Thursday, 27 September 2018

EURO 2024 kuchezwa UJERUMANI

Hii ni mara ya kwanza Ujerumani kuandaa michuano ya Euro tangu mwaka 1988
UJERUMANI imeteuliwa kuwa wenyeji wa fainali za kombe la mataifa ya ULAYA (EURO) mwaka 2024 baada ya kuishinda UTURUKI waliokuwa wakiwania nafasi hiyo pia.

Mataifa hayo mawili yaliingia katika kinyang’anyiro cha mwisho kuwania wenyeji huo kabla ya kura zilizopigwa mjini NYON nchini USWISS yalipo makao makuu ya shirikisho la soka barani ulaya UEFA ambao UJERUMANI wameibuka kidedea.

Nahodha wa zamani wa Ujeruman Philip Lahm ameteuliwa kuwa balozi wa michuano hiyo

Wenyeji huo unamaana kuwa kwa mara ya kwanza UJERUMANI itahodhi mashindano ya ulaya kama taifa MOJA baada ya iliyokuwa UJERUMANI MAGHARIBI kuandaa fainali kama hizo mwaka 1988 huku UTURUKI ikisalia bila kuandaa mashindano yoyote makubwa ya mpira katika historia yao.

Ujerumani waliomba kuanda michuano hiyo mwaka 2008, 2012, 2016 bila mafanikio

Kabla ya kupata wenyeji huo UJERUMANI iliwahi kuomba kuandaa faionali za EURO mwaka 2008, 2012 na 2016 ambako zote hawakufanikiwa lakini pia waliomba kuandaa michuano ya OLYMPIC ya mwaka 2020 ambayo nayo hawakufanikiwa baada ya kuzidiwa na JAPAN na walifanikiwa kuwa wenyeji wa fainali za kombe la FIFA la duinia za mwaka 2006.

VAR kutumika ligi ya mabingwa ulaya


Shirikisho lao soka barani Ulaya (UEFA) limesema litaanza kutumia Maamuzi ya msaada wa video (VAR) kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwenye msimu wa 2019-2020.

Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin amesema shirikisho lake litakuwa na mfumo ila wa kutumia VAR ili iweze kutenda haki kwa kila mtu pia watatoa mafunzo ya uhakika kwa waamuzi wote ili waweze kuelewa mfumo huo wa VAR.

Pia VAR itatumika kwenye mchezo wa Super Cup na michuano ya Ulaya ya mwaka 2020 pamoja na michuano ya Europa kwenye msimu wa 2020-2021.

VAR ilikuwa kivutio kwenye kombe la dunia huko Russia

Mfumu  wa kutumia msaada wa video  kutoa maamuzi hasa ya utata yalivutia wengi kwenye michuano ya kombe la Dunia ya mwaka huu iliyofanyika nchini Russia na ligi kubwa barani Ulaya zinatumia mfumo huo isipokuwa ligi kuu ya England.

Ronaldo kuivaa Man United

Ronaldo alioneshwa kadi nyekundu dhidi ya Valencia 

Nyota wa timu ya Juventus, Cristiano Ronaldo atacheza mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya timu yake ya zamani ya Manchester United baada ya shirikikisho la soka barani Ulaya kumpa adhabu ya kukosa mchezo mmoja.

Cristiano Ronaldo alitolewa kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Valencia ya Hispania ambapo Juventus ilishinda kwa bao mbili kwa bila.

Ronaldo atacheza dhidi ya Man Utd baada ya adhabu kupunguzwa

Hiyo ilikuwa kadi nyekundi ya kwanza kwa Ronaldo kwenye michuano hiyo ya Ulaya na kama angeongezewa adhabu na UEFA basi angekosa michezo yote miwili dhidi ya Manchester United.

Kwa maamuzi hayo ya UEFA sasa Ronaldo atakosa mchezo mmoja tu dhidi ya Young Boys ya Uswiss utakaocheza Octoba pili.

UJERUMANI itashinda kombe la dunia - LOW

Kocha wa Ujerumani Joachim Low
Kocha wa timu ya taifa ya UJERUMANI, JOACHIM LOW anasema kikosi cha DFB kinauwezo wa kushinda tena kombe la FIFA la dunia baada ya morali kurejea ndani ya timu hiyo.

