Thursday, 27 September 2018

RAMSEY kutimka ARSENAL

Aaron Ramsey akitekeleza majukuma yake uwanjani
Kiungo wa ARSENAL, AARON RAMSEY huenda akatimka katika klabu hiyo baada ya mazungumzo ya kumuongezea kandarasi mpya kugonga mwamba.

Mazungumzo kati ya mchezaji huyo na mabosi wa ARSENAL juu ya kandarasi mpya ya miaka MINNE awali yalielezwa kufikia pazuri lakini saa chache kabla ya kutiliwa saini ARSENAL walijitoa.

 Mkataba wa sasa wa RAMSEY na ARSENAL unafikia tamati JUNE 30 mwakani ambapo mchezaji huyo atakuwa huru au ARSENAL waamue kumuuza mwezi JANUARY kama wanataka kupata chochote kutoka mchezaji huyo.

Ramsey aliifungia Arsenal goli la ushindi kwenye fainali ya FA Cup 2017 dhidi ya Chelsea

Pamoja na yote hayo kiungo huyo wa kimataifa wa WALES atakuwa huru kuingia makubaliano yoyote ya awali na klabu nyingine kuanzia mwezi JANUARY mwakani kwani mkataba wake utakuwa umebakiza miezi sita ambayo kisheria unaruhusiwa kufanya makubaliano na timu nyingine.

RAMSEY alijiunga na GUNNERS mwaka 2008 kwa kitita cha paundi milioni 4.8 akitokea CARDIFF CITY na ndiye mchezaji wa ARSENAL aliyehudumu kipindi kirefu na kufunga bao la ushindi katika fainali ya kombe la FA mwaka 2017 dhidi ya CHELSEA.

Ramsey alijiunga na Arsenal mwaka 2008 akitokea Cardiff City akiwa na miaka 17

Hata hivyo RAMSEY alikuwa mchezaji wa ziada katika ushindi wa ARSENAL wa mabao MATATU kwa MOJA dhidi ya BRENTFORD kwenye kombe la CARABAO siku ya Jumatano ambapo aliingia kwenye dakika ya 84 kitendo kilichoongeza maneno kuwa huenda akatimka.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...