Thursday, 27 September 2018

AJIB, KICHUYA na NYONI wakatwa STARS

Kocha wa Taifa Stars Emanuel Amunike
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" EMMANUEL AMUNIKE ametangaza kikosi cha wachezaji 30 watakaoingia kambini Septemba 30 kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Africa dhidi ya CAPE VERDE. 

Katika kikosi hicho Kocha AMUNIKE amewaongeza wachezaji watano (5) kutoka kwenye kikosi cha awali ambao ni JONAS MKUDE, SHOMARI KAPOMBE, na JOHN BOKO kutoka SIMBA pamoja na FEISAL SALUM wa YANGA na ABDALLAH KHERI wa AZAM FC.

Mlinzi wa mkongwe Erasto Nyoni hajaitwa kikosi cha Stars

Amunike hajawajumuisha beki ERASTO NYONI na viungo SHIZA KICHUYA wa SIMBA na IBRAHIM AJIB wa YANGA katika kikosi chake cha wachezaji 30 kuelekea mechi hizo mbili za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya CAPE VERDE.

Taifa Stars watakuwa wageni wa CAPE VERDE katika mchezo wa Kundi L wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON Oktoba 12 mjini PRAIA kabla ya kurejea Dar es Salaa kwa mchezo wa marudiano na wapinzani wao hao utakaopigwa Oktoba 16 kwenye dimba la taifa.

Ibrahim Ajib amekuwa na kiwango bora sana msimu huu lakini hajaitwa timu ya taifa


Kwa kiasi kikubwa kocha huyo MNIGERIA ameita wachezaji waliomsaidia kupata sare ya ugenini Septemba 8 mjini KAMPALA dhidi ya UGANDA.

Tanzania inashika nafasi ya tatu katika Kundi L ikiwa na pointi mbili baada ya kutoka sare katika mechi zake mbili za mwanzo, wakitoka 1-1 na Lesotho nyumbani mwaka jana na 0-0 na Uganda ugenini mapema mwezi huu.

Kiungo msumbufu na mnyumbulifu Shiza Kichuya ameachwa Stars

Uganda wanaendelea kuongoza Kundi hilo kwa pointi zao nne, wakifuatiwa na Lesotho wenye pointi mbili sawa na Tanzania na mabao mawili ya kufunga, wakati Cape Verde wanashika mkia wakiwa na  pointi yao moja. 

Kihistoria Tanzania imecheza fainali moja tu za AFCON, mwaka 1980 nchini Nigeria, enzi hizo zikijulikana kama Fainali za kombe la Mataifa Huru ya Afrika. 

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...