Friday, 17 April 2015

TAZAMA PICHA ZAIDI HAPA JINSI WAAFRIKA KUSINI WANAVYOBEBA MAPANGANA MASHOKA KWA KUWAUA WAAFRIKA TOKA NCHI ZINGINE BARANI AFRIKA


Like · Comment ·  · 692717

SOMA HAPA UJUE NI KWA NINI WANAUME WANAJITOA UHAI. UTAFITI SAHIHI HUU HAPA .


Utafiti umeonesha kuwa wanaume wenye umri kati ya 40-50 wamo katika hatari kubwa ya kujinyonga
Wanaume wengi wenye umri kati ya miaka arobaini na 50 wamo katika hatari kubwa ya kujiua kuliko wanawake.
Kijana mmoja kutoka Uingereza ,Simon Jack alifanya utafiti huo baada ya baba yake kujiua katika siku yake ya kuzaliwa miaka 25 iliyopita akiwa na umri wa miaka 44.
Jack anasema alianza kuwa mdadisi kwa simulizi zote au habari kuhusu watu wanaojiua na amegundua kuwa wote ni wanaume.
Wanaume wanazongwa na mawazo na hawana wa kusema naye
''Sikujua kuwa kujiua ni adui mkubwa wa watu wenye umri chini ya miaka 50,ila sasa nafahamu kwanini wanaume mia moja wamejiua ndani ya wiki''.
Idadi hiyo imekuwa kubwa zaidi kuliko wakati wowote katika miaka 14 iliyopita ya wanaume wanaomaliza maisha yao wenyewe ni mara nne ya wanawake.
Jack,alitamani kufahamu sababu inayowafanya wanaume kufanya matukio hayo zaidi.
Na kama kuna namna yeyote ya kuzuia mauaji haya, ''Nilijiuliza nini kinachopelekea wanaume hawa kufanya hivi?
Simon Jack akielezea matokeo ya utafiti wake
''Miaka 40 ni miaka ambayo mtu ana majukumu mengi, Unaweza kudhani kuwa mke wake amemuacha na kuchukua watoto wote,au kapoteza kazi yake katika umri huo wakati ni vigumu kupata mwingine''alihoji Jack.
''Au sababu yoyote ambayo inaweza kumpa shinikizo mwanaume ambaye anahitajika kuhudumia familia yake''.
Kwa upande wa baba yake Jack, haikuwa hivyo kwani alikuwa ni baba mzuri mwenye upendo kwa familia yake,mwenye uwezo nau maarufu.
Simon Jack katika kaburi la babake
Kila mtu atakubali kuwa ni tatizo kubwa katika familia pale unapompoteza mtu kwa sababu ya ugumu wa maisha uliokithiri au kuachwa na mpendwa wako.
Wengine walitoa maoni kuwa wengi wanaojiua ni ushahidi tosha kuwa wana matatizo ya kiakili au wana msongo wa mawazo au huzuni katika maisha.
Prof Rory O'Connor ambaye anaongoza kituo maarufu duniani cha utafiti katika chuo kikuu cha Glasgow,
anasema tabia ya kujuiua ni tatizo la kisaikolojia ambalo hutokana na upungufu wa kiakili.
Jack akiwa na babake ufukweni
Ingawa watu wenye matatizo ya akili uwa ni vigumu sana kujiua ni asilimia tano tu ndio wanaweza kujiua kutokana na upungufu wa akili.
Hata hivyo katika maamuzi kuna tofauti kubwa kati ya namna wanaume na wanawake wanavyo weza kujielezea matatizo yao na kuyatatua.
''wanawake huwa wanatumia njia za kujieleza ambazo ni rahisi watu kumuokoa tofauti na wanaume''
Jack anasema ”Natamani kujua nini kilimpata baba yangu kwani fumbo hili linaweza jibu maswali ya familia nyingi wenye matatizo kama yangu”.

arsene wenger amesema ushindi unahitajika mapema sana ,soma hapa



Arsene Wenger

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameitaka timu yake kutafuta ushindi wa mapema katika pambano la mwishoni mwa wiki hii Jumamosi dhidi ya Reading. Kocha huyo raia wa Ufaransa amesema kuwa vijana wake wanapaswa kuanza kwa kasi na nguvu katika mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Wembley kama kweli wanahitaji kutetea taji lao.
Wenger amesema kwamba timu yake imejifunza msimu uliopita ambapo walihitaji penati kuishinda Wigan katika hatua ya nusu fainali kabla ya kutanguliwa goli mbili na wapinzani wao Hull City katika pambano la fainali ambapo hadi mwisho wa kipute hicho, waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 3-2.
Mechi hiyo itakuwa ni nusu fainali ya kumi kwa mzee Wenger ,huku akidai kwamba Arsenal inajiamini hasa kutokana na kushinda mechi nane mfululizo. Nusu fainali ya pili itapigwa Jumapili ambapo Aston Villa itawakaribisha Liverpool.

Wageni waendelea kushambuliwa afrika kusini na kuuwawa wakiwepo kutoka tanzania .



Raia wa kigeni ashambuliwa Afrika Kusini
Kumekuwa na mashambulizi zaidi usiku dhidi ya biashara zinazomilikiwa na raia wa kigeni nchini Afrika Kusini.
Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mipira kutawanya umati kusini mwa mji wa Johannesburg ambapo gari na nyumba vilichomwa moto.
Msemaji wa polisi aliiambia BBC kuwa karibu raia mia mbili wa kigeni walikimbilia usalama kwenye kituo cha polisi lakini wakaondoka muda baadaye.
Maandamano ya kupinga uvamizi wa wageni
Usalama umedumishwa kufuatia mashambulizi yaliyowalenga raia wa kigeni ambapo watu watano wameuawa.
Rais Jacob Zua amelaani ghasia hizo na maandamano ya amani mjini Durban siku ya Alhamisi yalihudhuriwa na zaidi ya watu elfu kumi.

ajali nyingine yatokea mbeya leo jionee hapa tukio zima

 Tukuyu Mbeya leo, Hiace ambayo ilikuwa imebeba abiria imepata ajali kwa kutumbukia mtoni, Kamanda wa Polisi Mbeya, RPC Ahmed Msangi amethibitisha kwamba watu 19 wamefariki kutokana na ajali hiyo.


Ajali MBY
ajali MbeyaAjali za Tanzania kwenye vichwa vya habari zimezidi kuongezeka, leo April 17 2015 ajali nyingine imetokea Mbeya baada ya gari la abiria kupoteza mwelekeo na kuingia mtoni Mbeya.

ajali 2
ajali 3
Ajali 4

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...