Friday, 1 May 2015

MUONE MWANAHARAKATI MDOGO DUNIANI KUTOKA PAKISTANI ALIYEPIGWA RISASI KWA AJILI YA KUTETEA HAKI ZA WOTOTO. WALIOMPGA RISASI WAFUNGWA MAISHA


malala-yousafzai-nobel-prize-winnerJina la Malala Yousafzai liliwahi kukaa kwenye vichwa vya habari vya Kimataifa mwaka 2012 kutokana na tukio la msichana huyo kupigwa risasi akiwa ndani ya basi lao la shule.
Malala alikuwa na umri wa miaka 15 wakati huo, tukio la kupigwa risasi linahusishwa na ishu yake kujihusisha na harakati za kudai haki za watoto hasa wa kike kwenye suala la elimu.
Mwaka 2014 jina lake likarudi tena kwenye headlines baada ya kupewa Tuzo ya amani ya Nobel, kilichoripotiwa leo kinarudisha kumbukumbu ya tukio la kupigwa risasi mwaka 2012.
Watuhumiwa 10 ambao walikamatwa kwa kesi ya kuhusika na tukio la kumpiga risasiMalala wamehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Malala Yousafzai lying in hospital bed
Malala baada ya shambulio akiwa Hospitali.
Baada ya kupigwa risasi Malala alifanyiwa upasuaji Uingereza, baada ya hali yake kukaa sawa ameendelea na kampeni zake Kimataifa.
Malala ni mmoja ya watu wenye umri mdogo na wana rekodi kubwa.. wakati anatunukiwa Tuzo ya Nobel alikuwa na umri wa miaka 17 tu.
Nobel Peace Prize laureate Malala Yousafzai poses with her medal during the Nobel Peace Prize awards ceremony at the City Hall in Oslo December 10, 2014. Pakistani teenager Malala Yousafzai, shot by the Taliban for refusing to quit school, and Indian activist Kailash Satyarthi received their Nobel Peace Prizes on Wednesday after two days of celebration honouring their work for children's rights. REUTERS/Cornelius Poppe/NTB Scanpix/Pool   (NORWAY  - Tags: SOCIETY CIVIL UNREST TPX IMAGES OF THE DAY) NORWAY OUT. NO COMMERCIAL OR EDITORIAL SALES IN NORWAY.
Malala alipotunukiwa Tuzo ya Nobel

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...