Thursday, 27 September 2018

UJERUMANI itashinda kombe la dunia - LOW

Kocha wa Ujerumani Joachim Low
Kocha wa timu ya taifa ya UJERUMANI, JOACHIM LOW anasema kikosi cha DFB kinauwezo wa kushinda tena kombe la FIFA la dunia baada ya morali kurejea ndani ya timu hiyo.

Mabingwa hao wa dunia mwaka 2014 waliishia katika hatua ya makundi kwenye fainali za kombe la FIFA la dunia mwaka huu kule nchini RUSSIA baada ya kutandikwa mabao MAWILI kwa BILA na KOREA KUSINI.

Ujerumani waliondolewa katika hatua ya makundi kombe la dunia 2018

LOW anasema wakati Fulani walikosa hamasa waliyokuwa nayo huko nyuma huku baadhi ya wachezaji wakiwa nje ya kiwango chao kitendo kilichowashangaza na wamejifunza kutokana na hilo na wamelifanyia kazi.

LOW aliajiriwa kukinoa kikosi cha UJERUMANI mwaka 2006 na kabla ya kuanza kwa fainali za kombe la FIFA la dunia kule RUSSIA aliongezewa kandarasi mpya itakayomfanya kuhudumu katika wadhifa huo hadi mwaka 2022 katika fainali za kombe la FIFA la dunia kule nchini QATAR.

Ujerumani walishinda kombe la dunia mwaka 2014

Mbali na kuiongoza UJERUMANI kushinda kombe la FIFA la dunia mwaka 2014 kocha huyo pia alikiongoza kikosi hicho kufika fainali ya kombe la mataifa ya ulaya mwaka 2008 na mwaka 2010 waliishia katika hatua ya nusu fainali kwenye fainali za kombe la FIFA la dunia hatua aliyowaongoza kufika katika fainali za Euro za mwaka 2012 na 2016.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...