![]() |
Ronaldo alioneshwa kadi nyekundu dhidi ya Valencia |
Nyota wa timu ya Juventus, Cristiano Ronaldo atacheza mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya timu yake ya zamani ya Manchester United baada ya shirikikisho la soka barani Ulaya kumpa adhabu ya kukosa mchezo mmoja.
Cristiano Ronaldo alitolewa kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya Valencia ya Hispania ambapo Juventus ilishinda kwa bao mbili kwa bila.
![]() |
Ronaldo atacheza dhidi ya Man Utd baada ya adhabu kupunguzwa |
Hiyo ilikuwa kadi nyekundi ya kwanza kwa Ronaldo kwenye michuano hiyo ya Ulaya na kama angeongezewa adhabu na UEFA basi angekosa michezo yote miwili dhidi ya Manchester United.
Kwa maamuzi hayo ya UEFA sasa Ronaldo atakosa mchezo mmoja tu dhidi ya Young Boys ya Uswiss utakaocheza Octoba pili.
No comments:
Post a Comment