![]() |
Hii ni mara ya kwanza Ujerumani kuandaa michuano ya Euro tangu mwaka 1988 |
UJERUMANI imeteuliwa kuwa wenyeji wa fainali za kombe la mataifa ya ULAYA (EURO) mwaka 2024 baada ya kuishinda UTURUKI waliokuwa wakiwania nafasi hiyo pia.
Mataifa hayo mawili yaliingia katika kinyang’anyiro cha mwisho kuwania wenyeji huo kabla ya kura zilizopigwa mjini NYON nchini USWISS yalipo makao makuu ya shirikisho la soka barani ulaya UEFA ambao UJERUMANI wameibuka kidedea.
![]() |
Nahodha wa zamani wa Ujeruman Philip Lahm ameteuliwa kuwa balozi wa michuano hiyo |
Wenyeji huo unamaana kuwa kwa mara ya kwanza UJERUMANI itahodhi mashindano ya ulaya kama taifa MOJA baada ya iliyokuwa UJERUMANI MAGHARIBI kuandaa fainali kama hizo mwaka 1988 huku UTURUKI ikisalia bila kuandaa mashindano yoyote makubwa ya mpira katika historia yao.
![]() |
Ujerumani waliomba kuanda michuano hiyo mwaka 2008, 2012, 2016 bila mafanikio |
Kabla ya kupata wenyeji huo UJERUMANI iliwahi kuomba kuandaa faionali za EURO mwaka 2008, 2012 na 2016 ambako zote hawakufanikiwa lakini pia waliomba kuandaa michuano ya OLYMPIC ya mwaka 2020 ambayo nayo hawakufanikiwa baada ya kuzidiwa na JAPAN na walifanikiwa kuwa wenyeji wa fainali za kombe la FIFA la duinia za mwaka 2006.
No comments:
Post a Comment