Mabingwa hao wa dunia mwaka 2014 waliishia katika hatua ya makundi kwenye fainali za kombe la FIFA la dunia mwaka huu kule nchini RUSSIA baada ya kutandikwa mabao MAWILI kwa BILA na KOREA KUSINI.

Ujerumani waliondolewa katika hatua ya makundi kombe la dunia 2018

LOW anasema wakati Fulani walikosa hamasa waliyokuwa nayo huko nyuma huku baadhi ya wachezaji wakiwa nje ya kiwango chao kitendo kilichowashangaza na wamejifunza kutokana na hilo na wamelifanyia kazi.

LOW aliajiriwa kukinoa kikosi cha UJERUMANI mwaka 2006 na kabla ya kuanza kwa fainali za kombe la FIFA la dunia kule RUSSIA aliongezewa kandarasi mpya itakayomfanya kuhudumu katika wadhifa huo hadi mwaka 2022 katika fainali za kombe la FIFA la dunia kule nchini QATAR.

Ujerumani walishinda kombe la dunia mwaka 2014

Mbali na kuiongoza UJERUMANI kushinda kombe la FIFA la dunia mwaka 2014 kocha huyo pia alikiongoza kikosi hicho kufika fainali ya kombe la mataifa ya ulaya mwaka 2008 na mwaka 2010 waliishia katika hatua ya nusu fainali kwenye fainali za kombe la FIFA la dunia hatua aliyowaongoza kufika katika fainali za Euro za mwaka 2012 na 2016.

RAMSEY kutimka ARSENAL

Aaron Ramsey akitekeleza majukuma yake uwanjani
Kiungo wa ARSENAL, AARON RAMSEY huenda akatimka katika klabu hiyo baada ya mazungumzo ya kumuongezea kandarasi mpya kugonga mwamba.

Mazungumzo kati ya mchezaji huyo na mabosi wa ARSENAL juu ya kandarasi mpya ya miaka MINNE awali yalielezwa kufikia pazuri lakini saa chache kabla ya kutiliwa saini ARSENAL walijitoa.

 Mkataba wa sasa wa RAMSEY na ARSENAL unafikia tamati JUNE 30 mwakani ambapo mchezaji huyo atakuwa huru au ARSENAL waamue kumuuza mwezi JANUARY kama wanataka kupata chochote kutoka mchezaji huyo.

Ramsey aliifungia Arsenal goli la ushindi kwenye fainali ya FA Cup 2017 dhidi ya Chelsea

Pamoja na yote hayo kiungo huyo wa kimataifa wa WALES atakuwa huru kuingia makubaliano yoyote ya awali na klabu nyingine kuanzia mwezi JANUARY mwakani kwani mkataba wake utakuwa umebakiza miezi sita ambayo kisheria unaruhusiwa kufanya makubaliano na timu nyingine.

RAMSEY alijiunga na GUNNERS mwaka 2008 kwa kitita cha paundi milioni 4.8 akitokea CARDIFF CITY na ndiye mchezaji wa ARSENAL aliyehudumu kipindi kirefu na kufunga bao la ushindi katika fainali ya kombe la FA mwaka 2017 dhidi ya CHELSEA.

Ramsey alijiunga na Arsenal mwaka 2008 akitokea Cardiff City akiwa na miaka 17

Hata hivyo RAMSEY alikuwa mchezaji wa ziada katika ushindi wa ARSENAL wa mabao MATATU kwa MOJA dhidi ya BRENTFORD kwenye kombe la CARABAO siku ya Jumatano ambapo aliingia kwenye dakika ya 84 kitendo kilichoongeza maneno kuwa huenda akatimka.

AJIB, KICHUYA na NYONI wakatwa STARS

Kocha wa Taifa Stars Emanuel Amunike
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" EMMANUEL AMUNIKE ametangaza kikosi cha wachezaji 30 watakaoingia kambini Septemba 30 kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Africa dhidi ya CAPE VERDE. 

