.
Wafanyakazi wakiandamana Taiwan, kudai nyongeza ya mishahara
Wafanyakazi wakiandamana Taiwan, kudai nyongeza ya mishahara
Shirika la Kazi Duniani-ILO, limetoa wito siku ya wafanyakazi duniani kwa mwaka huu kuzingatia zaidi usalama na afya kazini na hali hiyo inapaswa kuheshimiwa kwa wafanyakazi wa ngazi zote.
Kwa mujibu wa ILO, serikali, waajiri pamoja na wafanyakazi wanatakiwa kushiriki katika kuhakikisha mazingira ya kufanyia kazi ni salama kwa afya ya wafanyakazi, mfumo ambao utaelezea haki, majukumu na wajibu, ambapo kipaumbele kikubwa kikiwa kuhakikisha kuna mazingira mazuri.
Siku hii leo inaadhimishwa kwa maandamano, ambapo viongozi wa mataifa wamekuwa wakitoa hutuba zao kuzungumzia masuala mbalimbali yakiwemo yanayohusu maslahi ya wafanyakazi.
Mjini Berlin, Ujerumani, kiasi watu 200,000 wanatarajiwa kushiriki katika maandamano yaliyoandaliwa na mashirika ya wafanyakazi yanayofuata mrengo wa kushoto, huku kukiwa na ulinzi mkubwa wa polisi.
Aidha, polisi mjini Istanbul, Uturuki wako katika tahadhari, baada ya serikali kuonya kuhusu uchochezi wowote utakaofanywa, huku serikali ikiufunga uwanja muhimu wa Taksim kuwazuia waandamanaji.
Maandamano ya kudai haki za wafanyakazi
Kwa upande wa Urusi, vyama vya wafanyakazi vitakutana kwenye uwanja Mwekundu mjini Moscow, sambamba na maandamano mengine yaliyoandaliwa na Chama cha Kikomunisti ambapo wafuasi wake watakutana katikati ya mji wa Moscow.
Nembo ya Shirika la Kazi Duniani-ILO
Nembo ya Shirika la Kazi Duniani-ILO
Nchini Afrika Kusini ambako hivi karibuni kulikuwa na vurugu zinazofanywa dhidi ya raia wa kigeni na kusababisha watu 6 kuuawa, vyama vya wafanyakazi vitafanya maandamano nchi nzima katika kuiadhimisha siku huu.
Ama kwa upande mwingine wafanyakazi barani Asia wameandamana kupinga mageuzi ya ajira yaliyofanywa na serikali. Korea Kusini, wafanyakazi wameandamana wakiapa kufanya mgomo wa nchi nzima iwapo serikali itaendelea kushinikiza mipango yake ya kufanya mageuzi ya ajira. Serikali ya kihafidhina ya Rais Park Geun-Hye inapanga kufanya mageuzi yatakayolihusu soko la ajira, ikiwemo urahisi wa kuwaajiri na kuwafukuza kazi wafanyakazi.
Huko Taiwan, wafanyakazi walirusha mabomu ya kutoa machozi karibu na ofisi ya rais, wakimtaka atekeleze ahadi yake ya kuongeza mishahara pamoja na kulitafutia ufumbuzi suala la ukosefu wa ajira.
Nako Hong Kong wafanyakazi wa nyumbani nao wameandamana wakidai nyongeza ya mishahara pamoja na mazingira mazuri ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi ambao ni raia pamoja na wahamiaji.
Siku ya Wafanyakazi Duniani ilianzishwa mwaka 1886 kwa lengo la kumaliza mapambano pamoja na kuhimiza umuhimu wa muda wa saa nane wa kazi kwa siku. Awali mazingira ya kufanyika kazi yalikuwa magumu na watu walifanya kazi kwa muda wa saa 10 hadi 16 kwa siku.

BABA YAKE DIAMOND ATOA TAMKO SIKU MOJA KABLA YA ZARI WHITE PARTY .TAZAMA HAPA








DSC02005
DSC02007

BABA YAKE DIAMOND ATOA TAMKO SIKU MOJA KABLA YA ZARI WHITE PARTY .TAZAMA HAPA






DSC02005
DSC02007

diamond na zari the boss hawa hapa kwenda white party. tazama picha na matukio ya white clothes .exclusive hivi punde wanahojiwa

IMG_4056I
IMG_4056
IMG_3977
.
IMG_3981
.
IMG_4045
Diamond na Zari wakiwa wanafika kwenye studio za Clouds Media. Nyuma yao kuna support ya nguvu ya mabaunsa wao.
IMG_4056
IMG_4060
IMG_4065
Mtangazaji Gerald Hando anasalimiana na Zari.
IMG_4106
IMG_4144
IMG_4185
Mkono wa kushoto wa Zari unaonekana na pete, ndiyo kusema shughuli tayari kweli??
IMG_4192
Le Mutuz, mmoja ya Bloggers TZ
IMG_4242
IMG_4258
Diamond na Zari wanapiga picha na wanafamilia wengine wa Clouds FM.
IMG_4284
Baada ya kumaliza Diamond na Zari waliondoka kwen

DROGBA apewa tuzo nyingine ya heshima ya soka la uingereza. pia anafanya makubwa kimaendeleo nchini kwao tazama hapa

droooMbali na uwezo wake mkubwa wa kumiliki mpira uwanjani, Didier Drogba raia wa Ivory Coast amekuwa na mchango mkubwa katika shughuli za kijamii ambazo ambazo amekuwa akishiriki ndani ya nchi yake na Afrika kwa ujumla.
Uongozi wa ligi kuu ya England umeona ni vyema ukaonyesha kuridhishwa na kazi zake na kuamua kumpa tuzo kutokana na mchango wake mkubwa wa kuhamasisha soka la vijana Afrika kupitia michango yake na uamuzi wake wa kufungua Didier Drogba Foundation ambayo itakuwa ikifanya kazi ya kuwasaidia wenye matatizo.
tuzo
Staa huyo wa soka wa Chelsea amepewa heshima hiyo kubwa na uongozi huo kama sehemu ya kumpongeza kwa kazi nzuri za kijamii anazofanya.
Tayari Drogba amejenga hospitali kubwa ya kisasa nchini kwao Ivory Coast.

MAANDAMANO MAPYA MALTIMORE NCHINI MAREKANI.


Kumetokea maandamano mapya nchini Marekani katika mji wa Baltimore kufuatia kifo cha kijana mweusi Freddie Gray aliyekufa kutokana na majeraha akiwa mikononi mwa polisi. Mamia ya watu wameandamana katika mitaa, wakionyesha ujasiri licha ya hali mbaya ya hewa iliyokuwepo.
Matokeo ya mwanzo ya uchunguzi wa polisi wa jinsi kijana wa miaka ishirini na mitano mwenye asili ya weusi alivyouawa bado hayajawekwa hadharani.
Maandamano Baltimore
Mtetezi wa haki za binadamu, Mchungaji Al Sharpton, ameitisha mkutano mjini Baltimore ili kuimarisha uhusiano baina ya polisi na wanajamii.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...