Shirikisho lao soka barani Ulaya (UEFA) limesema litaanza kutumia Maamuzi ya msaada wa video (VAR) kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwenye msimu wa 2019-2020.
Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin amesema shirikisho lake litakuwa na mfumo ila wa kutumia VAR ili iweze kutenda haki kwa kila mtu pia watatoa mafunzo ya uhakika kwa waamuzi wote ili waweze kuelewa mfumo huo wa VAR.
Pia VAR itatumika kwenye mchezo wa Super Cup na michuano ya Ulaya ya mwaka 2020 pamoja na michuano ya Europa kwenye msimu wa 2020-2021.
![]() |
VAR ilikuwa kivutio kwenye kombe la dunia huko Russia |
Mfumu wa kutumia msaada wa video kutoa maamuzi hasa ya utata yalivutia wengi kwenye michuano ya kombe la Dunia ya mwaka huu iliyofanyika nchini Russia na ligi kubwa barani Ulaya zinatumia mfumo huo isipokuwa ligi kuu ya England.
No comments:
Post a Comment