Katika kikosi hicho Kocha AMUNIKE amewaongeza wachezaji watano (5) kutoka kwenye kikosi cha awali ambao ni JONAS MKUDE, SHOMARI KAPOMBE, na JOHN BOKO kutoka SIMBA pamoja na FEISAL SALUM wa YANGA na ABDALLAH KHERI wa AZAM FC.

Mlinzi wa mkongwe Erasto Nyoni hajaitwa kikosi cha Stars

Amunike hajawajumuisha beki ERASTO NYONI na viungo SHIZA KICHUYA wa SIMBA na IBRAHIM AJIB wa YANGA katika kikosi chake cha wachezaji 30 kuelekea mechi hizo mbili za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya CAPE VERDE.

Taifa Stars watakuwa wageni wa CAPE VERDE katika mchezo wa Kundi L wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON Oktoba 12 mjini PRAIA kabla ya kurejea Dar es Salaa kwa mchezo wa marudiano na wapinzani wao hao utakaopigwa Oktoba 16 kwenye dimba la taifa.

Ibrahim Ajib amekuwa na kiwango bora sana msimu huu lakini hajaitwa timu ya taifa


Kwa kiasi kikubwa kocha huyo MNIGERIA ameita wachezaji waliomsaidia kupata sare ya ugenini Septemba 8 mjini KAMPALA dhidi ya UGANDA.

Tanzania inashika nafasi ya tatu katika Kundi L ikiwa na pointi mbili baada ya kutoka sare katika mechi zake mbili za mwanzo, wakitoka 1-1 na Lesotho nyumbani mwaka jana na 0-0 na Uganda ugenini mapema mwezi huu.

Kiungo msumbufu na mnyumbulifu Shiza Kichuya ameachwa Stars

Uganda wanaendelea kuongoza Kundi hilo kwa pointi zao nne, wakifuatiwa na Lesotho wenye pointi mbili sawa na Tanzania na mabao mawili ya kufunga, wakati Cape Verde wanashika mkia wakiwa na  pointi yao moja. 

Kihistoria Tanzania imecheza fainali moja tu za AFCON, mwaka 1980 nchini Nigeria, enzi hizo zikijulikana kama Fainali za kombe la Mataifa Huru ya Afrika. 

AZAM FC, WAGOSI WA KAYA Kukinukisha leo


Ligi kuu TANZANIA BARA inaendelea leo ijumaa kwa michezo miwili katika majiji ya TANGA na DSM.

kwenye dimba la Mkwakwani huko jijini Tanga wagosi wakaya COASTAL UNION wanaoshika nafasi ya TISA kwenye msimamo wakiwa na alama TISA watakuwa nyumbani kuwaalika vinara wa ligi hiyo, Mbao FC ya jijini Mwanza wenye aklama 13 mchezo utakaochezwa majira ya saa kumi jioni.

Mchezo wa mwisho utawakutanisha wenyeji AZAM FC waliopo kwenye nafasi ya TANO wakiwa na alama 11 dhid ya wanapaluhengo LIPULI FC ya IRINGA wanaoshika nafasi ya 13 wakiwa wamejikusanyia alama SABA katika michezo MITANO waliyocheza mpaka sasa.

Chamazi Complex uwanja wa Azam Fc

Endapo AZAM FC wataibuka na ushindi watakwea hadi kileleni kwenye msimamo wa ligi kwa kufikisha alama 14 ambazo itakuwa ni alama MOJA dhidi ya MTIBWA SUGAR na MBAO FC wenye alama 13 kila mmoja.

Katika michezo iliyochezwa hapo jana, MTIBWA SUGAR wamepanda hadi kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kuilaza MWADUI FC kwa bao MOJA kwa BILA katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la MANUNGU huko TURIANI.

Matokeo ya Michezo miwili iliyochezwa Sept 27

Katika mchezo mwingine wazee wa kupapasa RUVU SHOOTING wamefufukua baada ya kuilaza AFRICA LYON kwa bao MOJA kwa BILA lililofungwa na SAID MUSSA kwenye dakika ya 50 ya mchezo huo.

Ushindi huo umeifanya RUVU SHOOTING kufikisha pointi TANO  baada ya kucheza michezo SITA  na huu ni ushindi wao wa kwanza kwenye msimu huu wa ligi kuu Tanzania Bara.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...